Maajabu: HESLB wamenifutia deni lote lililokuwa limesalia mwezi huu Januari

The unpaid Seller

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2019
Posts
2,113
Reaction score
6,251
Hallo hata sijui wamekosea au vipi. Nimecheck salary slip ya January nimekuta loan board hawajanikata na hawapo kabisa kwenye salary slip yangu.

Nikapagawa kwa muda ikabidi nicheck status ya loan yangu kwenye website yao, nikakuta napongezwa kwa kumaliza kulipa deni.

Awali mwezi uliopita deni lililobakia lilikua linasoma milioni mbili kasoro ila ghafla nimekuta limefutwa. Wakuu kuna nini kinaendelea loan board. Je kuna wengine wamepata mabadiliko na kufutiwa deni lililobaki kama mimi?
 
Nchi hii ina unyonyaji sana. Yaani mtu analipwa gross ya 1.2 M halafu wanakata mpaka anabaki na laki 5!! Laki 5 hapo sasa ule, watoto waende shule, upate nauli, ulipe kodi ya nyumba huku ukinunua mifuko ya sementi ili uanze kujenga yako, ulipe michango ya harusi na vifo halafu hautakiwi kula rushwa.

Hii mishahara inatakiwa kurekebishwa haraka sana.
 
Tena huyu ana mshahara mkubwa sana
 
Kumbe unakula 1.2M unapata wapi ujasiri wa kukopa NMB
 
We ni mwalimu mkuu kwani na hyo mil 9 ushamaliza wewe kwa kozi ya walimu ada ni ndogo huna deni wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…