Maajabu ya Upinzani Tanzania: CHADEMA wanashangilia ACT kuibiwa kura na CCM

Cdm hutoa maamuzi Yake kupitia vikao, ni wapi wamekaa na kutoa taarifa ya kufurahia huo uhayawani wa kwenye uchaguzi? Huwezi kutofautisha chama na maoni ya mtu?
Viongozi waandamizi na wanachama wake wakiwa wanashangilia mtandaoni na wala hawajakemewa nafikiri tunaweza kusema ni chama
 
Viongozi waandamizi na wanachama wake wakiwa wanashangilia mtandaoni na wala hawajakemewa nafikiri tunaweza kusema ni chama
Huna ujualo boss, taarifa za chama huletwa na msemaji wa chama. Wanachama na mashabiki huongea maoni Yao.
 
Ukweli wananchi bado hawana imani na wapinzani kwa hivyo siasa wao wanaona bora wapitie ccm tu. Yaani bora jini ulijualo. Pia wana matumaini makubwa atapatikana kiongozi mngine kama magufulu.
Kwa upande wa wapinzani hasa chadema wanafikiri demokrasia ni lazima wananchi wachague upinzani. Badala ya kutafuta sababu kwa nini hawachaguliwi wanakimbilia kusema ccm au serikali inawaibia kura. Hii sababu hua inawafurahisha mabeberu wa nchi za kibepari ambao kwa historia ya ccm kwamba wakati mmoja kilifuata ujamaa ule wa dola kuendesha yenyewe shughuli kuu za uchumi hawawezi kukisamehe. Wangetaka sana ccm iondoke madarakani. Pia wana kisassi na ccm kwa kuunga mkono ukombozi wa kusini mwa afrika na kuvuruga mirija yao ya kikoloni.
 
Mzee hivi tunaosema CCM wamefanya jambo fulani, kwani huwa wanakuwa wametoa taarifa rasmi kuwa wamefanya?
Kwahiyo mzee Sabaya aliposema wakichaguliwa wapinzani serekali haitapeleka maendeleo,ni maagizo ya ccm kwakuwa chama chake hakijamkea hadharani?
 
Kwahiyo mzee Sabaya aliposema wakichaguliwa wapinzani serekali haitapeleka maendeleo,ni maagizo ya ccm kwakuwa chama chake hakijamkea hadharani?
Unaweza kusema hivyo
 
Wanashangilia au kueleza hali halisi? Bila kubadilisha mifumo haya mambo hayataisha

Watu wa ajabu sana yaani wanalaumu Chadema kwa CCM kuiba kura. Kwanini hauongelei kura kuibiwa wewe unaona hiyo ni sawa ! Badala yake unaongelea watu wanaocheka wakati demokrasia inadidimizwa halafu unajifanya eti mzalendo 😂
 
ACT kwa Chadema ni sawa na Tembo vs Kiroboto, hebu waandamane tuone.
 
Jitahidi sana kwenye jamii usiitwe mchawi ukishaitwa mchawi na majirani zako hilo jinamizi halitoki ng'ooo. Kwahiyo hata ufanyeje ACT hasafishiki, ni msaliti na ataendelea kuwa msaliti mpaka kufa kwake.
 
Hao wazee wa SUK wako kimaslahi na vigeugeu geu wanauma nakupuliza Acha yawakute wako kimkakati kufubaza upinzani
 
Jitahidi sana kwenye jamii usiitwe mchawi ukishaitwa mchawi na majirani zako hilo jinamizi halitoki ng'ooo. Kwahiyo hata ufanyeje ACT hasafishiki, ni msaliti na ataendelea kuwa msaliti mpaka kufa kwake.

hasafishiki kutoka kwa nani? hivyi nyinyi munahisi Tanzania nzima ni CHADEMA ama?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…