Maajabu ya awamu ya Sita: Hotuba za mama zinapokonga nyoyo za watu

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mabibi na mabwana pongezi nyingi zimfikie mama Samia rais wetu.

Ama kwa hakika kajua namna za kukonga nyoyo za watu wake. Mama amekuwa muwazi. Sote sasa tunajua angalau tulipo na tunakoelekea.

Mama anaeleweka na mama anasomeka.

Mama hana makeke, mama hana kuomba omba kuombewa. Mama anajua anaongoza watu wenye akili zao si kundi la ng'ombe. Mama anachapa kazi.

Heka heka za kutafutana mitandaoni na ma bounty mazito mazito vichwani mwa watu yamekoma.

Pole pole tunaamini tutafika tu kunako mzizi wa yote kutakako tufanya tuwe watu wa furaha bila kujali nani yupo ikulu tena. Huko ni kunako katiba muafaka. Itakayotufanya tusijerejea tena kubaya kokote tulikotoka.

Kwa maneno yake mama mwenyewe, hii nchi ni yetu sote - na huu ndiyo ulio ukweli!

Ikumbukwe kuwa hotuba za mama zimeleta faraja si hapa nchini tu, bali hata katika mataifa alikokwisha kuzuru. Kwa hakika mama katutoa kimasomaso.

Hadhi yetu kama watanzania, inarudi.

Heko mama Samia Suluhu Hassan rais wetu.

Hadi hapa hakuzingui mtu.
 
Hata mimi nimeona. Hotuba yake iko vizuri. Imejaa busara na hekima sana...

Hata kama umeomba jambo lakini likawa haliwezekani kutekelezeka, anatoa maelezo ya wazi yenye sababu za kueleweka kirahisi kabisa...

Yaani hata kama mtu ulikuwa unadai deni, kwa maelezo haya tu, waweza kujikuta nguvu ya kudai inaisha hapohapo kwa kuwa unakuwa umeelewa maelezo na sababu za mdeni wako kushindwa kulipa deni...

Huu ndio uongozi sasa. Siyo kama Pombe Magufuli. Huyo mnyampara wala hakuwa kiongozi 100%...

Angalia tofauti yake. Wakati wa Jiwe, kwa kuwa wazee wameomba pensheni, nakuambia, mtu asingeshangaa wala kuona ajabu kusikia kauli kama hii kutoka kwake;

"....nawalipa wazee Wa CCM tu nyie wengine shauri yenu kwa sababu mko kwenye mavyama yasioeleweka labda mkiamua kujiunga na CCM nitawalipa. Serikali ya CCM ina hela nyingi. Tanzania ni dona cantri bwana. Hatuwezi kushindwa vipensheni tu kwa wazee wetu...!!!"

Lakini, aah huyu mama is very Inteligent, humble, humanly with full of wisdom....

Sijawahi kuipenda CCM wala viongozi wake. Ila huyu mama nadhani naweza kuanza kumuunga mkono kwa 100% sasa nje ya CCM...

Namwombea kwa Mungu Baba Yehova aendelee kumpa maarifa, busara na hekima ktk uongozi wake..AMINA..!!
 

Mama ana kipaji. Mama ni talented.

Ni kutokujitendea haki kutokuliona hilo.
 
Ajabu wanaomsifia humu JF ni sio wana CCM. Mama kama ana akili na ushauri mzuri itabidi ajitafakari!

Una uhakika gani kuwa wanaomsifia CCM hawamo?

Hujasikia bungeni wakiwamo Ndugai au hata leo Mlimani City.

Hujaona wote waliokuwa pale wakimsifia kwa bashasha wakiwamo Dr. Mpango, Majaliwa na kadamnasi yote ya waliokuwa pale? Hapo napo je CCM hawakuwamo?

Tofautisha wana CCM na magenge yenu ya yale makabila ambayo mama inabidi afanye hima kuyazingua mapema iwezekanavyo.
 
Nimesema JF dogo! Au hujasoma vizuri ukaelewa? Ndugai anaongeleaga JF? Pumbavu!!!
 
Kabisa mama anatupeleka kunako, hata wale wabelgiji wakae pembeni kwanza
 
Kwa hiyo wewe ulitegemea hao wasimsifu kwenye kikao hicho hata kama wasingekuwa wanakubaliana naye? Mpango, Waziri Mkuu asimsifu bosi wake?
Ndugai simhesabu kwenye kundi lolote ila la vilaza pekee.
 
Kwa hiyo wewe ulitegemea hao wasimsifu kwenye kikao hicho hata kama wasingekuwa wanakubaliana naye? Mpango, Waziri Mkuu asimsifu bosi wake?
Ndugai simhesabu kwenye kundi lolote ila la vilaza pekee.

Rejelea majibizano hayo yalikoyokea labda kama na wewe hoja yako ni kuwa mama anasifiwa na wasio wana CCM peke yao.
 
Nimesema JF dogo! Au hujasoma vizuri ukaelewa? Ndugai anaongeleaga JF? Pumbavu!!!

Nimekujibu na kulipa na majibu ya nyongeza. Ninakazia:

"Una uhakika gani kuwa wanaomsifia CCM hawamo?"

Povu lote hilo ni la Omo tu au cha Arusha kimo?

Mwaka huu mtaokota sana makopo hadi yaliyopo majalalani.

Nyambafu!!
 
Ngoja waamke wanakuja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…