Jana nimemuona Maalim Seif akichukukua fomu ya kugombea uraisi huko Zanzibar kupitia ACT,amedai amefanya hivyo baada ya kuona hakuna mtu mwingine aliyejitokeza kutoka upande wa chama chake cha ACT kuchukua fomu ya kuwania uraisi wa Zanzibar,huo ni uongo na uzandiki kwa mtu ambaye anataka kuwa raisi,tunajua fomu iliyochapwa ni moja tu.Seif anatakiwa apumzike,nimemuona hata kuweka saini yake kwenye hizo fomu umekuwa mtihani kwake,
umri umeshapita kwa Maalim angewapa fursa watu wengine,tumeanzia kumsikia Maalim kuanzia enzi za akina mzee Shabaan Mloo,James Mapalala na wengineo wengi ambao ama wametangulia mbele za haki ama wanalea vitukuu,huu ni udikteta uchwara kwa Maalim Seif,na kama vyeo serikalini kavishika sana, Maalim kawa mzee hambiliki yeye ni kuota tu ule mjengo wa Vuga kila kukicha. Ushauri wa bwelele ni kuwa Maalim kwa sasa pumzika siasa za vijana zimeshakupita, kwa kifupi Uraisi wa Zaanzibar utausikia tu.