Zanzibar 2020 Maalim Seif: Nitakubali matokeo ikiwa Uchaguzi Mkuu utakuwa huru

Zanzibar 2020 Maalim Seif: Nitakubali matokeo ikiwa Uchaguzi Mkuu utakuwa huru

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema atakubali matokeo ya uchaguzi hata kama atashindwa ikiwa uchaguzi utakuwa huru na wa haki.

Maalim Seif alitoa masharti hayo jana alfajiri wakati akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuhusiana na mambo mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu.

Alisema hayo baada ya kuulizwa kama atakubali matokeo yakionyesha ameshindwa kwa mara nyingine.

"Nimewaambia ikiwa uchaguzi utakuwa huru na wa haki, mimi sina tatizo kumpongeza Dk. Hussein Mwinyi (mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi- CCM)," alisema.

Hii ni mara ya sita kwa Maalim Seif kugombea urais wa Zanzibar.

Akizungumzia suala la wagombea wa ACT-Wazalendo ambao wameenguliwa kugombea katika nafasi mbalimbali, alisema chama kilifuata njia za kisheria kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC). Alisema kutokana na hatua hiyo, baadhi walirejeshwa na wengine hawakurejeshwa.

"Tulikata rufaa (rufani) kwa ZEC kwa wale wa Baraza la Uwakilishi wengine wamerejeshwa. Tunakwenda kwenye uchaguzi maeneo mengine ACT- Wazalendo haina wagombea," alisema.

Maalim Seif alisema wagombea wa nafasi ya uwakilishi ambao hawajarejeshwa itakuwa imeshatoka lakini kwa nafasi ya ubunge sheria inaruhusu baada ya uchaguzi wanaweza kufungua kesi mahakamani.

Kuhusu vipaumbele vyake ikiwa atapewa ridhaa ya kuwa rais, alisema kitu cha kwanza atakachokifanya ni kuunganisha wananchi wa Zanzibar ili kuleta maendeleo.

Maalim Seif pia alisema atainua hali ya maisha ya wananchi ambayo hivi sasa wanakabiliwa na hali ya umaskini kiasi kwamba hata mlo kwa siku umekuwa wa taabu.
 
Hapa ndipo ninapowashangaa wenzangu wapinzani. Mpaka leo hii, uchaguzi si huru , yaani mapaka sasa leo na dakika hii uchaguzi ni batili, sasa Maalim anasubiri kitu gani batili? Hakuna uchaguzi huru na wa haki hadi dakika hii. If action should start now! Not jioni au kesho...
 
na safari hii ukikosa urais ukapumzike Oman huko sasa maana umepigania urais kweli kweli hadi jasho...
 
Hapa ndipo ninapowashangaa wenzangu wapinzani. Mpaka leo hii, uchaguzi si huru , yaani mapaka sasa leo na dakika hii uchaguzi ni batili, sasa Maalim anasubiri kitu gani batili? Hakuna uchaguzi huru na wa haki hadi dakika hii. If action should start now! Not jioni au kesho...
Nguvu yao ni nyie wanannchi. Mpo tayari?
 
Ninakubaliana na wewe kabisa, huku kitaa watu wamechoka hawana hamu na CCM kabisa. Wako tayari kwa njia mbadala kwani haki imenyongwa.
Nilitegemea hili la Chato kutowaapisha mawakala wa CDM watu waingie mitaa/barabarani , lkn naona kimya, tunafanyaje hapo?
 
Nilitegemea hili la Chato kutowaapisha mawakala wa CDM watu waingie mitaa/barabarani , lkn naona kimya, tunafanyaje hapo?
Hujuma ni nyingi mno, lakini tutafika. Tunasubiri kipenga cha kamanda mkee mwenye dhamana.
 
1603357434938.png

huu ni ubaguzi wa wazi mchana kweupe.
 
No way, utakufa mwenyewe, sisi wengine tunajua CCM ni Chama makini, hiyo CHADEMA mnayotaka kufa kwa ajili yake, ufe mwenyewe, wakati Mwenyekiti wenu akitafuna hata ruzuku hamjui ziko wapi, je mkipewa nchi, mtabakiza gofu
 
Hata asipoyakubali dunia haiwezi kusimama!

BTW:Lini aliwahi kuyakubali?
 
ni aidha Bara ama Visiwani... mmoja lazima akose mwengine apate... ngoja tuone
 
No way, utakufa mwenyewe, sisi wengine tunajua CCM ni Chama makini, hiyo CHADEMA mnayotaka kufa kwa ajili yake, ufe mwenyewe, wakati Mwenyekiti wenu akitafuna hata ruzuku hamjui ziko wapi, je mkipewa nchi, mtabakiza gofu
Nilidhani naongea na sensible man, a rational one kumbe uko hivyo! Spana kali from now!
 
Uchaguzi hauwezi kuwa “huru” kwa TUME inayoteuliwa na Viongozi wa CCM. Lazima tu kutakuwa na tendencies za kujipendekeza/kulipa fadhila.

Maalimu mara hii keshasahau walichomfanyia mwaka 2015? CCM wapo radhi kuua watu kadhaa kuliko kuikabidhi Zanzibar kwa Maalim Seif. Walishafanya hivyo kitambo na hawatoacha kufanya hivyo mwaka huu.
 
Ninakubaliana na wewe kabisa, huku kitaa watu wamechoka hawana hamu na CCM kabisa. Wako tayari kwa njia mbadala kwani haki imenyongwa.
Wakuu kama Uchaguzi utakua huru na wa HAKI na Magufuli akatushinda tumpongeze mara moja hii ni Nchi yetu hakuna haja ya kuipiga Kiberiti

Ila iwapo tutaibiwa na ikithibitika tunawaogesha na Petroli halafu tunachomoa Betri

Akishinda kwa haki nitamnunulia maua
 
Kaanza kulainika taratibu, anajua hawezi kushinda, anaanza kuwaandaa kisaikolojia misukule yake, kama mwenzake lisu na sultan watagaragazwa vibaya, wote ni losers
 
Back
Top Bottom