Maajabu ya neno pepsi

Maajabu ya neno pepsi

John mungo

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2013
Posts
1,008
Reaction score
1,028
Pepsi ni jina la kinywaji aina ya soda ila uki tulia kwa makini na ukalifanyia utafiti wa jina hilo linatisha vibaya.
Nilicho gundua mimi katika pepsi ni maneno tofauti na awali.

siku moja nili kuwa nakunywa soda aina ya pepsi huku nina mawazo tele kichwani nikaanza kuigeuza chupa chini juu na kusoma nika pata maana, nikaigeuza wima na kusoma kiarabu na yenyewe ipo maana.nika soma kwa namba ipo maana zaidi ya moja.
CHEKI hapo chini.

Pepsi =is ded

pepsi= is 666

pepsi=12969

jamani pepsi ni hatari kwa afya zetu.

mfano chukua mfupa wa kuku ingiza kwenye pepsi wacha masaa 24, kisha rudi kautazame kama uta ukuta.Au tia msumari ktk pepsi acha saa 24 halafu kaangalie katika chupa kama uto kuta kutu.
Jamani ni kifo hicho kwenye soda
pepsi=is pep
 
wewe umeamuwa kuirudia Thread ya Madhara yavinywaji Baridi Soda za aina yoyote ile ni mbaya mimi nimesha weka Madhara ya kunywa Soda ya aina yoyote ile sio Pepsi tu soma bonyeza hapa https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/210672-madhara-ya-kunywa-soda.html

Madhara ya kunywa soda

KUNA mjadala mkali unaendelea kuhusu vinywaji baridi hususani soda, baada ya utafiti wa hivi karibuni kuonyesha kuwa soda inaweza kuwa na madhara zaidi kiafya kuliko hata sigara!

Hii inaweza kuwa changamoto nyingine kubwa kumkabili binadamu katika masuala ya afya, kwani makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji baridi yanatumia mabilioni ya dola kila mwaka kujitangaza na kutoa misaada ya kijamii kutokana na mauzo yake bila kutaja madhara ya vinywaji vyao.

Soda inahusishwa na matatizo mengi ya kiafya kwa watoto na watu wazima, yakiwemo matatizo ya kuongezeka unene kupita kiasi (obesity), ugonjwa wa ini (liver disease) na hata tabia za vurugu (violent behavior). Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni, unywaji wa vinywaji baridi mara kwa mara unachangia tabia ya ugomvi kwa asilimia kati 9-15!

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa nchini Marekani, soda huwekwa ‘fructose' (sukari) nyingi ikiwa katika mfumo wa sirapu (fructose corn syrup) ambayo inaongoza kwa kusababisha magonjwa ya unene, kisukari, ugonjwa wa moyo na magonjwa mengine sugu yanayowakabili Wamarekani wengi hivi sasa na dunia kwa ujumla.

Dk. Mercola, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya lishe asilia na tiba mbadala anasema: " Ninaposema kunywa soda ni hatari sawa na mtu anayevuta sigara au pengine zaidi, siyo jambo la kutia chumvi, bali ndiyo ukweli halisi".

Dk. anaendelea kusema kuwa unywaji wa soda kwa njia nyingi ni mbaya kuliko uvutaji wa sigara, ila kutokana na kampeni kubwa ya matangazo inayofanywa na makampuni haya, inafanya vinywaji hivi vyenye sukari kuonekana havina madhara kwa watu wasio na hatia, hasa watoto wetu!

SABABU KUBWA YA KUDHARAU SODA
Unayesoma makala haya kuhusu madhara ya soda kwa mara ya kwanza bila shaka utakuwa unashangaa na kujiuliza; soda ina ubaya gani? Kwa mujibu wa Dk. Mercola, hakuna sababu yoyote ya kuendelea kunywa soda, labda ujikute uko katikati ya jangwa na hakuna kinywaji kingine isipokua soda!

Kiafya, unywaji wa soda au vinywaji vingine baridi vyenye ‘fructose' una madhara. Unywaji wa kiasi cha kopo moja tu la soda kila siku, utakuongezea uzito wa mwili wa kilo 10 kila mwaka na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari (diabetes) kwa asilimia 85!

‘FRUCTOSE'
‘Fructose' ni kirutubisho kilichomo ndani ya sukari na kiwango kinachowekwa wakati wa utengenezaji wa soda ni kingi kuliko kawaida. Inaelezwa kuwa miaka 100 iliyopita, Mmarekani mmoja alikuwa akitumia kiasi cha gramu 15 ya sukari (fructose) kwa siku, tena kwa kula matunda. Miaka 100 baadaye, (yaani hivi sasa), robo ya Wamarekani wote wanatumia kiasi cha gramu 135 (kutoka 15) kwa siku, tena kwa kunywa soda!

Ulaji wa sukari (fructose) kiasi cha gramu 15 kwa siku hauna madhara kiafya, labda uwe na ugonjwa wa kisukari (high uric acid levels). Hata hivyo, kwa kula sukari mara kumi zaidi ya kiwango cha gramu 15 kinachokubalika kiafya, inakuwa ndiyo chanzo cha unene wa kupindukia na magonjwa mengine hatari yanayoibuka mwilini (degenerative diseases).

Utafiti unaonesha kuwa vinywaji vingi baridi vina sukari nyingi kuliko wastani unaotakiwa. Badala ya kuwa na asilimia 55 ya ‘fructose' na asilimia 45 ya ‘glucose', vingi vina asilimia 65 ya ‘fructose', ikiwa ni karibu asilimia 20 zaidi na inavyotakiwa.

Utafiti zaidi umeonesha kuwa ‘fructose' ndiyo chanzo kikubwa cha tatizo la ugonjwa wa ini kwa watoto wengi nchini Marekani, ingawa hawatumii kilevi chochote (alcohol). Inaelezwa kuwa ‘fructose' huleta madhara kwenye ini kama inavyofanya pombe.
 
Mie nimekueleza jina la pepsi na maana zake.usikurupuke soma vichwa vya habari.
Nitakuja kuku unga mkono huko kwako kwenye mada yako.
 
pepsi hivi kweli ukiligeuza hili neno unapata is ded kweli?????

dog= ukigeuza utapata ??? kweli god

Nakataa hii mifano kwa nini tugeuze maneno ?
 
Mimi sitaacha hadi nife, my Dear Dad hadi anakufa last minutes aliomba CocaCola na alikua na kisukari kibaya!!!! Mara tusile kitimoto mara mafua ya kuku
 
Pepsi ni jina la kinywaji aina ya soda ila uki tulia kwa makini na ukalifanyia utafiti wa jina hilo linatisha vibaya.
Nilicho gundua mimi katika pepsi ni maneno tofauti na awali.

siku moja nili kuwa nakunywa soda aina ya pepsi huku nina mawazo tele kichwani nikaanza kuigeuza chupa chini juu na kusoma nika pata maana, nikaigeuza wima na kusoma kiarabu na yenyewe ipo maana.nika soma kwa namba ipo maana zaidi ya moja.
CHEKI hapo chini.

Pepsi =is ded

pepsi= is 666

pepsi=12969

jamani pepsi ni hatari kwa afya zetu.

mfano chukua mfupa wa kuku ingiza kwenye pepsi wacha masaa 24, kisha rudi kautazame kama uta ukuta.Au tia msumari ktk pepsi acha saa 24 halafu kaangalie katika chupa kama uto kuta kutu.
Jamani ni kifo hicho kwenye soda
pepsi=is pep

We huna IQ iyo.
Umepesti tu humu.

Afu hiyo ni akili ya div 5, hujui mdomoni mpaka tumboni kuna enzymes?
Basi ka ni ivo basi hata kukanyaga ardhi mbichi kwa muda mrefu ni sumu kwani msumari huwa unapata kutu.
 
ukifatisha sana habari toka kwa watu wanao exaggerate issue za ki-freemason,hata K ya mkeo utashindwa kuihudumia vizuri kitandani.kisa kwa mahesebu ya ki-freemason cjui bla bla bla K ilitokana na namba 666.mwee!......nitakunywa pepsi na coca cola mpaka nitakapo aga dunia.ukweli ni kwamba hakuna chakula/kinwaji kilicho tengenezwa kwa mchanganyiko wa kimaabara/kiwandani kikakosa madhara kwa binaadam.period.
 
Kwani "DED" maana yake nini tofauti na kifupi cha DISTRICT EXECUTIVE DIRECTOR (Mkurugenzi wa wilaya), unamaana kuwa pepsi ni kwaajili ya wakurugenzi wa wilaya tu au?

Kuhusu kutu ni chemistry ndogo sana tu inahitajika! Uwepo wa chuma(Iron)+ Oxygen+Maji=rust(kutu) sasa kutokea kwa kutu wala kusikupe tabu. Kuhusu hizo namba ulizoziweka labda unifahamishe zaidi zina athari gani kiafya.
 
Mkuu hiyo ni chemistry ya form two kila mtu anafahamu, nilichotaka ni kumpa mwanga huyo jamaa wa cocacola aache ukilaza.
Make huwa tunaona hata masufuria nyumbani yanapata kutu au zile iron wool za kusafishia bila kuweka udongoni.
 
Pamoja sana mkuu. Na mimi pia nipo upande wako kumshangaa huyu mleta hoja.
 
Mimi sitaacha hadi nife, my Dear Dad hadi anakufa last minutes aliomba CocaCola na alikua na kisukari kibaya!!!! Mara tusile kitimoto mara mafua ya kuku

du kifo cha mjerumani
 
So ili iweje uishi milele!? Hujui hata bati lifunikalo nyumba yako lina madhara?! Tv uitazamayo, PC, simu uitumiayo pia na taa mwenyewe waziita energy saver...hata marafiki wako ni hatari kwa afya yako so waishi ktk ukimwengu wenye mashaka telee! ""shika sana ulicho nacho, usiruhusu mtu au kitu kikulubuni""
 
Naomba uendelee na kautafiti kako tugeuzie na cocacola tupate maana zolizojificha
 
Naomba uendelee na kautafiti kako tugeuzie na cocacola tupate maana zolizojificha

Haha nineipenda hiyoo ila niliwahi kutana na picha ya abstract ktk maandishi ya cocacola pana watu wawili wanavuta unga hapo ktk hayo maandiashi...najua nitadaiwa picha...na wadau...narudi nayo.
 
geuza na cocacola yalke maandishi ya mcharazo utapata tafsiri ya kutisha sana
 
Kwani had ugeuze jaman mbona hizi ni myth mnaleta humu ndani kwa utafiti wangu usio rasmi kila kinachogeuzwa kinakua na madhara tukianzia 0713, nk
 
wewe sijui ni wa wapi chemistry ya soda zote hihi hapa mzee .... kuna carbonated water,sodium benzoate, ascorbic acid, sugar pia kuna chemicals for its colour,, lemon .. flavour chemicals .... hivyo vyote vina side effects na kila kitu unachotumia kina side effects iwe computer, simu, gari, vyakula madawa hadi nguo unazovaa so usilete habari za kugeuza maneno hapa hivy vyote nilivyokutajia ni organic compounds zimo kwenye mitishamba unayotumia wacha watu wanye soda, bia na kadhalika
Pepsi ni jina la kinywaji aina ya soda ila uki tulia kwa makini na ukalifanyia utafiti wa jina hilo linatisha vibaya.
Nilicho gundua mimi katika pepsi ni maneno tofauti na awali.

siku moja nili kuwa nakunywa soda aina ya pepsi huku nina mawazo tele kichwani nikaanza kuigeuza chupa chini juu na kusoma nika pata maana, nikaigeuza wima na kusoma kiarabu na yenyewe ipo maana.nika soma kwa namba ipo maana zaidi ya moja.
CHEKI hapo chini.

Pepsi =is ded

pepsi= is 666

pepsi=12969

jamani pepsi ni hatari kwa afya zetu.

mfano chukua mfupa wa kuku ingiza kwenye pepsi wacha masaa 24, kisha rudi kautazame kama uta ukuta.Au tia msumari ktk pepsi acha saa 24 halafu kaangalie katika chupa kama uto kuta kutu.
Jamani ni kifo hicho kwenye soda
pepsi=is pep
 
Mimi sitaacha hadi nife, my Dear Dad hadi anakufa last minutes aliomba CocaCola na alikua na kisukari kibaya!!!! Mara tusile kitimoto mara mafua ya kuku

Na ukitaka usipone kisukari basi endelea kunywa soda.
 
Back
Top Bottom