Maajabu ya baadhi ya makanisa: Wapo radhi kumwabudu na kumheshimu Mwamposa lakini siyo Bikira Maria kama vile alifanya kosa kubwa sana kumzaa Yesu

Maajabu ya baadhi ya makanisa: Wapo radhi kumwabudu na kumheshimu Mwamposa lakini siyo Bikira Maria kama vile alifanya kosa kubwa sana kumzaa Yesu

deblabant

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2022
Posts
2,650
Reaction score
4,065
This is too contradictory.

Wanaojiita walikole wakiongozwa na KKKT wako radhi kumwabudu au kumheshimu mchungaji wao na kumuona Bikira Maria si chochote wala lolote. Naona hata yesu huwa anawashaa sana.

Bikira Maria kwao wanamuona kama bahasha iliyokuwa ndani ina barua. Baada ya kuitoa barua basi bahasha ile inatupw na kuonekana takataka. Hivi ndivyo wanavyomuona Bikira maria.

Huu ni upumbavu wa hali ya juu sana. Hata leo ikitokea Yesu akarudi duniani wako radhi kumkana na kusema mwamposa ndo yesu wao.

Hivi anachofanya Mwamposa kina tofauti gani ni mazingaombwe ya hapo awali yaliyokuwa yanafanywa mashuleni kama power mabula nk au utabili wa hali ya hewa.
 
Yaani unakuta mtu anamtukana mama yake Yesu alafu anaenda kumuomba Yesu amsaidie. Hivi kweli mtu anaweza akamtukana mama yako alafu ukamsaidia? WAJIRATIBU

USOME INJILI YA:

LUKA 1: 40-56

40 Baada ya siku chache, Mariamu aliharakisha kwenda mji mmoja katika milima ya Yudea. Akaingia nyumbani kwa Zakaria akamsalimu Elizabeti.

41 Naye aliposikia salaamu za Mariamu, mtoto aliyekuwa tumboni mwake aliruka. Elizabeti akajazwa na Roho Mtakatifu,

42 akasema kwa sauti kubwa: “Umebarikiwa wewe zaidi ya wanawake wengine wote, naye mtoto utakayemzaa amebari kiwa.

43 Sikustahili heshima hii ya kutembelewa na mama wa Bwana wangu!

44 Mara tu niliposikia salaamu zako, mtoto aliyeko tum boni mwangu aliruka kwa furaha.

45 Wewe umebarikiwa kwa kuwa uliamini kwamba Bwana atatimiza yale aliyokuambia.”

46 Mariamu akasema: “Namtukuza Bwana,

47 na roho yangu inamfurahia Mungu Mwokozi wangu.

48 Kwa kuwa ameutambua unyonge wa mtumishi wake. Tangu sasa vizazi vyote wataniita niliyebarikiwa.

49 Kwa maana, yeye Mwenye Uwezo, amenitendea mambo ya ajabu! Jina lake ni taka tifu.

50 Rehema zake hudumu vizazi hata vizazi kwao wamchao.

51 Kwa mkono wake ametenda mambo makuu. Wenye kiburi mioyoni mwao amewatawanya.

52 Amewaangusha wafalme kutoka katika viti vyao vya enzi na kuwainua wanyonge.

53 Amewashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri na matajiri amewafukuza mikono mitupu.

54 Amemsaidia mtumishi wake Israeli, akiikumbuka rehema yake,

55 kama alivyowaahidi baba zetu Ibrahimu na uzao wake daima.”

56 Mariamu akakaa na Elizabeti karibu miezi mitatu, kisha akarudi nyum bani kwake.
 
Una tatizo kubwa sana katika kufikiri.

Wa kupewa sifa na Heshima na utukufu ni Mungu pekee.

Mariam na Mwaposa ni viumbe tu.

Mungu ni MMOJA na YESU KRISTO/YESHUA HAMASHIACH ndilo JINA lake. Amen
Bikira Maria nafasi yale iko wapi sasa? Au alifanya kosa kumzaa huyo yesu
 
This is too contradictory.

Wanaojiita walikole wakiongozwa na KKKT wako radhi kumwabudu au kumheshimu mchungaji wao na kumuona Bikira Maria si chochote wala lolote. Naona hata yesu huwa anawashaa sana.

Bikira Maria kwao wanamuona kama bahasha iliyokuwa ndani ina barua. Baada ya kuitoa barua basi bahasha ile inatupw na kuonekana takataka. Hivi ndivyo wanavyomuona Bikira maria.

Huu ni upumbavu wa hali ya juu sana. Hata leo ikitokea Yesu akarudi duniani wako radhi kumkana na kusema mwamposa ndo yesu wao.

Hivi anachofanya Mwamposa kina tofauti gani ni mazingaombwe ya hapo awali yaliyokuwa yanafanywa mashuleni kama power mabula nk au utabili wa hali ya hewa.
Yaani wale wa Mwamposa na wewe wa Bikira Maria mpo fungu moja, wote mmepotea na njia yenu inaelekea moto wa jehanum.
 
This is too contradictory.

Wanaojiita walikole wakiongozwa na kkkt wako radhi kumwabudu au kumheshimu mchungaji wao na kumuona Bikira maria si chochote wala lolote. Naona hata yesu huwa anawashaa sana.

Bikira maria kwao wanamuona kama bahasha iliyokuwa ndani ina barua. Baada ya kuitoa barua basi bahasha ile inatupw na kuonekana takataka. Hivi ndivyo wanavyomuona Bikira maria.

Huu ni upumbavu wa hali ya juu sana. Hata leo ikitokea Yesu akarudi duniani wako radhi kumkana na kusema mwamposa ndo yesu wao.

Hivi anachofanya mwamposa kina tofauti gani ni mazingaombwe ya hapo awali yaliyokuwa yanafanywa mashuleni kama power mabula nk au utabili wa hali ya hewa.
Wewe ni mlevi wa Konyagi unayemcheka mlevi wa gongo. Kuna u-special gani kwa Maria kumzaa Yesu? Kanisa Katoliki ningewaona wajanja kama wangempa umuhimu Yosefu aliyekubali bila kusitasita kuwa ile mimba ilikuwa ya roho mtakatifu na sio mwanaume mwingine. Kijana gani wa sasa ambaye anasubiria kumuoa mchumba wake bikra halafu ghafla mchumba apate mimba na kudai ni kwa ya roho mtakatifu atakubali kuendelea kumuoa?
 
Bikira Maria nafasi yale iko wapi sasa? Au alifanya kosa kumzaa huyo yesu
Yesu ndiye alimuumba bikra Mariam,

Pia Yesu ndiye aliyejiumba ndani ya tumbo la Mariamu kupitia Roho wake mtakatifu.

Mariam pia alijua Hilo na alimwabudu Mungu.

Ninyi WANADAMU mnaomwabudu Mariam ni waabudu shetani.

Mungu ni MMOJA na YESU KRISTO/YESHUA HAMASHIACH ndilo JINA lake. Amen
 
yaani wale wa mwamposa na wewe wa bikira maria mpo fungu moja, wote mmepotea na njia yenu inaelekea moto wa jehanum.
Bikira maria alimzaa yesu na itabaki hivyo unless kuwe na mwanamke mwingine atakayemzaa yesu ili Bikra maria tumsahau. Anaheshimika kwa hilo kama aliyebatikiwa kuliko wanawake wote. Hivyo tuna acknowledge na kubappreciate sifa hizo
 
Yesu ndiye alimuumba bikra Mariam,

Pia Yesu ndiye aliyehiumba ndani ya tumbo la Mariamu.

Mariam pia alijua Hilo na alimwabudu Mungu.

Ninyi WANADAMU mnaomwabudu Mariam ni waabudu shetani.
Tumatambua Bikira maria kama ndiye aliyemzaa yesu na hivyo we pay respect for that
 
Wewe ni mlevi wa Konyagi unayemcheka mlevi wa gongo. Kuna u-special gani kwa Maria kumzaa Yesu? Kanisa Katoliki ningewaona wajanja kama wangempa umuhimu Yosefu aliyekubali bila kusitasita kuwa ile mimba ilikuwa ya roho mtakatifu na sio mwanaume mwingine. Kijana gani wa sasa ambaye anasubiria kumuoa mchumba wake bikra halafu ghafla mchumba apate mimba na kudai ni kwa ya roho mtakatifu atakubali kuendelea kumuoa?
Njia gani au ipi aliitumia Yesu kukufikia wewe kama siyo kwa njia ya Bikira maria. Hata hili hupay respect?
 
Una tatizo kubwa sana katika kufikiri.

Wa kupewa sifa na Heshima na utukufu ni Mungu pekee.

Mariam na Mwaposa ni viumbe tu.

Mungu ni MMOJA na YESU KRISTO/YESHUA HAMASHIACH ndilo JINA lake. Amen
Hata huyo Mungu mwenyewe huwezi kuthibitisha yupo.
 
Tumatambua Bikira maria kama ndiye aliyemzaa yesu na hivyo we pay respect for that
Sasa kwanini mnapiga magoti kumwabudu na mnazo Sala za kumwomba maria awasaidie!!

Hayo ni makufuru, JEHANUM inawahusu.

Hiyo ni dini ya shetani na pope ni agent wake mkuu.
 
Anayestahili kuabudiwa ni mmoja tuu naye ni Mungu mwenye Enzi

Hao wengine wote wanaweza kupewa sifa kwa vile Mungu anavyowatumia lakini utukufu ni kwa Mungu mkuu Yesu Kristo

Maria anaheshimiwa sana na wakristo na waislamu pia. Sio mchezo maana ilichukua miaka mingi haswa tangu unabii wa kuzaliwa kwa Kristo hadi kupatikana kwa tumbo lililoweza kumbeba... haikuwa rahisi
 
Unajua kabla walokole hawajakushangaa Yesu Kristo anakushangaa?
Soma alichowaambia watu wale waliotaka aache Kuhubiri Mkutano Neno la Mungu akamsikilize mama yake!🤔🤔
(Luka8:19-21)-Wakamwendea mama yake na ndugu zake, wasiweze kumkaribia kwa sababu ya MKUTANO.
20 Akaletewa habari akiambiwa, Mama yako na ndugu zako wamesimama nje wakitaka kuonana nawe.
21 Akawajibu akasema, Mama yangu na ndugu zangu ndio hao walisikiao neno la Mungu na kulifanya.
Sasa kati ya Mchungaji anayefanya kazi ya kuhubiri Neno la Mungu na Mama yake Yesu nani mkubwa?
Harafu fahamu Mariamu hakuwa bikra tena baada ya kumzaa Yesu,Mariam alizaa watoto wengine ndugu zake Yesu,(Mathayo13:53-55)
Mwisho Mariam alishakufa na yeye anangoja Ufufuo,na hakuna anayejua atafufuka ufufuo gani kama ni wa Uzima au wa Hukumu! Hilo anajua Yesu Kristo mwenyewe!
(Yohana5:28-29)
 
Back
Top Bottom