Asa
Ubarikiwe sana Mkuu
Nimejifunza vitu vingi kupitia uzi huu!
Nauli ya basi kutokea Dar ni Bei gani? Na hupitia mikoa Gani hadi kufika huko?
Sijui nauli ya kutokea Dar. Kama unataka "kuja" Kampala, panda basi hadi Mwanza ukashangae kwanza miamba ya jijini Mwanza ndipo uendelee na safari ya Kampala.
Na kama utaanzia safari Mwanza kwa magari ya kuunga unga kama nilivyofanya, utapanda gari kutoka Mwanza hadi Katoro (Geita) Tsh 8,000/=.
Katoro hadi Bukoba Tsh 20,000/=
Kutoka Bukoba Mjini utachkua daladala hadi Mutukula Tsh 4,000/=.
Mutukula ukishagongewa mihuri, unaweza ukavuka mpaka kwa miguu kuingia upande wa Uganda kwenda ziliko hiace (Waganda huziita taxi), au uchukue bodaboda Tsh 1,000/= au Tsh 2,000/=, lakini wakikuona wewe ni wa kuja, bodaboda wanaweza wakakuambia hata Tsh 5,000/=.
Kabla ya kuvuka kwenda upande wa Uganda, ni vizuri ukabadilisha hela upate za Kiganda, na pia ukasajili line ya Uganda, mfano MTN (Vodacom). Kama una passport kubwa (siyo EMERGENCY TRAVEL DOCUMENT) unaweza ukasajili line yako kwa jina lako hapo hapo Mutukula upande wa Tanzania, gharama ni Tsh 3,000/=, lakini kama unatumia EMERGENCY TRAVEL DOCUMENT, watakupatia line iliyokwishasajiliwa kwa jina la mtu mwingine kwa Tsh 10,000/=, ila wakikuona wewe ni mtoaji mzuri watakuambia Tsh 15,000/=.
Ukishaingia upande wa Uganda, utapanda "taxi" kwa hela ya Kiganda Ugx 40,000 Mutukula hadi Kampala. Ingawa nauli ni Ugx 40,000/= , mimi nililipa Ugx 35,000/=, na mtu mwingine alilipa Ugx 30,000/=. Wakati wa kurudi nitabargain hadi na mimi nipande kwa Ugx 30,000/=.