GHIBUU
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 4,432
- 3,013
........ Hivi sasa kuna wimbi kubwa sana la viongozi wa vyama viwili vikuu vya upinzani kujivua uanachama wao kutoka vyama vyao na kujiunga na CCM kwa madai yanayofanywa, wako wabunge , madiwani na wanachama wa kawaida ambao wameshafanya hivyo.
Hawa wanachama wa kawaida sio neno kwasababu ni haki ya kila mtu kujiunga na Chama akipendacho na hata hao wabunge na madiwani nao wanaweza kufanya hivyo. Lakini tujiulize kweli Mbunge au Diwani pamoja na wadhifa na mshahara, posho na madukhuli mengine inaingia akilini kuwa hayo yote yasiwe kitu kwako ila jambo muhimu kwako ni kuridhishwa na utendaji wa Rais katika kuisimamia na kuitekeleza ilani ya Chama pinzani kwako iwe ndio sababu ya kukiwacha Chama chako?
Hebu turudi nyuma kidogo tumtazame Mbunge wa mjini mkongwe Zanzibar alivyotusimulia kuhusu hili, Mh Ali Saleh anasema "alikuwa nyumbani kwake asubuhi akasikia mtu anabisha hodi akaenda kumsikiliza kuingia ndani mazungumzo ni kuwa kaja lakini hakutumwa na mtu kumtaka Ali Saleh ahme kutoka Chama chake na ajiunge na CCM" je mpaka hapo hujatengeneza picha itayokuonesha kuwa sababu za hao waliohama vyama vyao si za kweli?
Lakini naomba ikumbukwe kwamba mchezo huu unaofanywa kwa juhudi kubwa sana za CCM na Serikali zake ni juhudi kubwa za kukiua rasmi Chama cha Mapinduzi , huwezi kujenga siasa katika mfumo wa vyama vingi kwa kununua watu katika siasa watu hawanunuliwi, lakini pia unajenga uadui ndani ya Chama chako kwasababu wale waliomo wanaona kuwa sisi tupo hapa kila uchao lakini Chama chetu kinatumia mamilioni ya fedha kuwarubuni watu wakiunge mkono Chama chetu lakini huyu anaerubuniwa una uhakika gani kama kweli moyo wake uko na hicho Chama kilichomrubuni? lakini pia huoni kama inapunguza "moral" ya kiutendaji kwa hawa ambao wamo kwenye Chama ambao hawayapati kama hayo waliopewa hao walionunuliwa? ndio pale mnapopanga mambo yenu kabla ya kikao habari ishafika kwa Lowasa, Sumaye, Mbowe, Mbatia pamoja na Maalim Seif tena Maalim Seif yeye hupata mapema zaidi na kuwaambia wenziwe tena lakushangaza habari zikifanyika hata Tanganyika basi yeye anazipata mapema zaidi na ushahidi upo katika mabaraza yote ya kawahawa wanamokaa CUF basi utazisikia kabla, nilijaribu kukaa katika baraza hizo tofauti hapa Unguja na Dar es Salaam nimejionea mwenyewe.
Katika jambo ambalo sasa liko wazi wazi ni suala la Tanzania kuridhia matakwa ya dunia kurejesha demokrasi ya mshindwa kukubali kushindwa na kukabidhi madaraka kwa alieshinda. Zanzibar kulifanyika uchaguzi mwaka 2015 katika mwezi wa Oktoba hapa hapana asiejua kama Chama cha CUF kilishinda uchaguzi ule na Seif Sharif Hamad alimshinda Dr. Ali Mohd Shein kwa zaidi ya kura 20,000 kwakuwa Tanzania kupitia Kikwete kwa wakati huo hawakuridhika na matokeo hayo ya kushindwa na CUF kwa makusudi wakamlazimisha mtu mmoja anaeitwa Jecha ambae alikuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC kufuta matokeo yote ambayo kisheria za uchaguzi na katiba ya Zanzibar haikuliani na hilo wakafuta kwa nguvu wakitumia Jeshi. Na baadae kuitisha uchaguzi mwengine mpya huku wakiwa wamesahau kuwa tume ilishawapa washindi wote certificate zao na kumfanya Seif Sharif Hamad kama mtoto mdogo na asiekuwa na uwelewa juu ya mambo haya katika dunia ya leo.
Kwakuwa Seif Sharif Hamad alisoma kitu kinaitwa "Political science" na akafaulu vizuri sana hapo Chuo Kikuu na kuifanyia kazi muda mrefu sana fani hio akaweza kuiambia dunia na dunia ikamuelewa na kwa kweli Taasisi moja iko Marekani inaitwa NDI ikafanya juhudi kubwa sana ya kutengeneza mpango makhususi ya kuratibu haya mpaka UN, EU, The Commonwealth, Liberal Party International na USA wakakubali kuwa ni lazima demokrasi ifate mkondo wake Zanzibar na mshindi alieshinda akabidhiwe madaraka sasa Tanzania kwakuwa mara zote huwa wanacheza mchezo huu mara hii shughuli imewashinda na muda wowote Zanzibar kutatokea mabadiliko makubwa ya uongozi na utawala hili halitaki tena vikao sasa ni utekelezaji tu. Niliwahi kuzungumza na mtu mmoja kutoka Zimbabwe akasema yeye anamfahamu vizuri Seif Sharif Hamad na aliwahi kumfundisha akiwa chuo kikuu Dar es Salaam miaka ya 70 huyu mtu anaitwa Nathan Chamwiarira sijui yuko wapi siku hizi lakini alinambia hivyo.
Leo Ikulu ya Dar es Salaam haishi vikao kujadili ni vipi watafanyakazi na Seif Sharif Hamad huku wakijua kwamba Tanganyika kuna upinzani wa hali ya juu hivi sasa na Zanzibar CUF wanaingia madarakani na kwa upande wapili huyu alioko Zanzibar ni mwana UKAWA ndio ukaona hizi juhudi zinazofanyika za kuitia CUF katika mgogoro mkubwa wa kiuongozi na CHADEMA kuwarubuni wabunge na madiwani pamoja na kuwafungulia mashtaka Mbowe na wwenzake ili ipatikane nafuu kwa CCM iendelee kukaa madarakani lakini juhudi hizo zote haziwezi tena kufanikiwa kwasababu fedha haiwezi kuinasua siasa siasa moja kwa moja iliyobaki ni Serikali kukamilisha hili baadae tukaanza siasa za kistaarabu ili nchi yetu iepukane na umwagaji wa damu.
Kama nilivyoipokea.