Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Izungu ndio lugha gani?1. Si kubwa kama jiji la Dar Es Salaam, lakini ningeambiwa nichague pa kuishi, ningepapendelea Kampala kutokana na hali yake ya hewa nzuri
2. Lugha ya Kiganda ndiyo imetawala kuanzia kwenye maredio na mitaani. Kizungu hutumika kinapohitajika
3. Kuna maeneo kuna Waswahili pia. Kuna mahali nimepita leo kwenye gesti moja nikakuta watu wanaongea Kiswahili. Nikipata muda nitaenda kuwauliza kama ni Watz au la. Kwenye ubao wa matangazo wa hiyo gesti, matangazo yamewekwa kwa lugha ya Kingereza na Kiswahili
4. Kuna mitaa pikipiki ni nyingi sana. Uliiona zikipita barabarani unaweza kufukiri zipo kwenye maadamano ya "chama"
6. Huenda boda boda wa huku nao wapo rafu katika uendeshaji pikipiki kama wa Bongo. Nimeshuhudia zikipuuzia kuzingatia taa za kuongozea magari. Ni tofauti na boda boda wa Kigali ambao inasemekana ni watiifu sana wa Sheria za barabarani
7. Inawezekana ndilo jiji la Afrika Mashariki linaloongoza kwa mabinti kuvaa vimini. Unakuta mwingine kimini chake ni kifupi sana kiasi kwamba akitaka kupanda boda boda inamlazimu awe na koti la kufunikia mapaja ili kujisitiri. Sijui ni utamaduni wao au ni "Uzungu" umewakolea?
8. Watu ni wachapa kazi. Ni kawaida kukuta maduka yaliyo pembezoni mwa mji yameshafunguliwa saa kumi na mbili Asubuhi, na muda huo mama lishe naye ameshaivisha chakula
9. Utamaduni wao kwenye matumizi ya Vyuo unaweza kuendana na Wakenya, ingawa Wakenya wanaweza wakawa "more advanced". Katika gesti kadhaa nilizolala, hakuna kopo la chooni wala toilet paper. Uzoefu wangu kwenye gesti za Kenya ni kwamba vyoo, hata vile vya umma(vya kulipa), lazima viwe na toilet paper. Lakini kwa Waganda sikuziona toilet paper wala kopo. Nazungumzia gesti za gharama nafuu na siyo mahoteli
10. Gesti za kawaida zinagharimu wastani wa Ugx 20,000 mpaka 30,000. Lakini ukienda nje ya mji, unaweza kupata mpaka Ugx 20,000 (self) na Ugx 13,000 (single)
11. Ndizi (matoke) ni chakula "common" huku
12. Wali wa huku ni kama pilau. Nimeshakula pilau zaidi ya mara moja, lakini mara zote nilipoagiza wali, nililetewa "pilau"
13. Kwa baadhi ya niliongea nao, hasa wale waliokwishafika Tanzania, wanaamini Serikali ya Tanzania inawajali raia wake kuliko ya Uganda😄. Mfano mojawapo waliotumia ni gharama za Internet. Wanadai internet ya Tanzania ni nafuu sana ukilinganisha na ya Uganda
14. Nimeshangazwa pia na chipsi mayai za huku. Chipsi kavu zilipashwa kivyake na mayai yakakaangwa kivyake. Sijui ndiyo kawaida ya huku au ni kwangu tu ndiyo waliamua kufanya hivyo!
NB. Ni "maajabu" kwangu tu ambaye bado "mgeni"
Kwa jinsi nionavyo,Tupe utofauti wa maisha kati ya kampala na Dar? (Lifestyle,maendeleo ,watu) etc
GoldDhahabu
Rolex nilishasoma kwenye magazeti nikiwa "nyumbani". Nitaitafuta leo.Kaulizie chakula kinaitwa Rolex, hakipatikan mgahawani ni vijana barabarani wanakaanga chapati Inakunjwa Kwenye mayai ni very cheap. Wape hi ba sebo na wanyabo
Kwa nini hukuniambia hayo kabla sijaja huku?😀Ndio saizi huwezi kupigwa, elfu 1 nadhani wanaita Lukumi. Polepole ni mpola mpola, hao boda usiku wengi wanakuwa maji unakuta anakuita sebo(mwanaume) tugende(twende). Wewe unamuita Janguu(njoo) sebo
Kikomandoo kikoje mkuu?Bado hujazungumzia vyakula vyao maarufu mitaani Kama Kikomandoo (chikomandoo) na Rolex (chapati na mayai).
English!K
Izungu ndio lugha gani?
Sebo ni mwanaumeRolex nilishasoma kwenye magazeti nikiwa "nyumbani". Nitaitafuta leo.
"Wa sebo na wanyabo" ni nini
Kwa kuwa ulishafanya nao kazi, siwezi kukubishia. Ila pia na Mimi nilishafanya kazi na mmoja miaka ya nyuma. Yeye peke yake ndiye aliyekuwa Mganda kwenye taasisi yetu. Alikuwa mchapa kazi sana japo sijui kama hiyo ilikuwa ni tabia yake binafsi au alinadilishwa na mazingira.Nilifanya kazi katika kampuni ambayo nilideal na waganda.
Nashindwa kuelewa mleta uzi anaposema waganda ni wachapakazi, nitatoa mfano: Ikinyesha mvua mganda haendi kazini wala shambani, wanahusudu kula bata mno, akiwa ana pesa anatakiwa kulipa deni au kula bata atachagua kula bata, mostly wanaishi kwa kumaanisha kesho itajitegemea
🙏🙏🙏Sebo ni mwanaume
Nyabo ni mwanamke
OkayEnglish!
Hivi kuna boti au meli za abiria za kwenda Tz kutokea Uganda?Ni mji karibu na Ziwa Victoria kuna bandari kubwa inaitwa Port Bell, meli za kutoka Tanzania(Mwanza,Bukoba,Mara),Kenya( Kisumu) zinashusha mizigo na abiria hapo.
Sio mbali na Kampala, ukiwa na nafasi weekend ukatembee kuna waganda wanafanya booking boat za kuwatembeza ziwani na hapo ndio utakutana na wafanyabiashara kutoka Mwanza na Bukoba wakileta bidhaa na kutoa mizigo huko kuja Tanzania
Hamna ruti hio ukipanda meli either ushuke bukoba au kemondo ndio uende mutukula, meli unaanzia mwanzaHivi kuna boti au meli za abiria za kwenda Tz kutokea Uganda?
Asante sana mkuuSijui nauli ya kutokea Dar. Kama unataka "kuja" Kampala, panda basi hadi Mwanza ukashangae kwanza miamba ya jijini Mwanza ndipo uendelee na safari ya Kampala.
Na kama utaanzia safari Mwanza kwa magari ya kuunga unga kama nilivyofanya, utapanda gari kutoka Mwanza hadi Katoro (Geita) Tsh 8,000/=.
Katoro hadi Bukoba Tsh 20,000/=
Kutoka Bukoba Mjini utachkua daladala hadi Mutukula Tsh 4,000/=.
Mutukula ukishagongewa mihuri, unaweza ukavuka mpaka kwa miguu kuingia upande wa Uganda kwenda ziliko hiace (Waganda huziita taxi), au uchukue bodaboda Tsh 1,000/= au Tsh 2,000/=, lakini wakikuona wewe ni wa kuja, bodaboda wanaweza wakakuambia hata Tsh 5,000/=.
Kabla ya kuvuka kwenda upande wa Uganda, ni vizuri ukabadilisha hela upate za Kiganda, na pia ukasajili line ya Uganda, mfano MTN (Vodacom). Kama una passport kubwa (siyo EMERGENCY TRAVEL DOCUMENT) unaweza ukasajili line yako kwa jina lako hapo hapo Mutukula upande wa Tanzania, gharama ni Tsh 3,000/=, lakini kama unatumia EMERGENCY TRAVEL DOCUMENT, watakupatia line iliyokwishasajiliwa kwa jina la mtu mwingine kwa Tsh 10,000/=, ila wakikuona wewe ni mtoaji mzuri watakuambia Tsh 15,000/=.
Ukishaingia upande wa Uganda, utapanda "taxi" kwa hela ya Kiganda Ugx 40,000 Mutukula hadi Kampala. Ingawa nauli ni Ugx 40,000/= , mimi nililipa Ugx 35,000/=, na mtu mwingine alilipa Ugx 30,000/=. Wakati wa kurudi nitabargain hadi na mimi nipande kwa Ugx 30,000/=.
Hiyo namba 8, hicho chakula cha asubuhi asubuhi kinaitwa *akatogo"! Saa nne ndio Waganda wanakunywa chai.1. Si kubwa kama jiji la Dar Es Salaam, lakini ningeambiwa nichague pa kuishi, ningepapendelea Kampala kutokana na hali yake ya hewa nzuri
2. Lugha ya Kiganda ndiyo imetawala kuanzia kwenye maredio na mitaani. Kizungu hutumika kinapohitajika
3. Kuna maeneo kuna Waswahili pia. Kuna mahali nimepita leo kwenye gesti moja nikakuta watu wanaongea Kiswahili. Nikipata muda nitaenda kuwauliza kama ni Watz au la. Kwenye ubao wa matangazo wa hiyo gesti, matangazo yamewekwa kwa lugha ya Kingereza na Kiswahili
4. Kuna mitaa pikipiki ni nyingi sana. Uliiona zikipita barabarani unaweza kufukiri zipo kwenye maadamano ya "chama"
6. Huenda boda boda wa huku nao wapo rafu katika uendeshaji pikipiki kama wa Bongo. Nimeshuhudia zikipuuzia kuzingatia taa za kuongozea magari. Ni tofauti na boda boda wa Kigali ambao inasemekana ni watiifu sana wa Sheria za barabarani
7. Inawezekana ndilo jiji la Afrika Mashariki linaloongoza kwa mabinti kuvaa vimini. Unakuta mwingine kimini chake ni kifupi sana kiasi kwamba akitaka kupanda boda boda inamlazimu awe na koti la kufunikia mapaja ili kujisitiri. Sijui ni utamaduni wao au ni "Uzungu" umewakolea?
8. Watu ni wachapa kazi. Ni kawaida kukuta maduka yaliyo pembezoni mwa mji yameshafunguliwa saa kumi na mbili Asubuhi, na muda huo mama lishe naye ameshaivisha chakula
9. Utamaduni wao kwenye matumizi ya Vyuo unaweza kuendana na Wakenya, ingawa Wakenya wanaweza wakawa "more advanced". Katika gesti kadhaa nilizolala, hakuna kopo la chooni wala toilet paper. Uzoefu wangu kwenye gesti za Kenya ni kwamba vyoo, hata vile vya umma(vya kulipa), lazima viwe na toilet paper. Lakini kwa Waganda sikuziona toilet paper wala kopo. Nazungumzia gesti za gharama nafuu na siyo mahoteli
10. Gesti za kawaida zinagharimu wastani wa Ugx 20,000 mpaka 30,000. Lakini ukienda nje ya mji, unaweza kupata mpaka Ugx 20,000 (self) na Ugx 13,000 (single)
11. Ndizi (matoke) ni chakula "common" huku
12. Wali wa huku ni kama pilau. Nimeshakula pilau zaidi ya mara moja, lakini mara zote nilipoagiza wali, nililetewa "pilau"
13. Kwa baadhi ya niliongea nao, hasa wale waliokwishafika Tanzania, wanaamini Serikali ya Tanzania inawajali raia wake kuliko ya Uganda😄. Mfano mojawapo waliotumia ni gharama za Internet. Wanadai internet ya Tanzania ni nafuu sana ukilinganisha na ya Uganda
14. Nimeshangazwa pia na chipsi mayai za huku. Chipsi kavu zilipashwa kivyake na mayai yakakaangwa kivyake. Sijui ndiyo kawaida ya huku au ni kwangu tu ndiyo waliamua kufanya hivyo!
NB. Ni "maajabu" kwangu tu ambaye bado "mgeni"
Eagle's nest umenikumbusha mbali sana aisee. Nmesoma Ntinda View mitaa ya Ntinda. Nakawa unaingia kushoto.Nimesoma huko Uganda shule moja inaitwa Eagle's Nest iko meko hapo Kati Kati ya jiji karibu na ikulu ya kabaka, miaka ya 2006 - 2009. Nilipapenda ug.
Kwangu Kampala ndo jiji namba moja. Manyabo wa kule Wana nyash za hataree.