Maajabu: Magufuli anataka tuwe na Club ya Taifa

Maajabu: Magufuli anataka tuwe na Club ya Taifa

Naona yuko sasa. Kiongozi unatakiwa kuwa na maono na si kufanya mambo kwa mazoea. Tumekuwa tunachukua wachezaji simba na yanga. Tumefika wapi.
Tuwe na hiyo klabu ya taifa. Wakiamka mpira,wakilala mpira. Kazi yao iwe mpira. Ukiwadrill hawa kisawasawa unaweza kuta una bonge la timu. tunasema timu mbovu wachezaji hawana kemia, hawa watakuwa na kemia ya hali ya juu. Wamedrill pamoja muda wote. nchi nyingine zitaiga. Nampongeza kwa kukataa business as usual.
 
Hii club ya taifa inaweza kununua mchezaji kwa milioni 700 tena kutoka Zambia?
Club za majeshi tu zimeshindwa hiyo ya taifa itawezaje?
Timu ya taifa inashindwa kabisa,kuna vijana walifanya vema Serengeti boys lakini wengine sasa walishapotea.Itakuwa kazi ngumu sana ku manage hii club
Kuna mwaka waliandaa timu ya taifa walizunguka nchi nzima kusaka vipaj hawakuchukua mchezaj simba wala yanga ,wakaipa jina taifa maboresho mechi ya kwanza sikumbuk kat ya malawi au burundi ,tukala tatu kwa mkapa iyo timu mpaka leo sijui ilipo
 
mi ni mpinzani wa magufuri ,lakini kwa la simba na yanga kuua mpira wa tz yupo sahihi kabisa,,
ni kama ccm ndio kikwazo cha maendeleo hapa tz
Mkuu simba na yanga wanauwaje mpira wa Tanzania tusaidie kidogo hapo.
 
labda amemaanisha serikali iwe na club yake ya mpira wa miguu...achana na hizi club za taasisi mbalimbali
Mbona zipo Polisi Tanzania na JKT ambazo zinakula ela za taasisi za serekali na wala hazifurukuti?. Serekali iweke bajeti ya kutosha kwenye wizara ya michezo na kujikita zaidi kuinua michezo kwa vijana mashuleni
 
Kama mtu hujui kitu bora ukae kimya. Atupe mfano ambako kuna Taifa football Club.
 
Ana maana team zimilikiwe na liserikali lake au huyu bwana sijui aliwezaje kuapa bila kutetemeka
 
"Bashungwa tumekupeleka kwenye michezo tunataka tushinde, sio tukilala tukiamka mabao 10, wote mtaondoka hata wewe Naibu Waziri Ulega, tukashinde, na Simba na Yanga zimetuchelewesha ikiwezekezana tuwe na Club ya Taifa kabisa isiyokuwa na Usimba na Yanga” asema Rais Magufuli akiwaapisha Mawaziri wapya leo IKULU Dodoma.
Azijenge timu za jeshi zichukuw ubingqa africa
 
Chama cha mapinduzi football club (club ya Taifa)
 
Simba na Yanga ni vilabu binafsi vinawezaje kutuchelewesha kama nchi?

Atleast tungeongelea Tanzania Prisons...Ruvu shooting...Jkt Tanzania...Polisi Tanzania...Jkt Mlale..Mashujaa...KMC etc. hizo ndo timu za kujadiliwa maana ni za taasisi za Serikali siyo Simba na Yanga
 
mi ni mpinzani wa magufuri ,lakini kwa la simba na yanga kuua mpira wa tz yupo sahihi kabisa,,
Ni sawa na kusema kuwa vyama vya siasa vya upinzini ndo kikwazo cha maendeleo hivyo anachotaka Mr. Pombe ni kuwa na club moja tu ya CCM ili kusiwe na furukuta nyingine.
Mimi ndo nilivyouelewa kwa akili zangu finyu.
 
Anadandia vitu asivyovijua taahira huyu! Klabu ya Taifa, itashindana mashindano gani?
 
Back
Top Bottom