Ule wimbo wa kikatoliki umeandikwa hivi'sababu za kupewa sifa ziwe zipi?
''Msifuni Mama wa Yesu Kristu Mama wa Mungu wetu, Yeye ni Mama na Bikira''. Ndo maana namuuliza huyu ndugu mkatoliki kwa nini anapewa sifa wakati ni reserve ya Mungu na Kristu wake?. Mimi kwangu namheshimu kwa sababu Mungu alimchagua kuubeba wokovu wa dunia tumboni mwake. Baada ya kifo cha Yesu wote tunaokolewa kwa neema ya Msalaba. Nawaheshimu wakristo wote walio ndani ya Kristu maana hao ni kaka na dada zangu kwenye ufalme wa Mungu. Lakini siwezi kwa namna yeyote nikampa sifa za moyo wangu mtu yeyote maana na yeye ni chombo kama mimi. Labda amepewa utukufu uliozidi na Mungu nampongeza lakini sifa za moyo wangu ni za Bwana Mungu na Masiha wake yaani Kristu Yesu tu.