Maajabu ya fundi wa mpira, Said Mwamba Kizota

Maajabu ya fundi wa mpira, Said Mwamba Kizota

Cesar Saint

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2016
Posts
423
Reaction score
726
Leo nikiwa maeneo fulani nikiwa nafuatilia mchezo wa CHAN kati ya Tanzania na Sudan nikawa napata story fupi ya mpira yenye kusisimua kuhusu mchezaji wa zamani wa Yanga marehemu mzee SAID NASSOR MWAMBA KIZOTA .

IMG_4900.JPG

IMG_4896.JPG

Unaambiwa ilikuwa mwaka 1993 ndio mwaka ambao fundi huyu aliwapa burudani mashabiki wa Yanga na kumfanya kuwa kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo.

IMG_4902.JPG

Basi kipindi hicho Yanga ikiwa inajiandaa kuvaana na Sport Club Villa ya Uganda katika fainali ya klabu bingwa afrika mashariki na kati mjini Kampala Uganda.

IMG_4906.JPG

Timu ilikuwa imeshaondoka na kutangulia nchini Uganda jamaa alikuwa anaendelea na mishe zake akiwa na tuhuma za kupiga ulabu alipokuwa kambini basi akawa amepoa kwa dada yake maeneo ya mwembe yanga aitwaje White Mama (jina maarufu)

Basi watu wa Yanga baada ya kujishauri muda mrefu wakamfuata na kumchukua mahali hapo na kumpeleka nchini Uganda kuamkia siku ya fainali.

Siku ilipofika jamaa bila kufanya mazoezi ya pamoja na timu akaingia mzigoni akaweka kamba mbili wavuni huku goli la tatu la Yanga likifungwa na Lunyamila hivyo kuifanya Yanga kutawazwa ubingwa mbele ya SC Villa nchini Uganda Kizota akarudi na ufungaji bora wa michuano hii na katika mwaka huo huo akabeba kiatu cha ufungaji bora ligi kuu ya Tanzania bara kipindi ikidhaminiwa na TBL.

Mechi kubwa iliyoacha historia kipindi hicho ni ilipowakutanisha watani wa jadi Kizota alipiga goli mbili huku moja ya goli maridhawa akimchambua na kumfanya atakavyo goli kipa mahili wa wakati huo Mohamed Mwameja .

Wakati mwengine fundi huyu alitupiwa virago na wana Jangwani kwa tuhuma za kuhujumu timu walipopokea kipigo cha 4-1 kutoka kwa Simba na Kizota akadondokea Simba

IMG_4907.JPG

Kizota Vs Mmachinga

Mwaka 1995 ;Wakali hawa wa kufumania nyavu na kuchezea mpira walikutana katika Mbungi ya kkoo moto ulikuwa mkali pale ambapo Mmachinga alipopachika goli la kuwapa Yanga uongozi kipindi cha kwanza,wakati Yanga wakijua turubai limehamia kwa jirani Kizota anapiga goli maridadi la kusawazisha na kuwachanganya Yanga ambao kutahamaki wanapigwa kamba ya pili na Mchunga Bakari ‘Mandela’ kukamilisha hesabu ya 2-1 na mchezo kuishia hivyo.

IMG_4903.JPG

YANGA WAMPIGIA MAGOTI
Yanga walitambua makosa yao na kumsotea Fundi huyu wa mpira na kwa vile alikuwa akiishi maeneo hayo ya mitaa ya Jangwani haikuwa kazi sana kumpata na kumvisha tena uzi wa watoto wa Jangwani kwa mara nyingine.

IMG_4905.JPG

AKUTANA TENA NA SIMBA
Kizota anakutana tena na Simba mwaka 1996 na kushiriki katika matokeo ya sare ya maajabu jijini Arusha 4-4

IMG_4897.JPG

Hahah kuna hili la kizota na waarabu jamaa alienda uarabuni na kupiga mpira wakina maradona jamaa wakamtaka hadi abadilishe uraia usifanye masihara moto anaouwasha mtu mpaka waarabu waelewe somo (hii ni stori nyingine)

Kizota pia amechezea timu ya taifa na kupata mafanikio ikiwemo challenge cup

Fundi huyu wa mpira alifariki dunia tar 11/02/2007 kwa ajali ya gari maeneo ya Veterinary akitokea kushuhudia mchezo wa marudiano, Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, Raundi ya Awali kati ya wenyeji Simba dhidi ya Textil de Pungue ya Msumbiji ulioisha kwa Simba kutolewa kwa njia ya matuta 3-1 baada ya sare pacha ya 1-1 .

IMG_4895.JPG

IMG_4899.JPG

View attachment 1213794

Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya fundi huyu wa mpira na wengine wengi waliotangulia mbele ya haki.

Timu alizopitia Kizota ni pamoja na Shirika la posta Tabora (wakiti huo ikijulikana kama Posta na Simu) ,Yanga,Simba,Al Nasar ya Oman na Al Jazeera ya uarabuni Abu Dhabi.

Hebu tupia hapa kisa chochote unachofahamu au kusikia kuhusiana na wachezaji wa zamani wa Tanzania kama Sunday Manara ‘Computer’ ,Zamoyoni Mogella ‘Golden Boy’ ,Maulid Dilunga ‘Mexico’Juma Pondamali ‘Mensa’ ,Omar Hussein ‘Keegan’, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ ,Ezekiel Greyson ‘Jujuman’ ,Ally Yusufu ‘Tigana’ ,Athuman China na wengine wengi
 
Yaani mpira ulikuwa zamani huyu alikuwa anauwezo wa kuwa beki na kuwa mshambuliaji hatareee ,binafsi niliacha kushadadia,kubishana,na kuhudhuria uwanja wa taifa baada ya LUNYAMILA kustaafu mpira

Hawa jamaa wameondoka huku wakiudai mpira
 
Ukitazama maumbo ya Wachezaji wa zamani na wa Sasa hivi utagundua kuna Tatizo kubwa sana siku hizi

Sio tatizo mkuu , acheni kukariri.

Mifumo ya mpira imebadilika sana , sahizi mpira hauchezwi na Giants, mpira unachezwa na watu wenye maumbo madogo , haya Mapinduzi yalianza kufanyika Barcelona wakiifuata falsafa ya Cruyf..

Nenda England kaangalie Man city wanavyowasha Moto, angalia maumbo ya wachezaji kama Bernard Silva, sterling, Aguero, Gundogan n.k, wachezaji wadogo wadogo kiumbo ni ngumu kuwakaba na pili wana mbio balaa , hao MaGiant wenu wa zamani kwa mpira wa sahizi wangeweza kujiharishia uwanjani maana wangekimbizwa kwa kugongewa pasi kama 800 hivi fupi fupi mpaka wauone Moto.
 
Yaani mpira ulikuwa zamani huyu alikuwa anauwezo wa kuwa beki na kuwa mshambuliaji hatareee ,binafsi niliacha kushadadia,kubishana,na kuhudhuria uwanja wa taifa baada ya LUNYAMILA kustaafu mpira
Hao zamani walileta kombe gani na liko wapi? mbona Afrika magharibi wakati huo walikuwa wanacheza mpira wa kulipwa Ulaya tuambie hao waliokuwa hatari walicheza sehemu gani duniani. Usilete zile story za babu za kujifanya kuwa enzi zake alikuwa anaweza masomo yote kumbe alikuwa kilaza tuu
 
Sio tatizo mkuu , acheni kukariri.

Mifumo ya mpira imebadilika sana , sahizi mpira hauchezwi na Giants, mpira unachezwa na watu wenye maumbo madogo , haya Mapinduzi yalianza kufanyika Barcelona wakiifuata falsafa ya Cruyf..

Nenda England kaangalie Man city wanavyowasha Moto, angalia maumbo ya wachezaji kama Bernard Silva, sterling, Aguero, Gundogan n.k, wachezaji wadogo wadogo kiumbo ni ngumu kuwakaba na pili wana mbio balaa , hao MaGiant wenu wa zamani kwa mpira wa sahizi wangeweza kujiharishia uwanjani maana wangekimbizwa kwa kugongewa pasi kama 800 hivi fupi fupi mpaka wauone Moto.

Mimi nazungumzia umbo lililokosa Lishe na kujengeka kimichezo Wewe unazungumzia Size na Ukubwa wa Mwili
 
Ungesoma kwanza huu uzi vizuri mbona timu alizocheza ndani na nje ya Tanzania nimeziainisha.

Licha ya kuwa mazingira ya mpira ya nyakati hizo si sawa na ya sasa lakini hapa tunaongelea miongoni mwa kipaji bora kuwahi kutokea Tanzania.

Top scorer wa ligi kuu Tanzania bara
Top scorer cecafa

Na hata alipoenda Abu Dhabi walitaka kumpa uraia ili achezee timu yao moto wa huyu bwana ulikuwa si wa kitoto.

Sikulazimishi uamini katika mawazo yangu au facts nilizozileta hapa kama ubora kwako ni kucheza ulaya basi hata pele si bora kwa maana hakufanikiwa kucheza Ulaya zaidi ya kuishia Marekani
 
Mimi nazungumzia umbo lililokosa Lishe na kujengeka kimichezo Wewe unazungumzia Size na Ukubwa wa Mwili

Ukizungumzia lishe ni wazi kabisa picha ya marehemu Kizota zinaonyesha hakuwa na physical fitness kulinganisha na players wetu wa sasa .

Kwenye picha utaona mwili mkubwa ambao haujajengeka kabisa, no wonder inasemekana alikuwa anapiga sana pombe
 
Ungesoma kwanza huu uzi vizuri mbona timu alizocheza ndani na nje ya Tanzania nimeziainisha.

Licha ya kuwa mazingira ya mpira ya nyakati hizo si sawa na ya sasa lakini hapa tunaongelea miongoni mwa kipaji bora kuwahi kutokea Tanzania.

Top scorer wa ligi kuu Tanzania bara
Top scorer cecafa

Na hata alipoenda Abu Dhabi walitaka kumpa uraia ili achezee timu yao moto wa huyu bwana ulikuwa si wa kitoto.

Sikulazimishi uamini katika mawazo yangu au facts nilizozileta hapa kama ubora kwako ni kucheza ulaya basi hata pele si bora kwa maana hakufanikiwa kucheza Ulaya zaidi ya kuishia Marekani

Kwanini hakupewa uraia?

I’m curious.
 
hicho ndo kizazi kilichosababisha mzee ruksa atubatize tanzania kama kichwa cha mwendawazimu. ni wachezji waliokuwa wanajua kucheza mpira wa ridhaa na sio ufundi.. maguvu meeengi bila kutumia akili. tukicheza na timu za nje tulikuwa tunakula nyingi sana. cjui mnawasifia kwa lipi.. labda kwa sababu walikuwa wanasikika sana kwenye redio za mkulima...
 
Kwanini hakupewa uraia?

I’m curious.

Acha tu nikueleze ijapokuwa nilipanga kulielezea hili katika uzi mwengine;

Kwa ufupi ni kuwa Kizota alijiunga Yanga mwaka 1988 akitokea timu ya shirika la Posta na Simu Tabora na aliwasha moto kiasi cha kuwavutia waarabu sio wale wa Misri hapana bali timu ya Al Jazeera ya Abu Dhabi .

Alipofika uarabuni alikutana na mapro wengine na kuendelea kuwasha moto ;Kitu cha kipekee hapa ni kuwa huyu bwana alihama kutoka nafasi ya kiungo na kuunganisha nguvu na Mmalawi mmoja huko katika safu ya ushambuliaji wakatengeneza ufalme katika ardhi ya waarabu.

Kutokana na moto wake ndio jamaa wakaanza chokochoko za kutaka kumpa uraia (story za kijiweni zinasema walitaka kumtunuku na mke hahaha) Kizota akawaomba mabosi wake ruhusa aje kujadiliana na familia.

Fundi huyu alipofika bongo familia ikaweka ugumu na kutokana na sehemu kubwa ya maisha yake kuwa familia akaamua kuachana na swala la kufuatilia uraia wa uarabuni.

Nikuachie hapa chief huyu jamaa kuna kisa kinaendelea hapa aliwachachafya waarabu mpaka wakamfuata kumzoa huku ligi inaendelea chuma kimeshatupia kamba za kutosha na kuifanya yanga kuchukua ubingwa wa ligi
 
hicho ndo kizazi kilichosababisha mzee ruksa atubatize tanzania kama kichwa cha mwendawazimu. ni wachezji waliokuwa wanajua kucheza mpira wa ridhaa na sio ufundi.. maguvu meeengi bila kutumia akili. tukicheza na timu za nje tulikuwa tunakula nyingi sana. cjui mnawasifia kwa lipi.. labda kwa sababu walikuwa wanasikika sana kwenye redio za mkulima...

Brother naomba nikwambie kitu kauli kamili ya Mzee Mwinyi ilikuwa “Tanzania (hapa akiongelea timu za mpira zilizokuwa zinashiriki michuano ya kimataifa) ni kama kichwa cha mwenda wa zimu,Kila anayetaka kujifunza kunyoa hujifunzia “

Hii ilitokana na matokeo mabovu ya timu yetu ya taifa na hata zile za vilabu katika michuano ya kimataifa na nikukumbushe tu wakati huu Tanzania ilikuwa katika viwango bora vya FIFA ukilinganisha na sasa.

Kwa muktadha wa wanamichezo wetu kushindwa kuelewa na kutambua uwezo wao nadhani hapa ndio akaweka neno mwendawazimu

Maana uwezo tulikuwa nao wa kufika mbali na sapoti ilikuwepo kuanzia kambi za kimataifa kwaajili ya maandalizi nk
 
Hao zamani walileta kombe gani na liko wapi? mbona Afrika magharibi wakati huo walikuwa wanacheza mpira wa kulipwa Ulaya tuambie hao waliokuwa hatari walicheza sehemu gani duniani. Usilete zile story za babu za kujifanya kuwa enzi zake alikuwa anaweza masomo yote kumbe alikuwa kilaza tuu
Kwa ngazi ya afrika ya mashariki na kati kubeba kombe la klabu bingwa Mara mbili ni Hatua ambayo kizazi cha sasa kufikia ni ndoto vilevile kubeba kombe la challenge ugenini ni ndoto kwa kizazi cha sasa. Maajabu sasahivi wachezaji wanapata ela nyingi lakini hawa perform
 
Sio tatizo mkuu , acheni kukariri.

Mifumo ya mpira imebadilika sana , sahizi mpira hauchezwi na Giants, mpira unachezwa na watu wenye maumbo madogo , haya Mapinduzi yalianza kufanyika Barcelona wakiifuata falsafa ya Cruyf..

Nenda England kaangalie Man city wanavyowasha Moto, angalia maumbo ya wachezaji kama Bernard Silva, sterling, Aguero, Gundogan n.k, wachezaji wadogo wadogo kiumbo ni ngumu kuwakaba na pili wana mbio balaa , hao MaGiant wenu wa zamani kwa mpira wa sahizi wangeweza kujiharishia uwanjani maana wangekimbizwa kwa kugongewa pasi kama 800 hivi fupi fupi mpaka wauone Moto.
Wale wachezaji wa ulaya hawana maumbo madogo kama wa kwetu.Vp Ban Dijk na Koulibaly,Kompany etc
 
Wale wachezaji wa ulaya hawana maumbo madogo kama wa kwetu.Vp Ban Dijk na Koulibaly,Kompany etc

Nitajie timu kubwa ulaya iliyojaa Giants....

Ukinitajia kina VVD, nitakutajia kina firmino, keita,Mane, Salah , Xhaqiri na wengineo ambao sio Giants...

Every General rule has exceptions.
 
Mashindano yote mawili ya 93 na 98 wasededi alishiriki mwanzo mwisho tena hilo la 98 alianza kama mshambuliaji nadhani ilikuwa game na APR tukala thalatha ndipo mtu yule mkubwa akaamua kujibadilishia majukumu na kuwa kitasa. Game ambayo nakumbuka almarhumu huyu alitolewa bar na kupandishwa ndege ilikuwa baina yetu na pamba ya mwanza ndipo tukio hilo lilitokea na alifanya yake siku hiyo
 
Back
Top Bottom