Maafisa wa Marekani waduwazwa na silaha 'ngeni' za Urusi

Sikirimimimasikini

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2019
Posts
2,926
Reaction score
15,634
Wanaintelijensia wa Marekani wamesema kuwa Russia inatumia silaha za ajabu nchini Ukraine.

Wanainteligensia hao wamebaini kuwa makombora ya balistiki (Iskandar-M short range ballistic missiles) yanayovurumishwa na majeshi ya Russia nchini Ukraine yameongezewa vionjo au vikorombwezo fulani vipya, tofauti na hapo zamani yalivyozoeleka.

Vikorombwezo hivyo vigeni, hutolewa na makombora hayo pale yanapotambua yametagetiwa na mifumo ya ulinzi wa anga wa adui. Vikorombwezo hivyo huzivuruga rada za mifumo ya ulinzi wa anga ya jeshi la Ukraine (air defense systems), na pia huyachanganya makombora yanayotumwa (na Ukraine) kudungua silaha hizo.

Vikorombwezo hivyo vipya ndivyo vinavyopelekea mifumo ya ulinzi wa anga ya jeshi la Ukraine na silaha za kulinda anga hilo kushindwa kuyadungua makombora ya Russia.

======

 
ngapi ngapi huko?
Hata Kama mnapigwa msione aibu kusema.
Vita haina mwenyewe
 
Tuombe Mungu vita viishe,uchumi wa dunia utatikisika sana kwa hii vita...
 
Wiki ya tatu hii hizo silaha bado hazijaikamata Kyiv
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…