Uchaguzi 2020 Maalim Seif: ACT Wazalendo hatuna mpasuko lakini Membe anataka kuwaaminisha Watanzania hivyo. Adai Mzee wa Ubwabwa ni bora kuliko Mgombea wao

Uchaguzi 2020 Maalim Seif: ACT Wazalendo hatuna mpasuko lakini Membe anataka kuwaaminisha Watanzania hivyo. Adai Mzee wa Ubwabwa ni bora kuliko Mgombea wao

Hahaha ma CCM sasa yamepata mwanya wa kutuibia.

Huyu Membe huyu anajidai anawatu, mbona hawaji kumuunga mikono?!

Ndio maana anafukuzwa kumbe, sasa anataka na huko ACT afukuzwe?!
 
Namhurumia sana Membe, nauhurumia sana upinzani. Je, ni Membe huyu aliyefuatwa Rondo na kupokelewa na chama kwa shangwe?! Leo hii anatupwa na kudhihakiwa?

Afadhali angebaki huru bila chama kama mimi. Pengine mabadiliko hayataletwa na vyama na wasaka vyeo kupitia vyama vya siasa, bali sisi wananchi tukiungana pamoja bila kuegemea chama chochote isipokuwa taifa letu.
 
. Kamati ya uongozi kwa kauli moja pamoja na Membe tulikubaliana tumuunge mkono Tundu Lissu.
Alilosema Zitto si lake! Nililosema mimi Seif Sharif Hamad si langu! Bali ni maamuzi ya Chama. Ni msimamo wa ACT Wazalendo anayekaribia kumshinda Magufuli ni Tundu Lissu na huyo ndiyo tunamsapoti"
Membe alipitishwa na kamati kuu na mkutano mkuu wa chama
Hivyo vikao havikufanyika hadi leo .Hivyo Membe ni mgombea halali aliyepitishwa kihali na vikao.Kumtengua kulitakiwa vikao vile vile vikae vitengue sio kigenge cha watu wawili watatu wakae waseme tumeamua.Membe shikilia hapo hapo ili vyama viwe na nidhamu ya kuzingatia katiba zao

Hata CHADEMA kusema wanamuunga mkono mgombea Uraisi Zanzibar ni uamuzi batili sababu wana mgombea Urais wao kule Zanzibar waliyemchagua kwa vikao halali. Na yeye asiogope ajitokeze kama Membe aseme yeye mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CHADEMA
 
Umesema kweli kabisa!
Membe alipitishwa na kamati kuu na mkutano mkuu wa chama
Hivyo vikao havikufanyika hadi leo .Hivyo Membe ni mgombea halali aliyepitishwa kihali na vikao.Kumtengua kulitakiwa vikao vile vile vikae vitengue sio kigenge cha watu wawili watatu wakae waseme tumeamua.Membe shikilia hapo hapo ili vyama viwe na nidhamu ya kuzingatia katiba zao

Hata CHADEMA kusema wanamuunga mkono mgombea Urais Zanzibar ni uamuzi batili sababu wana mgombea Urais wao kule Zanzibar waliyemchagua kwa vikao halali. Na yeye asiogope ajitokeze kama Membe aseme yeye mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CHADEMA
 
Maalim mkorofi sana huyu babu,kaingia ACT juzi tu keshaanza migogoro,kwanini walimpa baraka zote Membe za kupeperusha bendera ya Urais ilhali wanajua kabisa hafai!?

Sasa wameona hauziki, ndio maana wamebadilisha Gia angani

Kama kweli lengo la Membe ni kuitoa CCM basi imefeli
 
Habari wana jf, maalim seif ameongea na waandishi wa habari na kuzungumzia suala la membe huku akimtolea maneno makali sana.

Nimeshindwa kushangaa, leo hii maalim seif unasema membe katumwa? Mbona siku ya kumpitisha pale chamani kuwa mgombea uraisi ulimsifia sana?
Membe unalo la kujifunza, pole sanaView attachment 1605967View attachment 1605968View attachment 1605969View attachment 1605971
Hongera CDM kwa kushutka mapema, vinginevyo, angekuwa nawapiga kutoea ndani. Ni afadhali ss anatokea nje.
 
Mwenyekiti wa Act taifa anaongea na wanahabari jijini dar es salam

--

Nimesikitika sana kwa aliyoyazungumza ndugu yangu Bernard Membe, ACT-Wazalendo kupitia mkutano mkuu wa Taifa ulisema tunataka mabadiliko, mkutano mkuu ukatoa mamlaka kwa uongozi ili kuhakikisha tunashirikiana na vyama vya wenzetu ambavyo ni makini

Membe alipokuja kwenye chama chetu, tulimwambia lengo letu ni kushirikiana na vyama makini na tulimwambia uko tayari akajibu yupo tayari. Mgombea wetu Bernard Membe haonekani. Ni afadhali mzee wa ubwabwa (Hashim Rungwe) anaonekana. Kamati ya uongozi kwa kauli moja pamoja na Membe tulikubaliana tumuunge mkono Tundu Lissu.

Sio kwamba hatumpendi Membe. Mimi ‘nam-challenge’ afanye hizo kampeni zake tuone hizo kampeni ziko wapi. Nia yake ni kutaka kuwachanganya Watanzania.

Alilosema Zitto si lake! Nililosema mimi Seif Sharif Hamad si langu! Bali ni maamuzi ya Chama. Ni msimamo wa ACT Wazalendo anayekaribia kumshinda Magufuli ni Tundu Lissu na huyo ndiyo tunamsapoti"

Zimebaki siku sana kwa wananchi kufanya maamuzi ya kuwachagua viongozi wanaowataka wao. Tunaelekea katika Uchaguzi Mkuu wakati wagombea wetu kadhaa wameenguliwa katika kinyang’anyiro hicho lakini tukafanye maamuzi

Nyakati zote mimi nilikua nawazuia watu wasiingie Barabarani! Sasa mwaka huu simzuii mtu. Yoyote atakayeamua kufanya lolote Afanye hiyo Tarehe 27 na 28. Wazanzibar wamepanga kulinda Demokrasia kwa gharama yoyote! Wamevuta subira kwa muda mrefu. Sasa Imetosha

Tulimwambia Benard Membe mapema wakati anakuja, kuwa tunashirikiana na chama makini na alikubali. Tuliona mgombea wetu haonekani bora, hata Mzee wa Ubwabwa (Hashim Rungwe) ni bora kuliko mgombea wetu, tukakubaliana kumuunga mkono Tundu Lissu

Kuna njama za wazi za kukamata viongozi wetu wa ACT Wazalendo na inasemekana yako maeneo yaliyotafutwa ili kuwaficha viongozi hao ili wasijulikane walipo mpaka uchaguzi uishe, sasa tunajiuliza serikali ya Chama cha Mapinduzi inaogopa nini?

Kuna minong'ono kuwa kuna vijana wa ACT Wazalendo wamevalishwa nguo za askari ili wakapige kura ya mapema. Kwa taarifa tulizonazo kuna zaidi ya wazanzibar 50,000 walionyimwa haki yao ya msingi ya kikatiba ya kupiga kura Zanzibar.
The game is over
 
Maalim mkorofi sana huyu babu,kaingia ACT juzi tu keshaanza migogoro,kwanini walimpa baraka zote Membe za kupeperusha bendera ya Urais ilhali wanajua kabisa hafai!?
Walikuwa hawajamjua, ukitaka kujua kina cha maji ya bahari sharti uzamie.
 
Ninachojiuliza ni kwamba, Membe yupo hapo Dar. inamchukua gharama gani kwenda kuwanadi hata wagombea ubunge wa chama chake hapo Dar? Maana nauli ni sh. 400 kutoka anapoishi hadi kwenye mikutano ya kampeni!!!
Jasusi kanyanganywa taulo, na amegoma kuchutama, huyu angepewa nafasi ya uenyekiti angekipasua ACT kabisa
 
Sawa kabisa, lakini hawasikii mpaka nilinyosha mikono!
Mimi huwa nashangaa sana mpaka leo vyama vya upinzani vinapokea wanasiasa kutoka ccm., Ni lazima upigwe mstari mwekundu hawa watu ata wakija vipi muachane nao, muachane nao ni virusi kuliko ata korona
 
Back
Top Bottom