MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 15,923
- 40,246
Pamoja na kuwa boda boda zinaajiri vijana wengi, ila kuna kitu hakipo sawa namna zinavyofanya kazi
China wana flying taxies,, sisi tunapongezana kwa kuvunjana miguu, na mikono, kwa hayo machuma ya moto (bodaboda) na kuimarisha biashara ya majeneza, any way sio mbaya.Pamoja na kuwa boda boda zinaajiri vijana wengi, ila kuna kitu hakipo sawa namna zinavyofanya kazi
Shida ya nchi hii ni kutokuwa na utamaduni wa kufuata Sheria. Hao maafisa usafirisha mitandao wanapokamatwa kwa wrong parking wanakuwa wamepark sehemu zilizoruhisiwa? Mara nyingi ni hapana. Hapo wanakuwa wametenda kosa. Lakini pia swali lingine ninalojiuliza jiji limetenga parking kwa ajili yao? Inawezekana jibu likawa hapana. Lakini hapo hapo wametoa vibali kwa ajili ya shughuli hizo za usafirishaji. Unaruhusu watu wa operate mjini lakini haujawapangia sehemu ya kupark unawakamata na kuwatoza fine. Hii haijakaa sawaMaafisa usafirishaji wa mtandao, maarufu kama bodaboda za mtandao, wamefunga barabara katika eneo la Chuo cha Biashara (CBE) Posta, Jijini Dar es salaam, wakipinga vitendo vya Maafisa wa Jiji kuwakamata wanapoingia katikati ya Jiji kuwachukua abiria walioita usafri kupitia programu za usafirishaji.
Madereva hao, ambao wamedai kuwa hukamatwa mara kwa mara wanapokwenda kuwachukua abiria waliowaagiza kupitia programu za usafirishaji ambapo wameeleza kuwa baada ya kukamatwa hupelekwa katika Ofisi za Jiji huandikiwa kosa la kupaki sehemu isiyoruhusiwa (Wrong Parking) na kutozwa faini ya shilingi 70,000.
“Tunalipa ada kwa kampuni za usafirishaji wa mtandao na tunafuata masharti yote ya kazi. Lakini kila tunapokwenda kumchukua abiria tunaishia kukamatwa kwa madai ya ‘Wrong Parking’. Askari wanatupeleka ofisi za Jiji na tunatakiwa kulipa shilingi 70,000. Tumechoka na hali hii.
Kama hatutakiwi kufanya kazi katikati ya jiji, basi waelekezwe kampuni za usafirishaji wa mtandao zifunge huduma hizo katika eneo hilo ili tusiendelee kupata hasara,” amesema mmoja wa madereva wa teksi za mtandao
okay,
I hope responsible authority is going to take every measure possible to sort the little issue.
ni muhimu sana kua wastahilivu na wenye subra, everything gonna be alright as soon as possible 🐒
I think it's over.Who are you?

just relax,Wewe vuvuzela ungenyamaza tu.
Umaskini wa Mtanganyika ndiyo furaha ya Chama chako.