Maajabu: Aliyetakiwa kumdhamini kada wa Chadema azuiwa kuingia mahakamani kwa kuambiwa kuwa ana Corona baada ya joto lake kusoma nyuzi 37.1

Maajabu: Aliyetakiwa kumdhamini kada wa Chadema azuiwa kuingia mahakamani kwa kuambiwa kuwa ana Corona baada ya joto lake kusoma nyuzi 37.1

Sasa usanii uko wapi kama amepimwa joto na likaonekana kuwa juu huku indicator ya kupima corona ya kwanza ni joto?
Ninaamini angekuwa wa chama kingine ungeleta habari za furaha hapa kuwa kada akutwa na corona na ukafanya sherehe
Aliewaroga kafa eeehh?
Lini mtakuwa huru?
Tushaambiwa magonjwa mengine kama malaria yapo
Sasa ukimpima mtu ukamkuta koto limepanda je hiyo sio dalili ya malaria au mnatetea hoja hamkumbuki viongozi tena wakuu Wanavyo tuambia.
Leo kenya wanawapima wa kwenu mnasema ni vita za kiuchumi
Huyu mtu joto kupanda ndo mseme Corona duuuuh
 
Haya nayo ni maajabu mengine yametokea huko Tarime hapo jana baada ya ndugu Chacha Heche aliyetakiwa kumdhamini kada wa Chadema mahakamani kupimwa joto la mwili likasoma nyuzi joto 37.1 kisha akaambiwa kuwa ana Corona na kuzuiwa kuingia ndani ya viunga vya mahakama.

Kada huyo alilazimika kurudishwa mahabusu kutokana na hali hiyo.

Wao kwao ukisema unaonekana wakali wa beberu ila kwa wengine ni sawa. Serikali ya CCM isipoacha usanii huu acha tuendelee tu kuungana na wanaoichapa nchi huko kwa wenzetu. Hakuna haja kuungana na serikali ya aina hii.
Si mgelileta mdhamini mwingine?
 
Bora kuungana na shetani kuliko hawa watu!

Namshukuru Kigogo anavyowaanika kwa kuendelea kuanikia nyaraka zao zinazowavua nguo na kuwaacha uchi

Endelea kukaa na shetani ili uendelee kuungua moto
 
Naona Corona imegeuka kuwa ngao nyingine ya maccm. Mkuu kwani polisi na mahakama haviwatoshi?

Nani alimtuma aende na hilo joto? Au kwa vile ni chadema basi aruhusiwe tu?
Chadema si.mpo wengi sasa mnakosaje mdhamini?

Ilitakiwa kama mnakubalika wadhamini wa ngekuwa wengi mmoja akishindwa mwingine anadhamini,

Na hapo utakuta ni mzazi au ndugu ndie anahangaika ila washabiki wa chama mmemtelekeza mtu wenu
 
Unategemea nini nchi inapoongozwa na mtu mmojaa aliyesema anapenda maamuzi ya "ukichaa kichaa"? Ni wazi kila mteule atakuwa na maamuzi ya kichaa .
 
Ni naona mmetoka kwenye mjadala wa nyuzijoto 37.1 kuwa si joto la mtu asiyeugua, ndiyo sababu huwa hamfikii muafaka zaidi ya porojo tu.
 
Usiwe mpuuzi joto wee!!! centigrade 37.1 ni joto la korona?!! Msitetee upumbavu unaopelekea kuonekana mazuzu nchi nzima.
Ukipinga tu, tayari unarudi Kwa Magu kukubaliana naye kuwa vifaa vya kupima Corona vinatia Shaka

Sasa hapo ni kuamua, ukubali ili vifaa viwe havina tabu, ukatae uungane na mkulu kuwa vifaa hivi ni feki
 
Kuwa na joto haimanishi una corona
Unaweza kupima mashine ikasoma 39
Ukapumzika kidogo na ukapima tena mashine ikasoma 35

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Nani alimtuma aende na hilo joto? Au kwa vile ni chadema basi aruhusiwe tu?
Chadema si.mpo wengi sasa mnakosaje mdhamini?

Ilitakiwa kama mnakubalika wadhamini wa ngekuwa wengi mmoja akishindwa mwingine anadhamini,

Na hapo utakuta ni mzazi au ndugu ndie anahangaika ila washabiki wa chama mmemtelekeza mtu wenu
Majibu ya Lumumba
 
Back
Top Bottom