Maalim Seif amkaribisha Bernard Membe ACT-Wazalendo huku akimuonya kuwa asiwe na masharti

Maalim Seif amkaribisha Bernard Membe ACT-Wazalendo huku akimuonya kuwa asiwe na masharti

Membe ni mgombea urais wa CHADEMA
HAPO HAPO NA INAELEKEA, NA ANAKUBALIKA.
membe akigombea na kushinda kuta wawezesha akina Lisu kurudi nchini kwa amani na uchunguuzi wa kupigwa kwake risasi kufanyika kwa kina na wahusika kufikishwa mbele ya sheria.
HUENDA NDOTO HII IKAWA KWELI WENGI WAKASHANGAA
MWISHO WA CCM UMEFIKA
 
Kumbe vyama vyote hivi viwili. Ajenda yao kubwa 2020 ni kuwa chama kikikuu cha upinzani na sio kuuondoa utawala Wa ccm?
Huwezi kuondoa utawala wa CCM bila kwanza kuwa chama kikuu cha upinzani hilo haliwezi tokea.
 
Ukawa mwaka huu haupo!mpinzani halisi atabaki CHADEMA TU!ambayo kwayo itabaki mioyoni mwa wasomi!Ila kwa walio wengi watarudi CCM!
NCCR,TLP,ACT yatakuwa ni matawi ya CCM!!!

CCM inataka kukuza chama kipya cha upinzani ambacho ni ACT!!
Kwaiyo mwaka huu kuna uwezekano mkubwa Wa vyama vya upinzani kutoungana kama ilivokuwa 2015?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshauri mkuu wa chama cha ACT- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amemkaribisha katika chama hicho aliyekuwa mwanachama wa CCM, Bernard Membe lakini akimuonya asiwe na masharti.

Maalim amtoa kauli hiyo siku chache baada ya Membe katika mahojiano na Mwananchi kudai kuwa alifukuzwa CCM kutokana na nia yake ya kutaka kupambana na mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Membe na makatibu wakuu wawili wastaafu, Abdulrahman Kinana na Yusufu Makamba walifikishwa mbele ya kamati ndogo ya udhibiti na nidhamu kujibu mashtaka ya kinidhamu.

Makada hao waliingia matatani baada ya sauti zao pamoja na za wanachama wengine watatu, kusambaa katika mitandao ya kijamii ikizungumzia kuporomoka kwa umaarufu wa chama hicho na uenyekiti wa Magufuli.

Makamba alisamehewa makosa yake wakati Kinana atakuwa chini ya matazamio kwa miezi 18, kipindi ambacho hataruhusiwa kugombea uongozi, wakati Membe amevuliwa uanachama na hivyo hataweza kutimiza ndoto yake ndani ya chama hicho.

Alipoulizwa na timu ya wahariri wa Mwananchi kuhusu Membe kujiunga ACT, Maalim Seif ambaye alifukuzwa CCM mwaka 1988, amemkaribisha Membe huku akisema yeye hawezi kurudi chama tawala.

“Ya ndugu yangu Membe sisi chama chetu kitampokea yoyote atakayekuja mradi asije na masharti,” amesema Maalim Seif.

Alipoulizwa kuhusu kuomba msamaha ili arejee CCM, Maalim Seif angeweza kuomba msamaha tangu wakati wa Mwalimu Julius Nyerere akiwa Mwenyekiti wa CCM.

“Wakati huo kulikuwa na mawazo hayo kwamba tumewaonea hawa vijana tumewafukuza, kwamba wakiomba radhi tutawarejesha. Mimi nikasema sijasahau kitu CCM nirudi kutafuta nini? Kwanza watuondoe, kwamba nitarudi CCM No, never. Sitorudi CCM,” amesema.

Mhe Membe ana nia na malengo ya kugombea urais 2020 lakini Mhe Maalim Seif katujulisha kuwa alipokutana na Rais Dr Magufuli juzi Ikulu, Rais alimuhakikishia kuwa hana nia ya kuongeza hata siku moja baada ya kumaliza muda wake 2025! It means Act wazalendo hawata husika na uchaguzi wa Urais 2020 ni mpaka 2025! It means Act-Wazalendo will not field a candidate for President in 2020!!!
 
Binafsi naamini ktk siasa ya ushindani na namwona membe bado ana nafasi ya kujiunga na upinzani wa kweli ili alete mabadiliko na atimize NDOTO zake za kugombea urais wa Tanzania.Hivyo basi ni muda muafaka sasa ajiunge na ACT Wazalendo sasa...

NB:mods msiunganishe Uzi huu na mwingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom