Elitwege
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 5,294
- 10,970
Tulishuhudia mkuu wa mkoa wa Dar Bw. Amos Makala alipoapishwa tu alitoka mbio mbio kwenda kutangaza oparation ya kuondoa machinga na ombaomba wote ili jiji lirudi kwenye hadhi yake ya usafi, lakini mpaka leo agizo hilo halijatekelezwa.
Makala alifanya mpaka kikao na wakuu wa wilaya, madiwani na wenyeviti wa mitaa kuwapa maagizo ili kuwezesha kuwatoa wamachinga, mpaka magari yalianza kupita mitaani yakitangaza wamachinga wote waondoke lakini mpaka leo kimya shughuli zinaendelea kama kawaida.
Haikupita muda kamati ya Corona iliyoundwa na rais Samia ikaja na mapendekezo ya kuwataka wanachi wote kuvaa barakoa na kufanya social distance, pia walimtaka waziri wa afya atangaze idadi ya wagonjwa wa corona wanaopatikana kila siku ,pia wiki mbili baadae chama cha madaktari Tanzania kikatoa tamko la kuwataka watanzania kuepuka mikusanyiko, kunawa mikono na kuvaa barakoa muda wote.
Freeman Mbowe na Chadema pia mapema kabisa alitangaza kuwa yeye amechanjwa na kuwataka watanzania kuvaa barakoa na kujiandaa kupokea chanjo, maagizo yote hayo yamepuuzwa na wananchi mpaka sasa.
Pita sabasaba, kwenye mwendokasi, Kariakoo wananchi wanaendelea na maisha yao kama kawaida kana kwamba kamati ya Corona na chama cha madaktari hawajatoa tamko lolote!
Chanzo cha maagizo haya kupuuzwa nini? Je, ni Kauli za Magufuli bado zinaendelea kuishi kwenye ubongo wa watu?
Baadhi ya wananchi wamehojiwa kuhusu maagizo hayo wamesema maagizo hayo hayana tija yoyote zaidi ya kutafuta namna ya kuwatia hofu watu.