Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,559
- 19,101
Nilimsikiliza vizuri Bernard Membe kwenye mkutano wake na waandishi wa habari juzi. Alizungumza kwa weledi sana akikwepa mipaka ya kisheria na kutoa staha kwa makubaliano yasio rasmi ya viongozi wa ACT na CHADEMA ya kumuunga mkono mgombea mmoja anayekubalika kwa nafasi za Urais wa JMT na ile ya SMZ.
Msikilize vizuri na umsome between the lines, anachosema ni kwamba CCM haiko shwari ndani. Na hii ni kwa advantage ya upinzani kwa maana kuna waliopo ndani ya CCM wanaunga mkono upinzani. Kwa akili aliyonayo anaelewa kabisa yeye hakubaliki kwa maana hiyo anazungumza kuutia nguvu upinzani hasa Lisu kwamba ana support kubwa hata ndani ya Chama Tawala. Isingewezekana yeye kutamka kujitoa au kuunga mkono Lisu sababu ingeweza kua na consequences kwa kina Lisu na hata Maalim mwenyewe kama kiongozi wa chama na mgombea wa Urais SMZ.
Kauli ya Maalim Seif kumzodoa Membe kwamba anakivuruga chama inaweza ikam provoke Membe naye akatamka anamuunga mkono mgombea mwingine na rungu likakishukia ACT! Ni vyema viongozi wa upinzani wakajenga nidhamu kama ya CCM kuitana kwenye vikao vya ndani na kumaliza tofauti zao huko na kamwe si kulaumiana kwenye vyombo vya habari na majukwaani.