Maajabu ya kutisha ya Mto Rutale (Chemchem ya Rutale) - Kigoma Ujiji

Maajabu ya kutisha ya Mto Rutale (Chemchem ya Rutale) - Kigoma Ujiji

German tricks,illusion water,illusion snakes, the near by area there is a stocks of treasures,note me!, in HUGE AND ABUNDANT...!
Jamaa walikuwa na uwezo wa kuficha kitu na kuanzisha chemchem isiyo na kichwa wala miguu.,usitafiti haya wala kuumiza kichwa chako!
Intelligence inaniambia kabla ya kuizamisha meli yao iliyokuwa imesheheni Mali walipakuwa Mali zote wakaficha wajuavyo kisha wakazamisha chini.
 
Miondoko hii ya maandishi haijafanyiwa utafiti wowote bali ni nadharia za kusikika kutoka kwa mashuhuda mbalimbali kunako mtikisiko wa maajabu ya chemchem hii kongwe ya Kanyabeza inayopatikana eneo la Rutale, pia unaweza kuita chemchemya Rutale hivyo unaruhusiwa kupinga au kukubali, kupunguza au kuongeza pale kwenye mapungufu.

View attachment 2364065

Rutale ni jina la chechem inayopatikana mkoani Kigoma, manispaa ya Kigoma Ujiji, kata ya Kipampa, eneo linaloitwa Rutale ambalo lipo karibu kabisa na ziwa Tanganyika mwambao wa Ujiji.
Jina Rutale inasemekana lilitokana na mkazi mmoja aliekuwa akiishi mahala hapo miaka mingi iliyopita, watu walikuwa wakija kuchota maji kwenye chemchem hii walikuwa wakisema tunakwenda kuchota maji kwa Rutale.

View attachment 2364068

Maji yake ni mazuri kwa kunywa, yenye baridi ya asili na yenye utulivu kwenye koo ambayo hukuacha na ladha itayokufanya uyakumbuke na kuyahitaji tena baadae. Sifa ya kipekee ya mto huu hata mvua inyeshe namna gani maji yake hayachafuki abadan, chemchem hii haijawahi kukauka tangu kuumbwa kwake, inatiririsha maji yake kuelekea ziwa Tanganyika ambapo pembezoni mwa mfereji kumelimwa nyanya na mazao mbalimbali, kilimo cha nyanya eneo hili kinakubali mno ikiwa tu nyanya zitamwagiliziwa kwa maji ya rutale. Barabara ya Rutale inatokea kwenye barabara kuu ya Kigoma Ujiji sehemu inayoitwa 'Bimala'

View attachment 2364072

Inasemekana mnamo miaka ya 1950 eneo hili lilikuwa linaaminika kuwepo kwa joka kubwa lenye pete ya dhahabu mkiani, nyoka huyu alikuwa akifanya safari zake baina ya Rutale na pori la uwanja wa Lake Tanganyika enzi hizo, inamaanisha huyu nyoka alikuwa akisafiri kutoka eneo hilo la rutale na kuvuka barabara ya Kigoma ujiji sehemu inayoitwa Mnarani, kwenye kona ambayo ukichomoza na gari unaanza kuiyona ujiji'

View attachment 2364082


Hii ndio sehemu nyoka huyu alikuwa akivuka na hii ndio sehemu iliyokuwa ikiongoza kwa matukio ya ajali za barabarani mara kwa mara kama gari kupinduka au magari kugongana au mtu kugongwa, inasemekana ajali hizi zilikuwa zikisababishwa na nyoka huyu wakati akivuka eneo hilo ambapo akikukuta ni lazima upate ajali.

View attachment 2364080

Nyoka huyu kutoka chemchem ya Rutale inasemekana pindi atokapo kunakuwa na upepo mwingi unavuma mfano wa kimbunga cha vumbi.

Nyoka huyu Rutale inasemekana alikuwa na uhusiano na nyoka wa Burega aliekuwa akienda kunywa maji kwenye mto Katubuka, nyoka wa Burega alikuwa akivuka barabara ya Kigoma Ujiji eneo la Mwanga selemala ambayo pia ni sehemu iliyokuwa ikiongoza kwa ajali za mara kwa mara. Vijana waliokuwa wakipotea kimazingara kwenye mto katubuka inakisiwa walikuwa wakichukuliwa na nyoka huyu wa Burega.

View attachment 2364085

Maji ya rutale inasemekana hayafahamiki haswa yanatoka wapi, yani chemchem ilipo haifahamiki ipo wapi lakini ni eneo kwa ujumla limelozungukwa na nyasi, maji ya rutale yalikuwa yakiuzwa kwenye madebe ya bati ambapo muuzaji hubeba madebe mawili yaliyoshikiliwa na mti mgumu kwenye bega la kulia na kushoto, pia muuzaji huvaa kengere za asili miguuni pindi anapoanza kuyatembeza maji haya kwenye mitaa, kengere zinamlio wakipekee ambao huamsha masikio ya msikilizaji na kufahamu kwamba maji ya ratule yanapita,

View attachment 2364091

Mzegamzega alikuwa ni yule muuza maji ya rutale ambae anabeba madebe manne, mawili bega la kulia na mawili bega la kushoto, msimulizi anatueleza kwamba mlio wa kengere hizi ulikuwa unasikika maeneo ya mto Rutale kama mlio wa ndge au wadudu ambapo wachota maji wengi wanaokwenda rutale walikuwa wakiusikia, ndipo wauza maji wakabuni kengere mfano wa mlio huo wa 'ngere, ngere, 'ngere, ngere, kwa hiyo wanunua maji mitaani wakisikia mlio huo akili hugota kwamba maji ya rutale yanapita.

View attachment 2364093

Kutokana na uhaba wa maji mjini Kigoma miaka hiyo ya 1990 hupelekea watu kuwa wengi kuchota maji ya rutale kwa ajili ya matumizi, inasemekana watu wakiwa wengi jambo ambalo hupelekea kelele na fujo kuwa kubwa basi maji hugeuka na kuwa mekundu mfano wa damu, msimulizi anaeleza kwamba nyakati za jioni majira ya saa kumi na mbili kulikuwa na kiumbe kikiuonekana eneo hilo na ghafla hupotea na watu hutawanyika kwa kukimbia.

View attachment 2364095

Inasemekana pia kulikuwa na mpango kabambe wa kuyadhibiti maji ya rutale, ambapo wadhamini walijenga mabomba na kuweka mifereji ili maji yatoke kwa utaratibu maalum na waweze kufanya biashara ya kuwauzia watu maji hayo, hali hii ilipelekea maji hayo kutoka yakiwa yameambatana na nyoka wengi wadogo wadogo, na baada ya nyakati maji yaligeuka rangi na kuwa mekundu, kwa hiyo zoezi la kuyadhibiti maji kwa ajili ya biashara lilisimama na watu wakaendelea kuchota maji bure kama kawaida.

View attachment 2364102

Huu ndio mto rutale wenye maajabu yakusisimua, sehemu ya kutolea maji nyakati zingine maji yalikuwa yakiambatana na samaki wadowadogo wazuri sana wenye rangi za kumeremeta na wanaovutia kwa macho mfano wa samaki wa mapambo, ilikuwa hairuhusiwa kuwagusa au kuwakamata samaki hao kutokana na imani za wazee kipindi hicho, samaki hawa wazuri wenye mvuto wa kila aina ya rangi walikuwa wakiporomoka kuelekea ziwa Tanganyika na baadae hupotea.

View attachment 2364106

Maji haya kwasasa yamepimwa na wataalam na pia yamethibitika kuwa yanafaa kwa afya ya binaadamu, ispokuwa sharti la kuchota maji hapa hutakiwi kugombania maji au kuleta fujo kwenye eneo hili, kwani kufanya hivyo huaminisha kutokea kwa matukio ya mauzauza. Eneo hili kwasasa linamabomba makubwa yasiyo na koki na maji humwagika masaa 24 kwa kasi ile ile, maji huchotwa kwenye mabomba, na yale maji yanayomwagika yanakwenda moja kwa moja ziwani Tanganyika.

View attachment 2364110

Inasemekana idara ya maji ilileta wadhamini kuja kufunga mitambo kama mradi wa maji, kitendo cha kufanya hivyo maji ndio yalianza kubadilika nakuwa mekundu kama damu ikabidi wataalam watoe mitambo yao na kukabaki mabomba makubwa ndio hayo yapo yanamwaga maji saa 24 miaka nenda rudi. Huu ndio mto rutale, hairuhusiwi kuingia na viatu, na pia maji yake hutakatisha nguo yoyote ile chafu na kuing'arisha upya.

Kwasasa Rutale haina budi kupewa hadhi ya kuwa kama sehemu ya kivutio kwa watalii wanaofika Kigoma.
Hilo ni eneo la water spring.
Mahali pa maji maji, kuwaona chatu ni kawaida kabisa, hizo nyingine ni sory za vijiweni Kigoma.
 
Jina Rutale inasemekana lilitokana na mkazi mmoja aliekuwa akiishi mahala hapo miaka mingi iliyopita, watu walikuwa wakija kuchota maji kwenye chemchem hii walikuwa wakisema tunakwenda kuchota maji kwa Rutale.
Rutale maana yake ni "mwamba" A.K.A jiwe kubwa
 
Hilo ni eneo la water spring.
Mahali pa maji maji, kuwaona chatu ni kawaida kabisa, hizo nyingine ni sory za vijiweni Kigoma.
nimeishi bimala na nyumbani kwetu tulikuwa tunakaa jirani na sheli hyo bara bara ukishuka nayo moja kwa moja unafika mpaka rutale na hayo aliyoyasema yote ni ukweli mtupu tumeyashudia katika udogo wetu.

tena nmejikuta nmekumbuka mbali alipozungumzia kuhusu mzega mzega,mtu mwenye kubeba dumu nne kwenye fimbo mbili katika mabega yake akiwa na singlend huku akiwa amevaa kaptula yake na miguu yote miwili akiwa amevaa kengele nakumbuka kipindi hicho unamlipa 100 kwa kila dumu wakati huo anatoa maji rutale mpaka bimala umbali wa around 3km

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
nimeishi bimala na nyumbani kwetu tulikuwa tunakaa jirani na sheli hyo bara bara ukishuka nayo moja kwa moja unafika mpaka rutale na hayo aliyoyasema yote ni ukweli mtupu tumeyashudia katika udogo wetu.

tena nmejikuta nmekumbuka mbali alipozungumzia kuhusu mzega mzega,mtu mwenye kubeba dumu nne kwenye fimbo mbili katika mabega yake akiwa na singlend huku akiwa amevaa kaptula yake na miguu yote miwili akiwa amevaa kengele nakumbuka kipindi hicho unamlipa 100 kwa kila dumu wakati huo anatoa maji rutale mpaka bimala umbali wa around 3km

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Karibu sana
 
Back
Top Bottom