Uchaguzi 2020 Maajabu: Fomu ya kuomba Wadhamini ya Mgombea wa CCM inatembezwa na Viongozi wa CCM Makao Makuu...

Uchaguzi 2020 Maajabu: Fomu ya kuomba Wadhamini ya Mgombea wa CCM inatembezwa na Viongozi wa CCM Makao Makuu...

Japo hujaweka ushahidi maana kwa uzushi hamjambo lakini kwani huyo mpogolo yeye sio mwanachama? kujazisha fomu kuna uhusiano gani na maamuzi?.Mimi fomu yangu ya kugombea ubunge nitampa mwanachama mwenzangu wa CCM JOHN Magufuli anizungushie kusaininisha fomu yangu sababu naye ni mwanachama. sioni shida
Hiyo akili matope?
 
Wewe ni mfuasi, kama siyo mwanachama, wa CHADEMA, wajibika kwa taratibu za chama chako. Hata vile, kama una nia ya kutia nia ya kugombea Urais CCM, fanya hivyo na bila shaka utapewa fomu na baada ya hapo fuata masharti yaliyomo.

Moja ya sharti la msingi ni kupata wadhamini kwenye mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar kwa idadi ya wadhamini na mikoa kama ilivyoainishwa. Njia gani utatumia kupata hao wafuasi ni juu yako mradi wawe ni wadhamini halisi siyo wa kugushi...
Sasa kama yupo mwenyewe wadhamini wa kazi gani? Maana hata wawepo au wasiwepo hamna impact yoyote.
Hayo mafuta na posho atakayozungukia huyo mpogoro Tanzania yangefanya mambo mengine ya msingi.
 
Sasa kama yupo mwenyewe wadhamini wa kazi gani?? Maana hata wawepo au wasiwepo hamna impact yoyote.
Hayo mafuta na posho atakayozungukia huyo mpogoro Tanzania yangefanya mambo mengine ya msingi.
Unauliza, kushangaa na kujijibu.
 
Jakaya alipochukua fomu ya kuwania Urais 2010 na kumpa Mwanachama mwenzake Ridhwan Kikwete amtaftie wadhamini basi kina Saeed kubenea na wana Chadema wenzie walimtukana sana Jk kwa madai eti kadharau Viongozi wenzake ambao wangeweza kumsaidia kupata wadhamin, leo hao hao wanapinga ushauri wao

Viva Ngosha
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Utaratibu wa miaka yote mgombea mwenyewe au wapambe wake ndio wenye jukumu la kutafuta wadhamini wa Mgombea wao , si viongozi wa Makao Makuu, hii ni kwa sababu viongozi hao hawatakiwi kubagua wanachama , maana wagombea wanaweza kuwa zaidi ya mmoja , ndio maana wagombea wote wa urais wa CCM 2015 akiwemo mkulima kapuku wa Kigoma waliwajibika wenyewe kutafuta wadhamini , lakini Rodrick Mpogolo ambaye ni kiongozi wa Makao Makuu anahangaika kumtafutia wadhamini Mgombea aliyeomba mwenyewe kugombea urais .

Sasa swali ni iwapo kutakuwa na wagombea wengine kama inavyotarajiwa na wanaccm , viongozi wa Makao Makuu watajigawa namna gani , kwanini wasiache wagombea wajitafutie wenyewe wadhamini ?

Kwani kuna nani anataka kuchukua fomu mwingine?
 
Vitu vingine hata msitokwe povu unnecessarily. Hivi unategemea kabisa CCM imtupe Magufuli na kuteua mtu mwingine? Nani kwanza atajitokeza zaidi ya wakulima hohehahe!?
 
Kwa saivi wadhamini ndo wanaitafuta form yake kuidhamini, wataifata popote ilipo na kusaini chap
 
Hilo halina mjadala, na ni muongo wa kutupa, achia mbali kwamba hana hoja za ushawishi zaidi ya shuruti. Hili taka usitake.
Wivu tu. Dkt Magufuli ni jembe letu! Mungu ambariki sana.
 
Back
Top Bottom