Waliodhani mama atakimbizwa mbio na presha za mabeberu kutuvalisha barakoa na kutupima pima pima pima na kututishia kwa takwimu zitokanazo na vipimo batili vya corona watakuwa wamekosea sana!! Waliodhani mama atawageuka wamachinga na kuwafanya kama raia wa daraja la chini watakuwa wamekoseà sana!! Mahesabu ya mama ni makali!! Kuhusu corona tunaendelea na tahadhari kwa mujibu wa maelekezo ya wataalamu bila shinikizo la nje!! Kwanza tuko vizuri kwa kuwa tulimtanguliza Mungu! Watanzania wako salama! Vinginevyo wanaokesha wakiitafuta corona hata kwa tochi wangeshapiga makelele sana Hilo wimbi la tatu liishie huko huko walikoiendekeza corona! Mipaka ya Tanzania yote angani, ardhini na majini inalindwa kwa damu ya Yesu kutokana na maombi ya watanzania!! Wanaoitakia mabaya nchi yetu watasubiri sana!! Waliotabiri miili kuokotwa barabarani saa hii wako kimyaa utafikiri hawakuwahi kusema hayo.
Kama watanzania tusipoweza kumshukuru Mungu kila siku kwa alivyotuponya na kutukinga na corona tutakuwa watu wa ajabu sana!!!