Uchaguzi 2020 Maalim Seif: ACT Wazalendo hatuna mpasuko lakini Membe anataka kuwaaminisha Watanzania hivyo. Adai Mzee wa Ubwabwa ni bora kuliko Mgombea wao

Hapo naona Membe hataki awe wa mwisho, kuwa wa mwisho ni fedheha mjue.
 
Huyo Membe since day one nilijua ametumwa na CCM. Nilisema kabisa inyeshe mvua liwake jua, CHADEMA wasikosee wakajiunga na Membe na kufanya naye vikao vya siri. Hata Nyalandu ni wa kumuweka pembeni kwenye vikao vya siri vya CHADEMA. Haya ya Membe yanaanza kuwa wazi, uzuri ni kuwa wananchi wameshafanya maamuzi, vinginevyo ingekuwa tatizo hizi dakika za lala salama.
 
Mwenyekiti wa ACT Taifa anaongea na wanahabari jijini Dar es salam...
Maalif Seif huwa ninamuelewa sana , na Znz hawatakuja kupata mtu mvumilivu kama Mzee Seif. Mzee akisema amechoka kuibiwa kwa kweli amemaanisha na sasa mimi naona ni sawa kabisa aruhusu watu waingie road kuipambania demokrasia ambayo ccm wao wamekuwa wakiiminya kila iitwapo leo
 
Uwaneni,piganeni,chambaneni ila Magufuri anashinda kwa asilimia nyingi mnooo....

Ccm iliyumba wakati wa lowassa.
wapiga kura Og wako nje ya mitandao,vijijin ndo usiseme kura kama zote
Tunaopiga kelele ni huku mitandaoni kwa Id fake tena nyuma ya keybo'd .
 
Maalif Seif huwa ninamuelewa sana , na Znz hawatakuja kupata mtu mvumilivu kama Mzee Seif. Mzee akisema amechoka kuibiwa kwa kweli amemaanisha na sasa mimi naona ni sawa kabisa aruhusu watu waingie road kuipambania demokrasia ambayo ccm wao wamekuwa wakiiminya kila iitwapo leo
Seif miaka yote kabla ya kura husemaga hivyo!

Hata baada ya matokeo ya uchaguzi wa marudio Zanzibar, seif alizunguka zunguka huko ulaya akaja kutwambia baada ya miezi 3 atakabidhiwa nchi yake. Mpka leo miak 4 imeshapita tunaingia kwenye uchaguz mwingine Seif akiwa yule yule.
 
Bora CHADEMA Lowassa kawafundisha akili, Membe yaani anaharibu mipango.
 
Jasusi is there to stay

Uchaguzi ukimalizika anaukurupusha mgogoro kama wa NCCR ya Mrema na Mabere Marando 1995~2000

Siku nyingine Ccm ikigombana na wanachama wake wapinzani wapunguze shobo
Uzuri Membe ataondoka yeye na mke wake kwenda ADC ya Hamad Rashid
 
Sawa kabisa. Kazi kubwa ni hiyo.
Usije shangaa ACT wakamvua uanachama Membe then uchaguzi ukaahirishwa kwa muda ili kuchapisha karatasi za kupigia kura upande wa Urais.
Au ACT ikamruhusu Membe kuendelea ili azigawe kura za WanaCCM na kumwacha Lissu akitamba, kitu ambacho hakiwezekani.
 
Membe alishapewa hela za kampeni kwa alio waahidi kuwa atakuwa rais wa JMT. Ni lazima wamuone amefanya kampeni ili ku halalisha matumizi ya pesa hizo. Hata mwenyewe anajua kuwa hawezi kuwa Rais nje ya CCM.
 
Mwenyekiti wa Act taifa anaongea na wanahabari jijini dar es salam

--

Nimesikitika sana kwa aliyoyazungumza ndugu yangu Bernard Membe, ACT-Wazalendo kupitia mkutano mkuu wa Taifa ulisema tunataka mabadiliko, mkutano mkuu ukatoa mamlaka kwa uongozi ili kuhakikisha tunashirikiana na vyama vya wenzetu ambavyo ni makini

Membe alipokuja kwenye chama chetu, tulimwambia lengo letu ni kushirikiana na vyama makini na tulimwambia uko tayari akajibu yupo tayari. Mgombea wetu Bernard Membe haonekani. Ni afadhali mzee wa ubwabwa (Hashim Rungwe) anaonekana. Kamati ya uongozi kwa kauli moja pamoja na Membe tulikubaliana tumuunge mkono Tundu Lissu.

Sio kwamba hatumpendi Membe. Mimi ‘nam-challenge’ afanye hizo kampeni zake tuone hizo kampeni ziko wapi. Nia yake ni kutaka kuwachanganya Watanzania.

Alilosema Zitto si lake! Nililosema mimi Seif Sharif Hamad si langu! Bali ni maamuzi ya Chama. Ni msimamo wa ACT Wazalendo anayekaribia kumshinda Magufuli ni Tundu Lissu na huyo ndiyo tunamsapoti"

Zimebaki siku sana kwa wananchi kufanya maamuzi ya kuwachagua viongozi wanaowataka wao. Tunaelekea katika Uchaguzi Mkuu wakati wagombea wetu kadhaa wameenguliwa katika kinyang’anyiro hicho lakini tukafanye maamuzi

Nyakati zote mimi nilikua nawazuia watu wasiingie Barabarani! Sasa mwaka huu simzuii mtu. Yoyote atakayeamua kufanya lolote Afanye hiyo Tarehe 27 na 28. Wazanzibar wamepanga kulinda Demokrasia kwa gharama yoyote! Wamevuta subira kwa muda mrefu. Sasa Imetosha

Tulimwambia Benard Membe mapema wakati anakuja, kuwa tunashirikiana na chama makini na alikubali. Tuliona mgombea wetu haonekani bora, hata Mzee wa Ubwabwa (Hashim Rungwe) ni bora kuliko mgombea wetu, tukakubaliana kumuunga mkono Tundu Lissu

Kuna njama za wazi za kukamata viongozi wetu wa ACT Wazalendo na inasemekana yako maeneo yaliyotafutwa ili kuwaficha viongozi hao ili wasijulikane walipo mpaka uchaguzi uishe, sasa tunajiuliza serikali ya Chama cha Mapinduzi inaogopa nini?

Kuna minong'ono kuwa kuna vijana wa ACT Wazalendo wamevalishwa nguo za askari ili wakapige kura ya mapema. Kwa taarifa tulizonazo kuna zaidi ya wazanzibar 50,000 walionyimwa haki yao ya msingi ya kikatiba ya kupiga kura Zanzibar.
Maalim Seif, wewe ulikuwa ukishinda miaka yote ya uchaguzi Mkuu Zanzibar. Ulikuwa ukipokwa ushindi wako. Sasa basi. Safari hii uhuni huu basi.
 
Kabla ya kuchukua maamuzi hayo walimshirikisha Membe kwenye huo mkutano wao?
 
CCM walijua wameimaliza CHADEMA wakahisi ACT ndo itainuka wakamtuma membe bahati nzuri baada ya ACT kukubali kushirikiana na CHADEMA wakashtuliwa, na wasingekubali wangeishia kuzimu
 
Yani vitu vyengine havina kichwa wala miguu,hivi kweli haya mambo walijadili na kushindwa kufikia muafaka au wanatuletea mapicha picha tu?

Halafu kuna watu wanashabikia hii michezo ya wanasiasa.
 
Back
Top Bottom