Uchaguzi 2020 Maalim Seif: ACT Wazalendo hatuna mpasuko lakini Membe anataka kuwaaminisha Watanzania hivyo. Adai Mzee wa Ubwabwa ni bora kuliko Mgombea wao

Nilimsikiliza vizuri Bernard Membe kwenye mkutano wake na waandishi wa habari juzi. Alizungumza kwa weledi sana akikwepa mipaka ya kisheria na kutoa staha kwa makubaliano yasio rasmi ya viongozi wa ACT na CHADEMA ya kumuunga mkono mgombea mmoja anayekubalika kwa nafasi za Urais wa JMT na ile ya SMZ.

Msikilize vizuri na umsome between the lines, anachosema ni kwamba CCM haiko shwari ndani. Na hii ni kwa advantage ya upinzani kwa maana kuna waliopo ndani ya CCM wanaunga mkono upinzani. Kwa akili aliyonayo anaelewa kabisa yeye hakubaliki kwa maana hiyo anazungumza kuutia nguvu upinzani hasa Lisu kwamba ana support kubwa hata ndani ya Chama Tawala. Isingewezekana yeye kutamka kujitoa au kuunga mkono Lisu sababu ingeweza kua na consequences kwa kina Lisu na hata Maalim mwenyewe kama kiongozi wa chama na mgombea wa Urais SMZ.

Kauli ya Maalim Seif kumzodoa Membe kwamba anakivuruga chama inaweza ikam provoke Membe naye akatamka anamuunga mkono mgombea mwingine na rungu likakishukia ACT! Ni vyema viongozi wa upinzani wakajenga nidhamu kama ya CCM kuitana kwenye vikao vya ndani na kumaliza tofauti zao huko na kamwe si kulaumiana kwenye vyombo vya habari na majukwaani.
 
MGOMBEA urais wa chama cha ACT Wazalendo visiwani Zanzibar ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, ameeleza kusikitishwa kwake na tamko la jana la mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho, Bernard Membe, kuwa yeye ni mgombea halali wa urais, hivyo ataipeperusha bendera ya chama na ana uhakika atashinda.

Akizungumza na wanahabari leo Jumanne, Oktoba 20, 2020, jijini Dar es Salaam, amesema ACT-Wazalendo kupitia mkutano mkuu wa taifa walisema wanataka mabadiliko nchini ambapo mkutano huo ulibariki kushirikiana na vyama vingine vya upinzani ili kuiondoa CCM madarakani.

“Membe alipokuja tulimwambia uamuzi wa mkutano mkuu ni tushirikiane na vyama vingine. Tukamuuliza tukiamua kushirikiana utakubali? Akasema ‘Naam.’ Tulipoona kampeni zetu zimesuasua, tukaamua, na Membe akiwepo, tumuunge mkono Tundu Lissu.

“Mgombea wetu (Bernard Membe) haonekani. Ni afadhali mzee wa ubwabwa (Hashim Rungwe) anaonekana. Kamati ya uongozi kwa kauli moja pamoja na Membe tulikubaliana tumuunge mkono Tundu Lissu. Siyo kwamba hatumpendi Membe.

“Alilosema Zitto Kabwe si lake! Nililosema mimi Maalim Seif si langu! Bali ni maamuzi ya chama. Ni msimamo wa ACT Wazalendo anayekaribia kumshinda Magufuli ni Tundu Lissu na huyo ndiye tunamsapoti. Mimi nam-challenge, afanye hizo kampeni zake tuone hizo kampeni ziko wapi. Nia yake ni kutaka kuwachanganya Watanzania.

”Zimebaki siku saba kwa wananchi kufanya maamuzi ya kuwachagua viongozi wanaowataka wao. Tunaelekea katika uchaguzi mkuu wakati wagombea wetu kadhaa wameenguliwa katika kinyang’anyiro hicho lakini tukafanye maamuzi.

“Nyakati zote mimi nilikuwa nawazuia watu wasiingie barabarani! Sasa mwaka huu simzuii mtu. Yeyote atakayeamua kufanya lolote afanye hiyo tarehe 27 na 28. Wazanzibar wamepanga kulinda demokrasia kwa gharama yoyote! Wamevuta subira kwa muda mrefu. Sasa imetosha!” amesema Maalim.

 
Kwani kumvua uanachama membe haiwezekani kwa Sasa??
 
Shekhe Ponda Issa Ponda amewataka Viongozi wa ActWazalendo watulie kidogo ili Magufuli arudishwe kwao Burundi
 
Mashabiki wa chadema watakwambia Membe ni jasusi mbobevu na huu ukimya wake ni strategy ya kuwachanganya NEC.
[emoji23][emoji23][emoji23]
Walimsifia sana ila kwa sasa hawana hamu nae na wanajuta kwa sifa walizokua wanampatia na majina ya kijemedari.
 
Kama majasusi tulionao wote ni kariba ya Membe basi nchi iko matatizoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…