Maafisa wa kampuni ya Barrick wakamatwa nchini Mali

Strong ladg

Senior Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
170
Reaction score
445
Maafisa wanne wa juu wa kampuni ya Barrick wamekamatwa na serikali ya nchini Mali kwa tuhuma za kampuni hiyo kutokulipa kodi stahiki.

Maafisa hao wanashikiliwa tangu Novemba 26 mwaka 2024 na watapelekwa mahakamani iwapo serikali ya kijeshi ya Mali na Kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Barrick hawatafikia muafaka juu ya madai hayo.

Katika sakata kama hilo, wiki chache zilizopita serikali ya kijeshi ya Mali iliwakamata maafisa wa juu ikiwemo afisa mtendaji mkuu ( CEO) wa Kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Resolute kutoka nchini Australia ambapo maafisa hao walishikiliwa hadi kampuni hiyo ilipokubali kulipa malimbikizo ya kodi pamoja na faini ambavyo kwa pamoja vilifikia kiasi cha dollar za Marekani milioni 160.

Kampuni hiyo ililipa nusu ya fedha hizo ambazo ni kiasi cha dollar milioni 80 Ili maafisa hao waachiliwe na kuahidi kulipa kiasi kilichobakia ndani ya miezi michache ijayo.

Vyanzo: Tovuti ya Barrick, ABC NEWS, AFRICAN STREAM.
 
Tulikubaliana kwenye kikao cha mwisho - taarifa bila picha au video ni uzushi kama uzushi mwingine. Mbona sasa?
 
Maafisa wanne wa juu wa kampuni ya Barrick wamekamatwa na serikali ya nchini Mali kwa tuhuma za kampuni hiyo kutokulipa kodi stahiki.

Maafisa hao wanashikiliwa tangu Novemba 26 mwaka 2024 na watapelekwa mahakamani iwapo serikali ya kijeshi ya Mali na Kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Barrick hawatafikia muafaka juu ya madai hayo.

Katika sakata kama hilo, wiki chache zilizopita serikali ya kijeshi ya Mali iliwakamata maafisa wa juu ikiwemo afisa mtendaji mkuu ( CEO) wa Kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Resolute kutoka nchini Australia ambapo maafisa hao walishikiliwa hadi kampuni hiyo ilipokubali kulipa malimbikizo ya kodi pamoja na faini ambavyo kwa pamoja vilifikia kiasi cha dollar za Marekani milioni 160.

Kampuni hiyo ililipa nusu ya fedha hizo ambazo ni kiasi cha dollar milioni 80 Ili maafisa hao waachiliwe na kuahidi kulipa kiasi kilichobakia ndani ya miezi michache ijayo.

Vyanzo: Tovuti ya Barrick, ABC NEWS, AFRICAN STREAM.
Mali Issues Arrest Warrant for Barrick Gold CEO Mark Bristow, jamaa hawana utani kabisa
 
Back
Top Bottom