Maajabu ya Upinzani Tanzania: CHADEMA wanashangilia ACT kuibiwa kura na CCM

ACT kuibiwa kura ndio kitu ambacho kilitakiwa kujadiliwa kwa nguvu na CDM na kuiuliza CCM maswali kuwa walikuwa wanamsingizia Magufuli huku wao wanafanya hayo hayo, Cha ajabu Chadema wanaipongeza CCM na kuicheka ACT
 
Chadema ni genge la wasakatonge kupitia siasa!
Kwao siasa ni kama biashara na wanapoona chama kingine kikiibuka na kuelekea kupata ushawishi mkubwa kwa wananchi.
Chadema wanaona kama wanaporwa biashara yao.

Pale Chadema mtu pekee ninayemuona akiwa na kariba halisi ya uanasiasa ni huyo J.J.Mnyika.
Hawa wengine kina Lema & the Company ni walanguzi wa kisiasa.

Sema Tanzania hatujapata upinzani wa kweli wa kisiasa.

Fikiria Chadema ilichowafanyia kina Advocate Mwabukusi pale walipoona wanaenda kuwapiku ushawishi kwa watanzania!
 
Unajiuliza maswali ya kijinga mura! CHADEMA walichokuwa wanataka ni kuwa na nguvu ya pamoja kati ya vyama vya upinzani! Ka hawara ka CCM kakaona kawakomoe CHADEMA kakasema mazingira yako sawa! Sasa yako wapo? Lema yuko sahihi kukazomea ka ACT! In short Zitto ameleta siasa za kipumbavu! CCM nayo kama hayana akili, hayajui kula na vipofu, kwenye hizi uchaguzi ndogo yangekuwa yanasimamia haki ili kuwakata kilimilimi wapinzani. Hapo yangekuwa yanapata points za kuongelea.
 
Chadema mbona nao wanashiriki uchaguzi katika mazingira haya haya?
Kipindi cha Magufuli si walikuwa wakisusia uchaguzi ndogo lakini wakaja kushiriki uchaguzi mkuu na mazingira yakiwa hayajabadilika?

Mwaka huu si wamesema watashiriki uchaguzi wa serikali za mitaa?
Mwakani si wamesema pia watashiriki uchaguzi mkuu ?
So Chadema wakishiriki ni sawa ila ACT ikishiriki ni nongwa?
 
Kwahio tuendelee kushiriki hali ya kua tunajua atushindi
Kisa ukimsusia nyani mahindi atakula yote
Na usipo msusia kinatokea nini
 
Kwahio tuendelee kushiriki hali ya kua tunajua atushindi
Kisa ukimsusia nyani mahindi atakula yote
Na usipo msusia kinatokea nini
Mafanikio yanakuja kwa jitihada na mapambano, siyo kususa.

Kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 walijaribu kufanya hivyo, kulikuwa na impact gani?!
 
Huoni kuwa wewe ndiye una matatizo,

Badala ya kuwashangaa CCM waiba kura, unashangaa mashuhuda wa WIZI wa kura.

Una tatizo kubwa,

Jitafakari.
 
ACT ni CCM hao hao. Ngedere na Nyani wameibiana mahindi hapo kesi anapewa tumbiri aamue.
 
Sawa na hata ukishiriki kutakuwa na impact gani
Hujui kwamba baadhi ya wagombea huwa wanashinda hadi waĺishaongoza Halmashauri kadhaa?

Ule wa jiwe haukuwa wizi tu, ulikuwa ni unyang'anyi wa mchana kweupe, kwa hiyo haufai kutumiwa kama kigezo
 
Huoni kuwa wewe ndiye una matatizo,

Badala ya kuwashangaa CCM waiba kura, unashangaa mashuhuda wa WIZI wa kura.

Una tatizo kubwa,

Jitafakari.
Kuna mtu alikuwa mwizi wa kura kuliko mwendazake?
 
ACT kuibiwa kura ndio kitu ambacho kilitakiwa kujadiliwa kwa nguvu na CDM na kuiuliza CCM maswali kuwa walikuwa wanamsingizia Magufuli huku wao wanafanya hayo hayo, Cha ajabu Chadema wanaipongeza CCM na kuicheka ACT
Ni chuki tu za kisiasa tu zinawasumbua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…