Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Habari wakuu!
Kwa umri wangu mdogo wa miaka takribani 30 nimejifunza mengi, sijabahatika kuvuka mipaka ya Tanzania lakini nimefika karibu mikoa 20 ya Tanzania bara.
Hulka na silka za Watanzania zinafanana.
Kwa uelewa wangu wa mambo ya kisiasa niliojifunza mitaani na mitandaoni nimehitimisha kuwa CCM inauwezo wa kushinda kwenye sanduku la kupigia kura kwa miaka 15 mbele. Yaani 2020, 2025 na 2030 watashinda kwa damu baada ya mtifuano utakaopelekea ccm kushinda kwa asilimia za single digit na hapo ndio utakuwa mwisho wa CCM kupata ushindi kwa miaka ya hivi karibuni. Kwa nini ninasema CCM watashinda ndani ya miaka 15 ijayo?
Wananchi wa Tanzania ndani ya hii miaka 15 bado wengi watakuwa hawajapata elimu ya msingi( namaanisha form 4), pili kizazi cha Nyerere (watu watii na wavumilivu) kitaendelea kuwepo kwa idadi kubwa ndani ya hii miaka 15.
Naamini ujinga na upumbavu unaowapelekea watanzania kusahau mambo haraka bado vinahitaji miaka si chini ya 15 kufutika.
Rushwa na takrima Tanzania bado changamoto, mtu anaweza kuuza kura yake kwa elfu 20 tu na kubadili uamuzi. Chama tawala ndicho chenye nguvu ya kifedha.
Ninaamini CCM October 2020 watapata kura nyingi za halali licha ya ;
- Watumishi wa umma kutopanda mshahara tangu 2015.
- Sarafu ya Tanzania kushuka kwa miaka hii 5.
-Bei za bidhaa mbalimbali kupanda.
-Uvunjaji holela wa katiba
-Ukosefu wa ajira kwa vijana, ikumbukwe ajira ni haki ya kijana pamoja na kwamba haijaandikwa kwenye katiba.
-Kupanda kwa gharama za matibabu(huduma za afya).
Asanteni.