Maajabu 8 ya mkoa wa Mara

Maajabu 8 ya mkoa wa Mara

Ila ukeketaji ndio jambo linalotia doa mkoa huu, cha ajabu zaidi, huko mara mwanamke anaweza kumuoa mwanamke mwenzie, wanaita "Nyumba Ntobhu'.
Ila elewa hii sio ndoa ya ushoga, hii ni mira tu ya mwanamke kumchumbia na kumtolea mahari mwanamke mwenzie ili aweze kumliki na kumletea uzao( yani ukiolewa nyumba ntobhu huyo mwanamke alie kuoa atakuchagulia ama kukuruhusu kuwa na mahusiano na mwanaume flani ili uweze kupata ujauzito na watoto watakao zaliwa wataesabika niwa huyo mwanamke alie kuoa na sio wa mwanaume aliekupa ujauzito) hii ufanywa na wamama wasio weza kuzaa ama umri wa kuzaa umepita na wanaitaji mtoto wa kurithi mali zao na majina yao
 
Hayo makabila yoote uliyoorodhesha ni makabila mawili tuu ambayo ni ya kikurya yanayoongea mura na makabila ya kijita wa chasugu.
 
Mkoa wa Mara unapatikana Kaskazini mashariki mwa nchi ya Tanzania. Kwa mujibu wa tovuti ya mkoa, kiutawala Mkoa umegawanyika katika Wilaya 6 ambazo ni; Musoma, Butiama, Bunda, Serengeti, Tarime na Rorya zenye Halmashauri 9 ambazo ni; Manispaa ya Musoma, Butiama, Bunda, Bunda Mji, Serengeti, Tarime, Rorya na Tarime Mji. Makao makuu ya Mkoa wa Mara ni Musoma na jina "Mara" ni kwa sababu ya Mto Mara ulio mkubwa kuliko wote katika mkoa huo.


Katika Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012, Mkoa wa Mara ulikuwa na watu takribani 1,743,830. Kijiografia mkoa umepakana na mikoa jirani ya Simiyu upande wa kusini, Arusha upande wa kusini-mashariki, upande wa Magharibi mkoa umepakana na ziwa Viktoria na Kenya kwa upande wa Mashariki.

Nadhani hadi kufikia hapo huwezi kupotea endapo utahitaji kutembelea Mkoa wa Mara hasa kushuhudia maajabu nitakayoyaelezea hapa chini. Turudi sasa kwenye maajabu 10 yanayopatikana mkoa wa Mara.

1. Muasisi wa Taifa la Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa ni mzaliwa wa mkoa wa Mara;
Nisingependa kumzungumzia sana mtu huyu ambaye kamwe habari zake haziwezi kusahaulika kwenye Historia ya Taifa la Tanzania vizazi na vizazi. Ninayo imani kuwa karibia asilimia 100 ya watu tulio humu Jamii forum, tutakuwa tunafahamu kuwa Mwalimu Nyerere alizaliwa wilaya ya Butiama ambapo ndipo hata makumbusho yake yanapatikana huko.

2. Hifadhi ya wanyama ya Serengeti:

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti yenye ukubwa wa kilometa za mraba 14,763 ilianzishwa mwaka 1951, ni Hifadhi ya Taifa ya pili kwa ukubwa nchini ikitanguliwa na hifadhi ya Taifa ya Ruaha yenye ukubwa wa kilometa za mraba 20,226 (Rejea tovuti ya TANAPA).

Licha ya kwamba hifadhi hii inapatikana mikoa mingine ya Tanzania lakini sehemu kubwa ya hifadhi hii inapatikana katika mkoa wa Mara. Kama ulikuwa hujui basi jua kuwa hii ni mbuga inayoheshimika kama moja ya urithi wa dunia na Shirika la umoja wa Mataifa linajishughulisha na masuala ya elimu, utamaduni na Sayansi (UNESCO). Hii ndiyo hifadhi maarufu zaidi Afrika japo zipo hifadhi zingine tena kubwa kuliko Serengeti lakini bado zinasalimu hapa.

3. Kuwepo kwa kanda maalumu (Mkoa wa kipolisi):
Huwezi kuamini hapa nchini ukitoa mkoa wa Dar es Salaam peke yake ila kanda maalumu nyingine inapatikana mkoa wa Mara tena kwenye wilaya mbili (Kanda maalumu ya Tarime-Rorya). Hakika hili ni ajabu ambalo linafikirisha na sababu zake yawezekana zinajulikana wazi au hazijulikani sana kwa wengi wetu.

4. Kuwepo kwa idadi kubwa ya wasomi:
Wengi watabisha ila wachache watakubali, kiuhalisia ukiutoa mkoa wa Kilimanjaro na Kagera basi mkoa wa Mara ni mkoa wenye idadi kubwa sana ya wasomi tena wa kiwango cha juu. Hivi juzi katika jimbo la Musoma vijijini peke yake walijitokeza Maprofesa 7 hapo bado majimbo mengine, achana na wale ambao hawakutia nia. Bado kuna majimbo mengine jumlisha na wale wenye elimu chini ya profesa.

Kuna mtu aliwahi kuandika uzi fulani humu Jf unaowahusu wasomi wa mkoa wa Mara nadhani ukiupata pia unaweza kukupa mwanga fulani.

5. Idadi ya makabila mengi:
Sikia hii, mkoa wa Mara unayo makabila zaidi ya 25 ya Kibantu na Kiniloti. Tofauti na watu wengi wajuavyo kwamba Wakuria (Wakurya) ndiyo kabila pekee, hii siyo kweli na sababu ya kuendana kwa matamshi ni kwa sababu ya kuingiliana tu wataalamu wa Kiswahili wanaelewa kuhusu "lahaja". Kwa msaada wa wengine, lahaja ni tofauti ndogondogo zinazojitokeza kwenye lugha yenye asili moja.

Mara nyingi huwa mtu akisema anatokea Mara basi watu hurahisha kwa kusema kuwa mtu huyo atakuwa Mkuria kitu ambacho sio ukweli. Tazama baadhi ya makabila yaliyopo mkoa wa Mara;
Waluo

Wajita

Waruri

Wazanaki

Wakurya

Wakabwa

Wakiroba

Wasimbiti


Wakwaya

Wanata

Waikoma

Waisenye

Waikizu

Sizaki

Wadatooga

Wakine

6. Tohara bila ganzi;
Wamasai kutoka Arusha na maeneo ya Kenya nao wana utamaduni wa namna hii ni yawezekana yakawa maajabu yao ila mkoa wa Mara nao ni mkoa ambao sio wanaume wala wanawake hufanyiwa tohara. Mwaka huu 2020 utakuwa ni mwaka wa tohara kwa makabila mengi ya mkoa wa Mara. Waluo pekee ndiyo kabila kutoka Mara ambalo kwao kufanya tohara sio jambo la muhimu kukamilisha mila na desturi ila wanafanya tohara hospitalini tu kama yalivyo makabila mengine.

KITU CHA AJABU KWENYE TOHARA;
-Hutakiwi kutikisika wala kuonesha dalili yoyote ya kuogopa au kulia na ukifanya hivyo utadharaulika hadi kwa watoto.

-Baadhi ya maeneo mengi ni ruksa mtu yeyote kuhudhuria isipokuwa shangazi, yaani chukulia mfano mwanaume unafanyiwa tohara basi jiandae kupata mashuhuda hadi wanawake.

-Eneo la kufanyia tohara huitwa "Kibaga" japo maeneo mengine hutamkwa vingine.

-Kirombe ni sherehe kabla ya tohara na ngoma yake ya jadi ni, rirandi, rithungu n.k.

-Mwanaume ukitahiriwa hospitalini unahesabika kama mwanamke na utapata tabu sana kwa vijana wenzio.

7. Panga ni kifaa muhimu kuliko jembe:
Japo kwa siku za hivi karibuni hali imekuwa tofauti kidogo lakini bado utamaduni huu upo. Maeneo mengi ya mkoa wa Mara usiogope kila kona hasa vijijini kukutana na mtu akiwa amebeba panga. Haijalishi mtu anakwenda shambani, disko, mpirani wengine hata kwenye mkutano wa kijiji akiwa na panga.

Kuna rafiki yangu mmoja daktari miaka 6 iliyopita alisema "akiwa Tarime, wagonjwa wengi walikuwa ni wale waliojeruhiwa na mapanga kuliko wagonjwa wengine". Hii sio sifa bali ni miongoni mwa maajabu ya mkoa wa Mara. Kwa wale wageni msiogope maana kwa sasa vyombo vya ulinzi na usalama vipo imara sana kudhibiti hali kama hii.

8. Kilimo cha bangi:
Hii nayo sio sifa wala kashfa bali ni maajabu, mkoa wa Mara ni miongoni mwa mikoa ambayo inajihusisha sana na ulimaji na hata wakati mwingine utumiaji wa mmea huu haramu hapa nchini. Mara nyingi, vyombo vya habari nchini vimekuwa vikiripoti sana kuendeshwa kwa kilimo hiki na hata uteketezwaji wake katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Mara. Soma hapa kwa uthibitisho zaidi... Mikoa 8 inayoongoza kwa kulima bangi Tanzania | East Africa Television

HITIMISHO

Mambo yote niliyoyaelezea nimeyafanyia utafiti na hata kupitia vyanzo vya uhakika ya habari. Siku zote kuna mtu anaweza kuwa anajua zaidi yangu na siogopi kukoselewa. Kitu cha msingi ni kuja na facts zako na kutumia lugha faafu bila kuvunja sheria za Jamii forum. Naomba kuwasilisha.......
Hizo ni koo sio makabila.
 
Tohara bila ganzi. Kama ka ngozi kakibanwa na zipu tuu ni msala. Sasa unapata picha ngozi yote inakatwa bila ganzi,, pah ngozi hamna unatulia
 
Hayo makabila yoote uliyoorodhesha ni makabila mawili tuu ambayo ni ya kikurya yanayoongea mura na makabila ya kijita wa chasugu.
Nimeongelea kuhusu lahaja, rejea kusoma
 
Wajaruo,washashi mbona hujawataja kwenye makabira
 
Ila ukeketaji ndio jambo linalotia doa mkoa huu, cha ajabu zaidi, huko mara mwanamke anaweza kumuoa mwanamke mwenzie, wanaita "Nyumba Ntobhu'.
Idadi ya jamii zinazokeketa ni kubwa kuliko jamii zisizokeketa! Fanya utafiti utabaki mdomo wazi..
 
Wajaruo,washashi mbona hujawataja kwenye makabira
Neno Washashi ni maarufu sana kwa "Wasukuma", kuhusu Waluo nimewataja na hilo neno "Warujuo" halipo katika lugha ya Kiswahili ila ni namna ambavyo watu wamezoea kuwaita hiyo. Waluo watakuja kuelezea mengi zaidi.
 
Back
Top Bottom