NI KIONGOZI WA CHAMA SI KIONGOZI MKUU WA CHAMA!
Kama ilivyo kwa vyama vingine duniani vinavyofuata mfumo huu, Kiongozi wa Juu huitwa Kiongozi wa Chama (Party Leader) na si Kiongozi Mkuu Wa Chama (Supreme Party Leader) Kama ambavyo baadhi ya watu huita kimakosa. Dhana “Mkuu(Supreme)” huambatana na utukufu/kutopingika. Hakuna sehemu yoyote Kwenye Katiba ya ACT Wazalendo ambako kuna rejea ya ‘Kiongozi Mkuu’.
Tuhitimishe Mjadala wetu kwa kuona nafasi ya Kiongozi wa Chama ndani ya ACT Wazalendo;
Kiongozi wa Chama atakuwa ndiye Msemaji Wa Kisera. Katika kutekeleza wajibu huu, Kiongozi wa Chama atawajibika kutoa mwongozo na mwangaza kuhusu maeneo mbalimbali ya kisera. Baada ya mwongozo wake kusemwa, ni wajibu wa Wenyeviti Wa Kamati (Wasemaji Wa Kisekta) na Msemaji Wa Chama (Msemaji Wa Jumla) kuendeleza na kueneza kwa umma.
Mkuu Wa siasa. Katika kutekeleza wajibu huu, Kiongozi wa Chama anapaswa kuwa kielelezo cha kuimarisha taswira ya Chama na kukiuza ndani na nje ya Bunge na kwenye Jamii kwa ujumla
Kiongozi wa Chama hataongoza vikao vya Chama, isipokuwa Mkutano Mkuu Wa Kidemokrasia. Vikao vya Maamuzi Kama vile Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu vitaongozwa na Mwenyekiti. Wajibu wa kusimamia utekelezaji Wa maamuzi ya vikao vya Chama pia upo kwa Mwenyekiti.
Na ufahamu tu kiongozi wa chama huchaguliwa kwa kura.