MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 14,311
- 36,056
Maria mtakatifu mama wa Yesu, utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu. AminaMleta mada tofauti mojawapo ya katoliki na madhehebu mengine ni kuwa wakatoliki huongea na maiti waliozikwa miaka awe Maria, Mitume nk kuwa wawaombee madhehebu mengine hayaombi maiti awaombee
Pili Mungu ni Roho tupu kamilifu kabisa kwa mujibu hata wa katekisimu ya kanisa Katoliki
Hakuna binadamu mwenye uwezo wa kubeba mimba ya roho na kuzaa roho
Maria alizaa Yesu mwili wa Yesu sio Roho
Kuita Maria ni Mama wa Mungu kama watu wanavyosali kwenye rozali sio sahihi ni kufuru.Binadamu hawezi kuzaa roho yaani Mungu ambaye ni Roho tupu isiyo na mwili
Mungu hana mama yake sababu Maria ni mwili mtupu wakati Mungu ni Roho tu
Kumwita Maria Mama wa Mungu ni kumfanya yeye mkuu kuliko Mungu mwenyewe.Lakini ukisema Maria mama yake Yesu haina shida mtoto kuwa mkuu kuliko wazazi kawaida tu
Mungu hana Mama yake na hatarajii kuwa na mama yake
wakatoliki kutwa kusali Maria mtakatifu mama wa Mungu utuombe ni kufuru
Lakini Yesu ni Mungu, Mungu mwana, katika lile fumbo la utatu mtakatifu ambalo ndiyo msingi wa imani yetu
Sasa ukilijua hilo, na kama wewe ni mkristu na ukiamini kwamba Yesu ni mwana wa Mungu na ni Mungu mwana katika utatu mtakatifu basi kuna ubaya gani tuki-address hivyo?
Yaani: MARIA MTAKATIFU MAMA WA MUNGU
Yeye Bikira Maria, siyo Mugu, ila Mungu mwana (YESU) alikaa ndani yake, tumboni mwakae miezi 9 na kunyonya maziwa yake miaka miwili, na kujifanya mtu ili aje kutukomboa