Bulamba
JF-Expert Member
- Sep 17, 2011
- 13,741
- 13,049
NEC sio NACTE.Uchaguzi sio mtihani.Ni kuhakiki ambao wanastahiki kuwa viongozi mfano masuala ya uraia na masuala ya maadili.Hivi ukiingia chumba cha mtihani kwenye mitihani ya mwisho (final exams) mfano wa kidato cha sita , ukikosea hata kuandika namba yako ya mtihani na ukarejesha karatasi bila uhakiki, lawama utampa msimamizi, msahihishaji ama msoma matokeo au Wewe mwenyewe?
Mbona enzi za Kikwete na Mkapa wagombea wote walikuwa wanapata haki yao ya kikatiba ya kugombea na kuchaguliwa?
Mbona tunapoenda kuomba pasipoti tunarudishwa mara kumi kumi mpaka tujaze kwa usahihi fomu za maombi.
Mbona wanaokatwa ni wa upande mmoja tu.
Watu wa NEC wanaofanya dhuluma wajue hii ni dhuluma na malipo yao yatakuwa hapa hapa duniani.Watu wanaoshabikia uhuni wa NEC nao watapata malipo hapa hapa duniani kwa kushangilia dhuluma.
Januari Malamba amesikitishwa na uhuni wa NEC.Alitamani ashinde kihalali kwa kupitia sanduku la kura kwa vile anajiamini bado ana ushawishi.