DOKEZO Maafisa wa LATRA Morogoro wanalazimisha nilipe Faini kwa cash au Lipa Namba, eti hawana Control Number

DOKEZO Maafisa wa LATRA Morogoro wanalazimisha nilipe Faini kwa cash au Lipa Namba, eti hawana Control Number

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Naomba ufafanuzi kutoka LATRA, juzi nilikamatwa na LATRA sijalipia Pikipiki yangu lakini wakati naomba Control Number wanasema natakiwa kulipa faini kwanza ambayo ni Sh 15,000 lakini cha ajabu hiyo faini hupewi Namba ya Malipo wanataka cash.

Tukio lilitokea Morogoro sehemu moja inaitwa Kiroka. Nikawaambia sina cash nipeni namba ya simu niwatumie mmoja akasema hizi namba zetu hazitakiwi kuingia hela nikawauliza kwani hazipo kwenye mfumo?

Mwingine akaitikia weka kwenye Lipa Namba, yaani kila tunapokwenda ni mazingira ya rushwa tu zimetawala na muamala nimeu screenshot kama ushahidi.

Tulikamatwa wengi ila Mimi tu ndiyo nililipa kupitia Lipa Namba wengine walitoa cash.
 
Bora wewe. Mimi ni ilikuwa mtendaji wa moshi pale soko la maimoria, nilipigwa faini 50000/= alafu mtendaji akaniambia nilipe kwa kumtumia afisa mazingira wake kwa namba ya simu. Niliwaomba control number nilipe faini iyo wakasema faini zinalipwa kwenye namba ya simu🙌🙌🙌 risiti iyo apo


75f489fc-6f5b-4d7b-a570-0f0ee13884bb.jpeg
 
Back
Top Bottom