Maalim Seif amkaribisha Bernard Membe ACT-Wazalendo huku akimuonya kuwa asiwe na masharti

Maalim Seif amkaribisha Bernard Membe ACT-Wazalendo huku akimuonya kuwa asiwe na masharti

Habari ndio hiyo kurudi ccm -NO NEVER. CCM mujiandae kugaragazwa tena Zanzibar na the one and only one Mr Maalim.
Teh teh

Unajidanganya.

Ukipata muda kasikilize clip ya jana akitoka ikulu.

Kwamba maongezi mengine ni SIRI yao(yeye na mheshimiwa rais),unayajua hayo ya SIRI?
 
Kwahiyo cdm ikiisha kufa ndiyo USA wanamuondolea ban Makonda?
ACT itakuwa chama kikuu cha upinzani badala ya CHADEMA na huko ndiko kuunizwa kwa CHADEMA

In God we Trust
 
The same ballads gonna be sung again!
Hivi upinzani mnawaaminije hawa watu wa CCM waliosomea ujamaa na ujasusi?
Kwa akili zenu mnajipa asilimia kubwa kwamba membe anaaminika?

CCM walishawaambia kuwa wanna mbinu kibao, hii ni episode nyingine baada ya Lowassa, hamjiulizi kwanini haya maigizo huibuka kipindi Cha chaguzi?

[emoji125][emoji125][emoji125]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ndivyo Vyama vya upinzani wengi mnasema visited dola, wanatumiwa kama condom na kutelekezwa.
 
Hizo njama alienda kupanga na magu jana yaani membe akienda act maalim anajitoa anarudi ccm na anapewa shavu..
Naomba niishie hapo
Mshauri mkuu wa chama cha ACT- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amemkaribisha katika chama hicho aliyekuwa mwanachama wa CCM, Bernard Membe lakini akimuonya asiwe na masharti.

Maalim amtoa kauli hiyo siku chache baada ya Membe katika mahojiano na Mwananchi kudai kuwa alifukuzwa CCM kutokana na nia yake ya kutaka kupambana na mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Membe na makatibu wakuu wawili wastaafu, Abdulrahman Kinana na Yusufu Makamba walifikishwa mbele ya kamati ndogo ya udhibiti na nidhamu kujibu mashtaka ya kinidhamu.

Makada hao waliingia matatani baada ya sauti zao pamoja na za wanachama wengine watatu, kusambaa katika mitandao ya kijamii ikizungumzia kuporomoka kwa umaarufu wa chama hicho na uenyekiti wa Magufuli.

Makamba alisamehewa makosa yake wakati Kinana atakuwa chini ya matazamio kwa miezi 18, kipindi ambacho hataruhusiwa kugombea uongozi, wakati Membe amevuliwa uanachama na hivyo hataweza kutimiza ndoto yake ndani ya chama hicho.

Alipoulizwa na timu ya wahariri wa Mwananchi kuhusu Membe kujiunga ACT, Maalim Seif ambaye alifukuzwa CCM mwaka 1988, amemkaribisha Membe huku akisema yeye hawezi kurudi chama tawala.

“Ya ndugu yangu Membe sisi chama chetu kitampokea yoyote atakayekuja mradi asije na masharti,” amesema Maalim Seif.

Alipoulizwa kuhusu kuomba msamaha ili arejee CCM, Maalim Seif angeweza kuomba msamaha tangu wakati wa Mwalimu Julius Nyerere akiwa Mwenyekiti wa CCM.

“Wakati huo kulikuwa na mawazo hayo kwamba tumewaonea hawa vijana tumewafukuza, kwamba wakiomba radhi tutawarejesha. Mimi nikasema sijasahau kitu CCM nirudi kutafuta nini? Kwanza watuondoe, kwamba nitarudi CCM No, never. Sitorudi CCM,” amesema.
 
Membe+maalimu+zito+mbatia Hawa ni usalama wa Taifa mbowe na wasi wasi nae. ila Lisu ndo mpinzani kutoka moyoni.
 
Sasa mku wewe ulitaka kama Membe amefukuzwa ccm asiende kwenye chama chochote akae tu nyumbani? Wanasiasa wana ndoto zao za mbali acha usiwabanebane maisha yao ni kutokana na karata za siasa. Angeomba kwenda Chadema watasema Lowasa alituacha nawewe usije.

Ajiunge vicoba tu eti
 
Mshauri mkuu wa chama cha ACT- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amemkaribisha katika chama hicho aliyekuwa mwanachama wa CCM, Bernard Membe lakini akimuonya asiwe na masharti.
Very soon huyu Maalim atakwaruza na Kiongozi Mkuu Kabisa wa Chama - Ayattollah Mwami Zitto Ruyagwa Kabwe. Hii kazi ya "kukaribisha" watu sio ya Mshauri Mkuu wa Chama. 😎
 
Very soon huyu Maalim atakwaruza na Kiongozi Mkuu Kabisa wa Chama - Ayattollah Mwami Zitto Ruyagwa Kabwe. Hii kazi ya "kukaribisha" watu sio ya Mshauri Mkuu wa Chama. 😎
Lakini Membe ana mtaji mkubwa,Maalim Seif na Mwami sio wajinga ati,kutembelewa na 'Mike Blomberg'.
 
Siasa za Tz buaaaana ni zaidi ya choo cha jumuiya!
Endeleeni kutuburuza tu
Maalim usimtukane jiwe tena maana Jana umeonyesha madhaifu yako hadharani vigumu kukuamini tena
 
Huyu maalim kalambishwa ubuyu was ikulu kalewa😂😂, kasahau tune huru??

Anasema wameongea Mambo ya ndani mengine hawezi kuyasema?? Hayo Mambo NI yapi na kwanini asiyaseme??, Akae akijua WaTz sio wajinga wasiseme rais kakutana na vyama pinzani Bali amekutana na ACT pamoja na nccr (ccm c).

Kama chadema waliomba kukutana na rais na mpaka leo kagoma Hawa kawaita akiwa na ajenda gani??,
 
This time we can't fall into your trap[emoji6][emoji6][emoji6][emoji6]only fools can!!!!
CHADEMA IPO NDANI YA MIOYO YA WATU,labda matatizo yote ya wananchi yatatuliwe!suala ambalo ni gumu kutokea
2015 ni tofauti na 2020

2015 Lowasa aliondoka CCM kwa hiyari yake mwenyewe
2020 Membe kafukuzwa uanachama CCM, ni mtu huru, ana haki ya kujiunga chama chochote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ACT itakuwa chama kikuu cha upinzani badala ya CHADEMA na huko ndiko kuunizwa kwa CHADEMA
Kumbe vyama vyote hivi viwili. Ajenda yao kubwa 2020 ni kuwa chama kikikuu cha upinzani na sio kuuondoa utawala Wa ccm?
 
Lakini Membe ana mtaji mkubwa,Maalim Seif na Mwami sio wajinga ati,kutembelewa na 'Mike Blomberg'.
Mtaji mkubwa kushinda ule wa Lowassa na Sumaye? Well, CCM ina mtaji mkubwa zaidi - NEC, DEDs na polisi. Huu ndio ukweli. Unless sheria na vifungu vya Katiba virekebishwe, hakuna "mtaji" mwingine unaoweza kuwang'oa hawa jamaa madarakani
 
Back
Top Bottom