Zanzibar 2020 Maalim Seif achukua Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar kupitia ACT Wazalendo

Zanzibar 2020 Maalim Seif achukua Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar kupitia ACT Wazalendo

20 Jun 2020
MAALIM : 'TUTAPAMBANA, SAFARI HII HATUNYANG’ANYWI NG’OO KAMA NOMA NA IWE NOMA'


Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif amesema kuelekea uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka huu wamejipanga kuhakikisha wanashinda na sio kushiriki. ''Sisi sio chama sindikiza ni chama ambacho tunataka ushindi''

Source : Muungwana TV
 
Ngoja tuone!!!ccm watamuandaa jecha mwingine!!!Benki ya Dunia kukubali uchumi wetu wa kati sio Bure!!labda makubaliano ya ACT KUSHIKA HATAMU ZANZIBAR!!!
 
5 July 2020
Vuga, Unguja
Zanzibar

Shuhudia Shangwe, Hoihoi na Nderemo za Kumlaki Maalim Seif Zikirindima Kweupe Bila Uficho Wakati wa Kuchukua Fomu



Hakika Hii ni fahari yetu kuona mgombea mwenye mapenzi mema na nchi ya Zanzibar akiwasili kuchukua fomu ili ashiriki ktk uchaguzi kuwaomba ridhaa wananchi wampe uRais wa Zanzibar 2020 kupitia chama cha ACT-WAZALENDO.

Source: KTV TZ online
 
Jana nimemuona Maalim Seif akichukukua fomu ya kugombea uraisi huko Zanzibar kupitia ACT,amedai amefanya hivyo baada ya kuona hakuna mtu mwingine aliyejitokeza kutoka upande wa chama chake cha ACT kuchukua fomu ya kuwania uraisi wa Zanzibar,huo ni uongo na uzandiki kwa mtu ambaye anataka kuwa raisi,tunajua fomu iliyochapwa ni moja tu.Seif anatakiwa apumzike,nimemuona hata kuweka saini yake kwenye hizo fomu umekuwa mtihani kwake,

umri umeshapita kwa Maalim angewapa fursa watu wengine,tumeanzia kumsikia Maalim kuanzia enzi za akina mzee Shabaan Mloo,James Mapalala na wengineo wengi ambao ama wametangulia mbele za haki ama wanalea vitukuu,huu ni udikteta uchwara kwa Maalim Seif,na kama vyeo serikalini kavishika sana, Maalim kawa mzee hambiliki yeye ni kuota tu ule mjengo wa Vuga kila kukicha. Ushauri wa bwelele ni kuwa Maalim kwa sasa pumzika siasa za vijana zimeshakupita, kwa kifupi Uraisi wa Zaanzibar utausikia tu.
 
Maalim ukimcheki anaonekana kabisa umri na afya vimemtupa mkono.hapa napata picha ya tamaa ya madaraka iliyomjaa huyu babu.
 
Safarai hii ni kuandika historia katika dunia na Tanzania.Na kwa upande wa Mafuli atakuwa ameandika historia nyengine baada ya ile kuhamia Dodoma,kushinda hofu ya corona.Sasa itakuwa ni raisi wa mwanzo wa chama tawala CCM kufanya kazi na chama cha upinzani.Kila mmoja atafurahi na nchi kuingia baraka na kupanda daraja la uchumi kuwa taifa tajiri zaidi Afrika.
 
Jana nimemuona Maalim Seif akichukukua fomu ya kugombea uraisi huko Zanzibar kupitia ACT,amedai amefanya hivyo baada ya kuona hakuna mtu mwingine aliyejitokeza kutoka upande wa chama chake cha ACT kuchukua fomu ya kuwania uraisi wa Zanzibar,huo ni uongo na uzandiki kwa mtu ambaye anataka kuwa raisi,tunajua fomu iliyochapwa ni moja tu.Seif anatakiwa apumzike...
Maalim ndo mpinzani pekee mwenye ushawishi wa kutosha Zanzibar...ili kumpata mtu kama Maalim Znz inabidi ama huyu mzee afariki au ajiuzulu siasa abaki kuwa mshauri tu...ila kwa sasa hakuna jinsi inabdii awe yeye tu kwa sababu ushawishi wake kwa kundi kubwa la wazenji haumithiliki..na pengine ACT wameona kwa Zanzibar ili watie hamsha hamsha ya kweli lazima wamsimamishe huyu jembe.
 
Hatoshinda yeye agombee ubunge wa Prmba mjini atashinda yeye yupo kama Raila Odinga ,
Nyota yake sio ya uraisi nyota yake ni ya ubungee.
 
Back
Top Bottom