Teh tehHabari ndio hiyo kurudi ccm -NO NEVER. CCM mujiandae kugaragazwa tena Zanzibar na the one and only one Mr Maalim.
ACT tayari tumekichukua
Rais kaongea na Seif Sharif Chairman wa ACT japo sio Kiongozi
Sent using Jamii Forums mobile app
Mtake radhi Dr Kikwete kumhusisha na huyu Mtovu wa nidhamu
Kikwete anaheshimu na kuunga mkono mamlaka 100%
Sent using Jamii Forums mobile app
ACT itakuwa chama kikuu cha upinzani badala ya CHADEMA na huko ndiko kuunizwa kwa CHADEMA
Mshauri mkuu wa chama cha ACT- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amemkaribisha katika chama hicho aliyekuwa mwanachama wa CCM, Bernard Membe lakini akimuonya asiwe na masharti.
Maalim amtoa kauli hiyo siku chache baada ya Membe katika mahojiano na Mwananchi kudai kuwa alifukuzwa CCM kutokana na nia yake ya kutaka kupambana na mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Membe na makatibu wakuu wawili wastaafu, Abdulrahman Kinana na Yusufu Makamba walifikishwa mbele ya kamati ndogo ya udhibiti na nidhamu kujibu mashtaka ya kinidhamu.
Makada hao waliingia matatani baada ya sauti zao pamoja na za wanachama wengine watatu, kusambaa katika mitandao ya kijamii ikizungumzia kuporomoka kwa umaarufu wa chama hicho na uenyekiti wa Magufuli.
Makamba alisamehewa makosa yake wakati Kinana atakuwa chini ya matazamio kwa miezi 18, kipindi ambacho hataruhusiwa kugombea uongozi, wakati Membe amevuliwa uanachama na hivyo hataweza kutimiza ndoto yake ndani ya chama hicho.
Alipoulizwa na timu ya wahariri wa Mwananchi kuhusu Membe kujiunga ACT, Maalim Seif ambaye alifukuzwa CCM mwaka 1988, amemkaribisha Membe huku akisema yeye hawezi kurudi chama tawala.
“Ya ndugu yangu Membe sisi chama chetu kitampokea yoyote atakayekuja mradi asije na masharti,” amesema Maalim Seif.
Alipoulizwa kuhusu kuomba msamaha ili arejee CCM, Maalim Seif angeweza kuomba msamaha tangu wakati wa Mwalimu Julius Nyerere akiwa Mwenyekiti wa CCM.
“Wakati huo kulikuwa na mawazo hayo kwamba tumewaonea hawa vijana tumewafukuza, kwamba wakiomba radhi tutawarejesha. Mimi nikasema sijasahau kitu CCM nirudi kutafuta nini? Kwanza watuondoe, kwamba nitarudi CCM No, never. Sitorudi CCM,” amesema.
Sasa mku wewe ulitaka kama Membe amefukuzwa ccm asiende kwenye chama chochote akae tu nyumbani? Wanasiasa wana ndoto zao za mbali acha usiwabanebane maisha yao ni kutokana na karata za siasa. Angeomba kwenda Chadema watasema Lowasa alituacha nawewe usije.
Very soon huyu Maalim atakwaruza na Kiongozi Mkuu Kabisa wa Chama - Ayattollah Mwami Zitto Ruyagwa Kabwe. Hii kazi ya "kukaribisha" watu sio ya Mshauri Mkuu wa Chama. 😎Mshauri mkuu wa chama cha ACT- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amemkaribisha katika chama hicho aliyekuwa mwanachama wa CCM, Bernard Membe lakini akimuonya asiwe na masharti.
Lakini Membe ana mtaji mkubwa,Maalim Seif na Mwami sio wajinga ati,kutembelewa na 'Mike Blomberg'.Very soon huyu Maalim atakwaruza na Kiongozi Mkuu Kabisa wa Chama - Ayattollah Mwami Zitto Ruyagwa Kabwe. Hii kazi ya "kukaribisha" watu sio ya Mshauri Mkuu wa Chama. 😎
Membe kwenda ACT inaiuwaje chadema??
Na akitokea asiende ACT akaenda chadema. Huo utakuwa mkakati upi mtaalam?
2015 ni tofauti na 2020
2015 Lowasa aliondoka CCM kwa hiyari yake mwenyewe
2020 Membe kafukuzwa uanachama CCM, ni mtu huru, ana haki ya kujiunga chama chochote
Kwaiyo mwaka huu kuna uwezekano mkubwa Wa vyama vya upinzani kutoungana kama ilivokuwa 2015?Kwa vyovyote vile ahamie ACT au CHADEMA au chama chochote kingne,lengo ni kuiangamiza CHADEMA-wenye macho matatu tumeona mbali Sana!
Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe vyama vyote hivi viwili. Ajenda yao kubwa 2020 ni kuwa chama kikikuu cha upinzani na sio kuuondoa utawala Wa ccm?ACT itakuwa chama kikuu cha upinzani badala ya CHADEMA na huko ndiko kuunizwa kwa CHADEMA
Mtaji mkubwa kushinda ule wa Lowassa na Sumaye? Well, CCM ina mtaji mkubwa zaidi - NEC, DEDs na polisi. Huu ndio ukweli. Unless sheria na vifungu vya Katiba virekebishwe, hakuna "mtaji" mwingine unaoweza kuwang'oa hawa jamaa madarakaniLakini Membe ana mtaji mkubwa,Maalim Seif na Mwami sio wajinga ati,kutembelewa na 'Mike Blomberg'.
Sanchez magoli, HIYO NDIYO TUZO YA JUU KABISA WANAYOWEZA KUFIKIAKumbe vyama vyote hivi viwili. Ajenda yao kubwa 2020 ni kuwa chama kikikuu cha upinzani na sio kuuondoa utawala Wa ccm?