Maajabu: Magufuli anataka tuwe na Club ya Taifa

Maajabu: Magufuli anataka tuwe na Club ya Taifa

Mkuu usisahau huyu aliwahi kujiita Mwendawazimu pia JIWE. Akikwambia 10 usishike hata moja.
"Bashungwa tumekupeleka kwenye michezo tunataka tushinde, sio tukilala tukiamka mabao 10, wote mtaondoka hata wewe Naibu Waziri Ulega, tukashinde, na Simba na Yanga zimetuchelewesha ikiwezekezana tuwe na Club ya Taifa kabisa isiyokuwa na Usimba na Yanga” asema Rais Magufuli akiwaapisha Mawaziri wapya leo IKULU Dodoma.
 
"Bashungwa tumekupeleka kwenye michezo tunataka tushinde, sio tukilala tukiamka mabao 10, wote mtaondoka hata wewe Naibu Waziri Ulega, tukashinde, na Simba na Yanga zimetuchelewesha ikiwezekezana tuwe na Club ya Taifa kabisa isiyokuwa na Usimba na Yanga” asema Rais Magufuli akiwaapisha Mawaziri wapya lelo IKULU Dodoma.
Alisema timu ya taifa siyo club ya taifa.
Acha upotoshaji.
 
Naomba kutoa maoni yangu.

Kama katika maisha yako huna mipango ya maendeleo ya muda mfupi na muda mrefu, hutaweza kufanikiwa. Upeo wa kuona zaidi ya leo na kesho ni tatizo kubwa sana kwa maendeleo ya nchi zetu za Afrika.

Naomba kutoa mfano hai. Ninaishi Marekani (miaka 25 sasa). Nimeona jinsi wanavyopanga mipango ya muda mfupi na muda mrefu. Nitoe mfano wa mchezo wa mpira wa kikapu (Basketball), ambao Marekani ameutawala kwa muda mrefu. Kuna viwanja vya kikapu (Basketball playgrounds) kila sehemu. Kila shule za awali (pre-school), shule za msingi na sekondari (grade and high schools), na vyuoni, pamoja na sehemu zilizotengewa kama za wazi zimesheheni viwanja vya nje na ndani. Kwahio watoto kuanzia umri mdogo wanacheza na kufundishwa kuucheza mchezo huo. Kuanzia shule za msingi na sekondari mpaka vyuoni, kila shule ina makocha wa karibu kila mchezo aliyeajiriwa na shule. Sehemu ya kodi unayolipia sehemu unayoishi (kitongoji, mji, nk.) inalipia mishahara ya makocha na gharama nyingi za shule ikiwemo viwanja vya michezo. Kuanzia shule za msingi, kuna mashindano ya kitongoji (wilaya) mpaka jimbo zima. Kwahio, toka udogoni, unapata vikundi vya vijana ambao wanafundishwa jinsi ya kucheza pamoja na kuwa mwanamichezo (namna ya kufanya mazoezi, kula, kuongea na waandishi wa habari, nk).
Ukienda vyuoni, kuna chama kinachoongoza michezo (NCAA). Kinashirikisha vyuo vyote kulingana na madaraja (division 1, 2, etc). Wachezaji karibu wote mashuhuri wa kikapu waliopata na wanaocheza sasa katika ligi kubwa na maarufu ya kikapu duniani (NBA) kama Michael Jordan, Magic Johnson, Shaquille O'Neal, Hakeem Olajuwon, Tim Duncan, etc. wametokea katika mfumo huo. Mpaka wamefika kucheza vyuoni (NCAA), wameshapikwa kutoka mfumo wa chini (msingi na sekondari). Haya mashindano yanadhaminiwa na makampuni yote makubwa duniani kama Nike, Adidas, Coca Cola, nk. Hii ndio sababu Marekani wanatamba zaidi katika mchezo waliowekeza zaidi.

Kutokana na uwekezaji mkubwa na faida kubwa makampuni yaliyowekeza wanayopata, sekta ya michezo imefungua na kukuza sana michezo. Zaidi ya kuwafanya wachezaji wa kikapu kuwa matajiri sana, imefungua uchumi wa nchi na kuwajumuisha madaktari wa michezo, hospitali zenye vitengo vya kutibu wana michezo, wahasibu wa wachezaji, mawakala wa wachezaji, sports trainers, wasemaji wa wana michezo, etc. Imefanikisha kufanya vyuo kuanzisha degrees za michezo. Kwahio sekta ya michezo imekuwa muhimu sana katika kukuza uchumi wa Marekani.

Hata tulipowekeza kwa kiasi kidogo, mafanikio na maendeleo yaliwahi kuonekana. Mimi nilisoma shule ya msingi ya Upanga miaka ya themanini. Kulikuwa na mashindano ya mpira wa miguu kati yetu na Zanaki, Muhimbili, Olympio, nk. Wakati nasoma sekondari shule ya Azania (nikiwa nacheza kikapu), tulikuwa tunashiriki mashindano ya mkoa. Nimeshiriki Umisseta mara mbili (1990 na 1991). Timu yetu yote ya kanda ya Mashariki ndio iliyokuja kuunda vikosi vya kwanza vya Pazi na Vijana, ambazo ndio zilizokuwa zinatamba kwenye kikapu Tanzania. Nilienda Umisseta na wachezaji kadhaa ambao walikuwa kucheza Simba, Yanga, na timu zingine kwenye soka pia.

Ninachotaka kusema ni hichi. Katika orodha ya nchi zinazotamba katika michezo (kwa mfano mpira wa miguu), asilimia kubwa zaidi ni nchi zilizowekeza zaidi kuliko wengine. Zinakuwa zinashindana wenyewe kwa wenyewe. Hakuna suala la njia ya mkato au bahati. Ni mipango thabiti ya kuinua vipaji toka utotoni ndio njia pekee ya kupata vipaji na kuvikuza katika misingi mizuri. Kama unajua mwanao atakuwa anakwenda chuoni miaka mitatu ijayo na hujaanza kujipanga kupata fedha za ada na za kujikimu toka sasa, usilaumu mtu yoyote utakaposhindwa kumpeleka.

Michezo inahitaji uwekezaji kama vile tunavyowekeza kwenye sekta zingine. Lakini tukichukua michezo kama njia ya vijana kutoka jasho na kufanya mazoezi tu, hatutafika popote.

My 2 cents.
 
Madikteta wakiamka wanaamua watakavyo hatari sana.

Ndiyo maana karudisha enzi za chama kimoja.
 
Raisi Magufuli ni kama Watanzania wengi hawaelewi maana ya football club, ndo shida ya kuletewa kila kitu nafikiri Muzungu angetuelewesha kwanza haya mambo kabla ya kutukabidhi na kuondoka, I mean kama unashindwa kujenga football club unawezaje kujenga nation's club ? Kuna sababu kwa nini kuna ligi daraja la kwanza, pili, tatu mpaka la nne huko, kuna sababu kwa nini kila Mkoa (unapaswa) kuwa na Timu na kila timu iwe na football club, sasa huwezi tu wewe kutoka ulikotoka kutaka kubadilisha rules of game na ukafikiri utafanikiwa.

Nasema Watanzania wafundishwe kwanza maana ya football club kabla ya kujifanya mnajua sana kuhusu soka, ...
 
Tuanze na hizo timu za Halmashauri, Mbeya City, Dodoma Jiji na Namungo . Tukimaliza tusngalie hizo timu za Jeshi Polisi TZ, Ruvu Shooting na JKT T.. Wakijua makosa yaliyopo ndio tuende huko kwenye timu ya taifa.. Simba na Yanga zitaendelea kuwepo tu.
 
Hahahahahaha😂😂😂😂, tutaweka historia mpya.
 
Club ya Taifa lazima itachukiwa na wapinzani wote pamoja na wale waliotumbuliwa majipu.
Wizara ijikite na kuzisaidia timu za Taifa na kuhamashisha uzalendo wa kuzishabikia timu zote zinazowakilisha nchi

Pia kuwe na mpango mkakati wa muda mrefu. Mfano kuwatafutia timu ulaya wachezaji wote wa timu ya taifa ya vijana (serengeti boys) ili wakalelewe huko. Baada ya miaka mitano tutakuwa na timu ya taifa inayojimudu. (Tukajifunze walivyofanya Madagasca)
Ulaya sio ndio waliopo mabeberu huko?
Kwa hiyo Magufuli atawezaje kukubali vijana wa Kitanzania wapelekwe?
 
Raisi Magufuli ni kama Watanzania wengi hawaelewi maana ya football club, ndo shida ya kuletewa kila kitu nafikiri Muzungu angetuelewesha kwanza haya mambo kabla ya kutukabidhi na kuondoka, I mean kama unashindwa kujenga football club unawezaje kujenga nation's club ? Kuna sababu kwa nini kuna ligi daraja la kwanza, pili, tatu mpaka la nne huko, kuna sababu kwa nini kila Mkoa (unapaswa) kuwa na Timu na kila timu iwe na football club, sasa huwezi tu wewe kutoka ulikotoka kutaka kubadilisha rules of game na ukafikiri utafanikiwa.

Nasema Watanzania wafundishwe kwanza maana ya football club kabla ya kujifanya mnajua sana kuhusu soka, ...
Kuna siku alisema atawapeleka wanajeshi vipi alitoa boko au hamu zilikuwa karibu
 
labda amemaanisha serikali iwe na club yake ya mpira wa miguu...achana na hizi club za taasisi mbalimbali
 
Mpira kwasasa kuna vitu vingi ilikupelekea mafanikio labda ajiulize, kwanini timu za taifa nyingi maendeleo yao sio mazuri?

Jibu ni masilahi katika timu zao wanazolipwa hela vingi hivyo upelekea wachezaji kutokuwa na morali katika timu za Taifa. ( Kwasababu tu hakuna hela za kutosheleza)

Na hili tatizo hata wazungu wanalijua!! Jingine la mwisho kabisa kwa timu pale TFF lakini hakuna impact yoyote katika timu yetu ya Taifa, ni kwasababu watoto wa pale TFF wanacheza kwa kujuana na viongozi.

NB , Senegal mwaka 2002 walifanya maajabu katika Kombe la dunia sio kwa maajabu walijipaga , ndio maan waliwapeleka vijana nchini France wote kwa pamoja.

Mpira sio siasa , mpira sio nguvu mpira unahija akili.
Usilete frustrations zako za kisiasa kwenye jukwaa hili...endelea na masuala yako ya siasa kwenye jukwaa la siasa Kama ulivyofanya kipindi Cha kampeni
 
Usilete frustrations zako za kisiasa kwenye jukwaa hili...endelea na masuala yako ya siasa kwenye jukwaa la siasa Kama ulivyofanya kipindi Cha kampeni
Mpira ujacheza uwezi kuelewa kima wewe.
 
Hii club ya taifa inaweza kununua mchezaji kwa milioni 700 tena kutoka Zambia?
Club za majeshi tu zimeshindwa hiyo ya taifa itawezaje?
Timu ya taifa inashindwa kabisa,kuna vijana walifanya vema Serengeti boys lakini wengine sasa walishapotea.Itakuwa kazi ngumu sana ku manage hii club
 
Ana sifa za Mfalme JUHA,Andazi kuwa na bei ya juu kuliko dhahabu.
Magufuli anaamini anajua kila kitu,ndo maana nchi imemdodea amebaki kulaumu wateule wake.
 
anataka tujue historia ya tanzania tena anasema kuwe na somo kuhusu historia ta tz apo apo ni kama vile azitak simba na yanga wakat pia izo timu mi historia ya tz ,mimi nazan haupend mpra na ata kama anaufuatilia sio kiivyo
 
Back
Top Bottom