Maajabu 8 ya mkoa wa Mara

Maajabu 8 ya mkoa wa Mara

Mpakani?
Kwa nini mnufaika mkubwa wa mbuga hiyo ni mkoa wa Arusha na Mara inabaki mtazamaji tu?
Ni ujinga mkubwa uliofanywa na serikali zilizopita. Wachaga na watu wa kaskazini wameuhujumu sana mkoa wa Mara.

Kwa takwimu za Tanapa, zaidi ya 80% ya watalii wanaokuja nchi hii wanakuja kwa sababu ya mbuga ya serengeti, ukiona shilingi 100 ya utalii basi shilingi 80 inatokana na mbuga ya serengeti.

Serengeti ndio utalii wa nchi hii, bila serengeti hakuna utalii. Lakini cha ajabu serengeti hakuna miundombinu yoyote, hata chuo cha utalii au maliasili, yote haya yalifanyika makusudi kuhujumu mkoa wa Mara. Kuna kipindi hata makao makuu ya serengeti national park yalikua Arusha.

Kuna kipindi ilikua ujengwe uwanja wa ndege serengeti, wachaga wakasema ukijengwa uwanja wa ndege utau KIA, hivyo hiyo ikapigwa chini, Magufuli ndie kakomaa sasa wanajenga ila miaka yote huo uwanja ulikua unapingwa na kupigwa vita eti utadhoofisha KIA.

Juzi aliongea Msiba, kwenye magroup ya mkoa wa Mara hasa ya waliokua viongozi na ambao bado wapo walimshambulia sana ila alisema ukweli. Tumekua na wasomi na watu wenye madaraka wengi lakini hakuna walichosaidia mkoa wa Mara.
 
Hii pia...ndio mkoa ambao makabila yake ni mahasimu.inamaana kuwa wangoreme na wakurya haziivi wanagombana kila uchwao.chanzo kikubwa cha ugomvi ni wizi wa ng'ombe ambapo jamii ya kikurya inaamini kijana lazima atafute ng'ombe kwa kunyang'anya wenzake....wakati tunakuwa tulifundishwa namna ya kutumia upinde na mishale ili kujihami.
 
Nikisoma kuhusu hii [emoji115]huwa sielewi kuhusu Serengeti na uwiano wake kwa Mkoa wa Mara na Arusha.
Kimsingi hii mbuga ilikuwa moja na Ngorongoro!.. Kilichofanyika mbuga hii iligawanywa kutokana na mikoa ilimo. Kipande cha Mbuga upande wa Arusha ndio inaitwa Ngorongoro na kipande cha mbuga upande wa mkoa wa Mara na Simiyu ndio inaitwa Serengeti.. Kimsingi ngorongoro na serengeti ni mbuga moja na ndiyo mbuga kubwa kuliko zote hapa Tz. Lakini walipoweka mipaka ndii zikapungua ukubwa
 
Mpakani?
Kwa nini mnufaika mkubwa wa mbuga hiyo ni mkoa wa Arusha na Mara inabaki mtazamaji tu?
Huko sipendi kufika kwa sababu sina uhakika, labda kama yupo mwenye uelewa zaidi.
 
Mkoa wa Mara hauko Kaskazini Mashariki ya Tanzania bali uko Kaskazini Magharibi ya Tanzania, nadhani hapo mtoa post ulijichanganya
Watu wa Jiografia watakuja kuthibitisha
 
Sema 4,wakati mwingine inaweza kuwa ni tafsiri hafifu ya waliyonayo wasomi ambapo Sasahivi inaonekana ukiwa Prof au Masters holder gombea then shavu nje nje.

Au wakati mwingine labda tatizo la Ajira ni kubwa kiasi kwamba ma Prof kutoka Mara wamesanuka deal ni kuomba Ajira husika.
 
Kuna Kijiji kinaitwa Rung'abure daah nilikaa pale Kuna wababe serikali imeshindwa kujenga hata kituo Cha polisi pale.​
Huwa hawachelewi kukatana mapanga pale. maduka mengi yamejaa mapanga wanauza sana​
Napafahamu sana hapa,ukienda mosongo,nyamatoke,monuna,kemgesi huko kukuta mtu kakatwa kichwa ni jambo la kawaida
 
Mkoa wa Mara unapatikana Kaskazini mashariki mwa nchi ya Tanzania. Kwa mujibu wa tovuti ya mkoa, kiutawala Mkoa umegawanyika katika Wilaya 6 ambazo ni; Musoma, Butiama, Bunda, Serengeti, Tarime na Rorya zenye Halmashauri 9 ambazo ni; Manispaa ya Musoma, Butiama, Bunda, Bunda Mji, Serengeti, Tarime, Rorya na Tarime Mji. Makao makuu ya Mkoa wa Mara ni Musoma na jina "Mara" ni kwa sababu ya Mto Mara ulio mkubwa kuliko mito yote katika mkoa huo.

Katika Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012, Mkoa wa Mara ulikuwa na watu takribani 1,743,830. Kijiografia mkoa umepakana na mikoa jirani ya Simiyu upande wa kusini, Arusha upande wa kusini-mashariki, upande wa Magharibi mkoa umepakana na ziwa Viktoria na Kenya kwa upande wa Mashariki.

Nadhani hadi kufikia hapo huwezi kupotea endapo utahitaji kutembelea Mkoa wa Mara hasa kushuhudia maajabu nitakayoyaelezea hapa chini. Turudi sasa kwenye maajabu yanayopatikana mkoa wa Mara.

1. Muasisi wa Taifa la Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa ni mzaliwa wa mkoa wa Mara;
Nisingependa kumzungumzia sana mtu huyu ambaye kamwe habari zake haziwezi kusahaulika kwenye Historia ya Taifa la Tanzania vizazi na vizazi. Ninayo imani kuwa karibia asilimia 100 ya watu tulio humu Jamii forum, tutakuwa tunafahamu kuwa Mwalimu Nyerere alizaliwa wilaya ya Butiama mkoani Mara ambapo ndipo hata makumbusho yake yanapatikana.

2. Hifadhi ya wanyama ya Serengeti:
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti yenye ukubwa wa kilometa za mraba 14,763 ilianzishwa mwaka 1951, ni Hifadhi ya Taifa ya pili kwa ukubwa nchini ikitanguliwa na hifadhi ya Taifa ya Ruaha yenye ukubwa wa kilometa za mraba 20,226 (Rejea tovuti ya TANAPA).

Licha ya kwamba hifadhi hii inapatikana mikoa mingine ya Tanzania lakini sehemu kubwa ya hifadhi hii inapatikana katika mkoa wa Mara. Kama ulikuwa hujui basi jua kuwa hii ni mbuga inayoheshimika kama moja ya urithi wa dunia na Shirika la umoja wa Mataifa linajishughulisha na masuala ya elimu, utamaduni na Sayansi (UNESCO). Hii ndiyo hifadhi maarufu zaidi Afrika japo zipo hifadhi zingine tena kubwa kuliko Serengeti lakini bado zinasalimu hapa.

3. Kuwepo kwa kanda maalumu (Mkoa wa kipolisi):
Huwezi kuamini hapa nchini ukitoa mkoa wa Dar es Salaam peke yake ila kanda maalumu nyingine inapatikana mkoa wa Mara tu tena kwenye wilaya mbili (Kanda maalumu ya Tarime-Rorya). Hakika hili ni ajabu ambalo linafikirisha na sababu zake yawezekana zinajulikana wazi au hazijulikani sana kwa wengi wetu, wenye uelewa wanaweza kufafanua zaidi.

4. Kuwepo kwa idadi kubwa ya wasomi:
Wengi watabisha ila wachache watakubali. Kiuhalisia ukiutoa mkoa wa Kilimanjaro na Kagera basi mkoa wa Mara ni mkoa wenye idadi kubwa sana ya wasomi tena wa kiwango cha juu. Hivi juzi katika jimbo la Musoma vijijini peke yake, walijitokeza Maprofesa 7 kutia nia ya kuomba ubunge. Kumbuka hapo bado majimbo mengine, achana na wale ambao hawakutia nia, bado kuna majimbo mengine, jumlisha na wale wenye elimu chini ya profesa mfano, wenye Shahada za Uzamivu, Shahada za uzamili, Shahada ya kwanza, Astashahada, Shahada n.k.

Kuna mtu aliwahi kuandika uzi fulani humu Jf unaowahusu wasomi wa mkoa wa Mara nadhani ukiupata pia unaweza kukupa mwanga fulani kuthibitisha dai hili.

5. Idadi ya makabila mengi:
Sikia hii, mkoa wa Mara unayo makabila zaidi ya 25 ya Kibantu na Kiniloti. Tofauti na watu wengi wajuavyo kwamba Wakuria (Wakurya) ndiyo kabila pekee lakini hii siyo kweli na sababu ya kuendana kwa matamshi ni kwa sababu ya kuingiliana tu, wataalamu wa Kiswahili wanaelewa kuhusu "lahaja". Kwa msaada wa wengine, lahaja ni tofauti ndogondogo zinazojitokeza kwenye lugha yenye asili moja. Kwa maana hiyo makabila mengi ya mkoa wa Mara yanaingiliana ila yapo tofauti sio kwenye salamu tu bali hata matamshi mengine.

Mara nyingi huwa mtu akisema anatokea Mara basi watu hurahisisha kwa kusema kuwa mtu huyo atakuwa Mkuria kitu ambacho sio ukweli kwa sababu mkoa unayo makabila mengine mengi tu. Tazama baadhi ya makabila yaliyopo mkoa wa Mara;
Waluo

Wajita

Waruri

Wazanaki

Wakurya

Wakabwa

Wakiroba

Wasimbiti

Wakwaya

Wanata

Waikoma

Waisenye

Waikizu

Sizaki

Wadatooga

Wakine

6. Tohara bila ganzi;
Wamasai kutoka Arusha na maeneo ya Kenya nao wana utamaduni wa namna hii, ni yawezekana yakawa maajabu yao ila kwa mkoa wa Mara nao ni mkoa ambao sio wanaume wala wanawake hufanyiwa tohara. Mwaka huu 2020 utakuwa ni mwaka wa tohara kwa makabila mengi ya mkoa wa Mara. Waluo pekee ndiyo kabila kutoka Mara ambalo kwao kufanya tohara sio jambo la muhimu kukamilisha kama mila na desturi japo huwa wanafanya tohara hospitalini tu kama yalivyo makabila mengine.

KITU CHA AJABU KWENYE TOHARA;
-Hutakiwi kutikisika wala kuonesha dalili yoyote ya kuogopa au kulia na ukifanya hivyo utadharaulika hadi kwa watoto wadogo.

-Baadhi ya maeneo mengi ni ruksa mtu yeyote kuhudhuria tohara isipokuwa shangazi, yaani chukulia mfano mwanaume unafanyiwa tohara basi jiandae kupata mashuhuda hadi wanawake eneo la tukio.

-Eneo la kufanyia tohara huitwa "Kibaga" japo maeneo mengine hutamkwa vingine.

-Kirombe ni sherehe kabla ya tohara na ngoma yake ya jadi ni, rirandi, rithungu n.k.

-Mwanaume ukitahiriwa hospitalini unahesabika kama mwanamke na utapata tabu sana kwa vijana wenzio.

7. Panga ni kifaa muhimu kuliko jembe:
Japo kwa siku za hivi karibuni hali imekuwa tofauti kidogo lakini bado utamaduni huu upo. Maeneo mengi ya mkoa wa Mara usiogope kila kona hasa vijijini kukutana na mtu akiwa amebeba panga. Haijalishi mtu anakwenda shambani, disko, mpirani wengine hata kwenye mkutano wa kijiji akiwa na panga.

Kuna rafiki yangu mmoja daktari miaka 6 iliyopita alisema "akiwa Tarime, wagonjwa wengi walikuwa ni wale waliojeruhiwa na mapanga kuliko wagonjwa wengine". Hii sio sifa bali ni miongoni mwa maajabu ya mkoa wa Mara. Kwa wale wageni msiogope maana kwa sasa vyombo vya ulinzi na usalama vipo imara sana kudhibiti hali kama hii na amani imetawala.

8. Kilimo cha bangi:
Hii nayo sio sifa wala kashfa bali ni maajabu, mkoa wa Mara ni miongoni mwa mikoa ambayo inajihusisha sana na ulimaji na hata wakati mwingine utumiaji wa mmea huu haramu hapa nchini. Mara nyingi, vyombo vya habari nchini vimekuwa vikiripoti sana kuendeshwa kwa kilimo hiki na hata uteketezwaji wake katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Mara. Soma hapa kwa uthibitisho zaidi. Mikoa 8 inayoongoza kwa kulima bangi Tanzania | East Africa Television

HITIMISHO
Mambo yote niliyoyaelezea hapo juu, nimeyafanyia utafiti na hata kupitia vyanzo vya uhakika vya habari na kutembelea maeneo husika. Siku zote kuna mtu anaweza kuwa anajua zaidi yangu, hivyo ni ruksa kuongeza, kurekebisha na hata kukosea ili uzi uwe bora zaidi ya hapa. Kitu cha msingi ni kuja na facts zako na kutumia lugha faafu bila kuvunja sheria za Jamii forums.

Naomba kuwasilisha.
View attachment 1524759
Hili LA tohara hata Pemba ila siku hizi imebadilika, linafanywa hospitali
 
Back
Top Bottom