Maajabu ya dunia,mtu aliepata mtoto pasipo kuwahi kuishi kabisa

Maajabu ya dunia,mtu aliepata mtoto pasipo kuwahi kuishi kabisa

hypothalamus

Senior Member
Joined
Feb 19, 2018
Posts
126
Reaction score
153
Unaweza kufikiria ilikuwaje mtu ambae hajawahi kuishi kupata mtoto?

Familia moja huko marekani ilipata mtoto na baba alipoamua kufanya kipimo cha DNA majibu yalimshangaza
Hakuwa baba wa mtoto

Familia iliamua kufanya kipimo maalumu cha 23andMe na matokeo yaliwashangaza zaidi
Baba halali wa mtoto alikuwa ndugu wa kiume wa baba anaetambulika

Hii ilikuwa haileti sense yoyote kwa sababu mtoto alipatikana kwa njia ya Vitro Fertilization ambapo mtoto hutengenezwa kwa kurutubisha mayai ya mama na manii za baba nje ya mwili kwenye kifaa maalumu kinachoitwa Vitro

Baba anaetambulika alipojua hili mtazamo wake kuhusu yeye ni nani kama mtu ulibadiliki, na alipofanya uchunguzi zaidi.....

Aligundua yeye ni Chimera Human, Chimera human ni binadamu anaebeba pair mbili za DNA, ni sawa na kusema wanakuw watu wawili ndani ya mtu mmoja

Baba anaetambulika alipokuwa tumboni wakati wa hatua za mwanzo kabisa za utungaji wa ujauzito alikuwa na pacha wasio fanana, pacha wake ambae pia alikuwa wa kiume alifariki na yeye alinyonya asilimia 10 ya DNA cell za pacha wake huyo,kwa hiyo ndani ya mwili wake alibeba asilimia 10 ya DNA ambazo si za kwake

Cha kushangaza mtoto alirithi asilimia 10 tu za DNA za pacha wa baba yake na hakurithi ata asilimia 1 ya DNA za baba anaetambulika

Kibaiolojia mtu ambae hajawahi hata kuishi aliweza kupata mtoto
 
Hizi mambo acha zifanyike huko huko tu, huku afrika daaa!.
 
Sasa si ndio hadi uwe na pacha na hiyo DNA ya pacha ambae hakuishi waliitoa wapi kuifananaisha na mtt ?
Kufananisha wanafananisha kwa hicho kipimo cha 23andMe ambacho chenyew kinaweza kudetect patterns za urithi za DNA,mfano kwa taifa lenye mixture ya origin kama marekani mtu anaweza kufanya hicho kipimo akagundua lets say 70% ya herditary patterns zake ni muAfrica,30% ni muAsia

sio lazima kwa pacha tu,inaweza ikatokea mtoto akabeba cell za mama yake akiwa tumboni inaweza pia kutokea kwenye transplant ya viungo vya mwili kutoka kwa mtu mmoja kwenda mwengine
 
Mtoa post hapa napata shida kidogo. Hiyo fusion ya pacha mojawapo kuwa mwenzake ndiyo iliyopelekea awe na DNA mbili tofauti.? Na DNA zinaweza kuwa tofauti kwa mapacha wa kufanana? Maana wanatokana na the same sperm, na the same overy.?
 
Back
Top Bottom