Mabibi na mabwana pongezi nyingi zimfikie mama Samia rais wetu.
Ama kwa hakika kajua namna za kukonga nyoyo za watu wake. Mama amekuwa muwazi. Sote sasa tunajua angalau tulipo na tunakoelekea.
Mama anaeleweka na mama anasomeka.
Mama hana makeke, mama hana kuomba omba kuombewa. Mama anajua anaongoza watu wenye akili zao si kundi la ng'ombe. Mama anachapa kazi.
Heka heka za kutafutana mitandaoni na ma bounty mazito mazito vichwani mwa watu yamekoma.
Pole pole tunaamini tutafika tu kunako mzizi wa yote kutakako tufanya tuwe watu wa furaha bila kujali nani yupo ikulu tena. Huko ni kunako katiba muafaka. Itakayotufanya tusijerejea tena kubaya kokote tulikotoka.
Kwa maneno yake mama mwenyewe, hii nchi ni yetu sote - na huu ndiyo ulio ukweli!
Ikumbukwe kuwa hotuba za mama zimeleta faraja si hapa nchini tu, bali hata katika mataifa alikokwisha kuzuru. Kwa hakika mama katutoa kimasomaso.
Hadhi yetu kama watanzania, inarudi.
Heko mama Samia Suluhu Hassan rais wetu.
Hadi hapa hakuzingui mtu.