Watoto wa viongozi wa umma wenye mitaji mikubwa watoto wao wanaajiriwa katika nafasi za kiuongozi . Ila wewe unawaambia watoto wa maskini wakajiajiri kuuza viatu chini Kariakoo.
Wewe nawe ni maajabu pia .
Haya niambie juhudi walizoziweka CCM za kumfanya kijana ajiajiri na afurahie kazi yake?
Mimi ninaona hizo ni chuki za kimasikini ambazo ni donda ndugu kwa vijana.
Hapa sizungumzii CCM wala Chama chochote cha siasa na kama kuna chama cha siasa kinaahidi ajira kwa wasomi wote, basi chama hicho ni feki.
Ajira ninavyofahamu inaenda na mahitaji (ikama) Kuna kipindi nchi yetu ilikuwa inaajiri vijana bila ya kufuata mahitaji ikajikuta ina wafanyakazi wengi na ufanisi ulishuka kiasa ilibidi baadhi ya wafanyakazi wapungunzwe.
Kurudi kwenye mada Ajira maana yake ni shughuli yoyote ile (halali)ambayo inaweza kukuletea kipato. Kuwa Tajiri siyo lazima uanze na mtaji mkubwa. Nitakupa mifano miwili tofauti
1. Marehemu Mzee Mengi. Mzee huyu alizaliwa kwenye familia masikini sana ila alifanya vizuri sana masomoni na akawa moja ya vijana wa
mwanzo kupata hati ya ACCA. Alipata kazi nzuri tu kwa wakati ule, lakini hakuridhika na kuajiriwa aliacha kazi. Aliangalia fursa zilizopo na moja
wapo ni kalamu za kuandikia. Alianza mradi huo akishirikiana na mkewe na huo ndiyo ukawa mwanzo wa mafanikio yake kwani kiu ya
maendeleo iliwaendesha kiasi cha kuwa mwanzo wa uwekezaji ambao hadi leo unaendelea ingawa wenye wametangulia mbele ya haki.
2. Mzee Bakhressa. Huyu kwao unguja kazi kubwa familia yake ilikuwa inafanya ni kutengeneza viatu makubadhi pamoja na viatu vya sandal za
ngozi. Alihamia Dar na kuanza shughuli hizo hapa kwa kuwa aliamini kuna soko kubwa la bidhaa hizo. pole pole akajiingiza kwenye
mgahawa. Kutoka hapo alianza kutengeneza mikate kwa watu wa kariako. Amekuwa akipanua biashara na kuwekeza kiasi cha hivi leo, ni
mmoja ya watu matajiri sana.
Nitakupa mfano hai ambao miimi nimeshuhudia. Nilikuwa na shughuli maeneo ya gerezani. Kulikuwa na kijana mmoja mwenye umri wa miaka 14. Huyu asubuhi alikuwa anauza tangawizi na maandazi , mchana anauza karanga na sigara na jioni alikuwa ana uza kahawa.
Nilizoweana naye sana kiasi cha yeye kunihadithia kuwa alikimbia nyumbani kwao usambaani kutokana na umaskini wa wazazi wake na alitoroka kuja Dar na mwenzake ambaye alikuwa anafanya shughuli kama hiyo .
Miaka mingi ilipita bila kuonana naye. Miaka ya karibuni nilibahatika kuonanan naye alikuwa amebadilika sana. Katika maongezi aliniambia kuwa kipindi kile alikuwa anahangaika karibu masaa 15 na alikuwa hana mapumziko kabisa ukiondoa wakati akiumwa.
Kutokana na kuchukia umaskini uliozonga familia yake na jitihada alizochukua kufukuza umasikini. Leo hii yule kijana amekuwa mtu mzima na amefanikiwa sana kimaisha kwani ana biashara ambazo zimezagaa kariako, naye sasa ameajiri vijana na pia akiwa na mjengo wa ghorofa ia biashara eneo hilo hilo la gerezani . Watoto wake wanapata elimu bora kabisa.Watoto wake kwenye shule nzuri sana.hizo ndizo kiu za maendeleo.
Aina ya watu kama nyinyi ambao mnapenda kulalamika tuu mtaishia hivyo hivyo hata serikali ikichukuliwa na vyama vingine mtabaki hivyo kutokana na 'attitude yenu'
Miaka ya mwanzoni tuliambiwa kuwa na adui 3 yaani ujinga, umasikini na maradhi. Mimi ni ninaamini ujinga ukiondoka baada ya kupata elimu, maradhi na umaskini ni lazima uondoke .