Maajabu ya jiji la Kampala

K Izungu ndio lugha gani?
 
Tupe utofauti wa maisha kati ya kampala na Dar? (Lifestyle,maendeleo ,watu) etc
GoldDhahabu
Kwa jinsi nionavyo,
1. Dar kumeendelea zaidi ya Kampala, ingawa Kampala kumepangika vizuri zaidi. Labda kwa vile sijatembelea maeneo yote, ila mpaka sasa sijayaona mazingira ya "Uswahilini". Nafikiri naeleweka nikisema "Uswahilini"
2. Watu wa huku ni wachapa kazi. Wapo busy sana.
3. Sijui kama kuna watoto wa "mitaani", sijakutana nao huku. Labda sijafika mitaa wanapopendelea
4. Ni waelewa. Ukimwuliza mtu kitu, kama anafahamu, atakuelekeza vizuri
 
Kaulizie chakula kinaitwa Rolex, hakipatikan mgahawani ni vijana barabarani wanakaanga chapati Inakunjwa Kwenye mayai ni very cheap. Wape hi ba sebo na wanyabo
Rolex nilishasoma kwenye magazeti nikiwa "nyumbani". Nitaitafuta leo.

"Wa sebo na wanyabo" ni nini
 
Ndio saizi huwezi kupigwa, elfu 1 nadhani wanaita Lukumi. Polepole ni mpola mpola, hao boda usiku wengi wanakuwa maji unakuta anakuita sebo(mwanaume) tugende(twende). Wewe unamuita Janguu(njoo) sebo
Kwa nini hukuniambia hayo kabla sijaja huku?😀

Kuna raha kufahamu lugha ya wenyeji wako, alau misamiati ya muhimu kama salam na jinsi ya kuuliza au kuomba kitu.
 
Nilifanya kazi katika kampuni ambayo nilideal na waganda.

Nashindwa kuelewa mleta uzi anaposema waganda ni wachapakazi, nitatoa mfano: Ikinyesha mvua mganda haendi kazini wala shambani, wanahusudu kula bata mno, akiwa ana pesa anatakiwa kulipa deni au kula bata atachagua kula bata, mostly wanaishi kwa kumaanisha kesho itajitegemea
 
Kwa kuwa ulishafanya nao kazi, siwezi kukubishia. Ila pia na Mimi nilishafanya kazi na mmoja miaka ya nyuma. Yeye peke yake ndiye aliyekuwa Mganda kwenye taasisi yetu. Alikuwa mchapa kazi sana japo sijui kama hiyo ilikuwa ni tabia yake binafsi au alinadilishwa na mazingira.

Kilichonifanya niwaone wa huku ni wachapa kazi ni baada ya kushuhudia maduka na mama lishe yamesahafunguliwa saa kumi na mbili Asubuhi, na mama lishe kuivisha chakula mapema sana Asubuhi.
 
Hivi kuna boti au meli za abiria za kwenda Tz kutokea Uganda?
 
Asante sana mkuu
 
Kitu kingine kuhusu waganda , hoja ya uchapakazi hii haipo kwa miaka miwili niliokaa kule kwani starehe kwao ni kipaumbele kikubwa ,wanaishi wakiwaza sana kutoka nchini kwao wakiamini kutoboa zaidi.Hawajitumi ila ni wajanja wajanja sana na ukikaa vibaya watakupiga ,tabia ya udokozi kwa vitu vidogo vidogo kwao ni kawaida.
Ngono ni kitu simple sana kwani wanakauzungu flani hata dem akikuelewa anakufata anakueleza uhalisia kua anakutaka .
Bidhaa zao sijui ni kwa nn ila nyingi ni org kwa asilimia 100, copy ni chache labda miaka hii ya sasa .Kama taifa kl Waganda ni kabila kubwa ila wanawabagua sana makabila mengine .
Kujiunga UPDF (jeshini ), kiswahili ilikua sifa ya ziada
 
Hiyo namba 8, hicho chakula cha asubuhi asubuhi kinaitwa *akatogo"! Saa nne ndio Waganda wanakunywa chai.
 
Nimesoma huko Uganda shule moja inaitwa Eagle's Nest iko meko hapo Kati Kati ya jiji karibu na ikulu ya kabaka, miaka ya 2006 - 2009. Nilipapenda ug.

Kwangu Kampala ndo jiji namba moja. Manyabo wa kule Wana nyash za hataree.
Eagle's nest umenikumbusha mbali sana aisee. Nmesoma Ntinda View mitaa ya Ntinda. Nakawa unaingia kushoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…