Zanzibar 2020 Maalim Seif, punguza ukali wa maneno kutunza heshima yako

Wala hakukosea kujaza kama mnavyodhani hawa jamaa wana rough mbaya sana hasa kwenye kuforge documents. Ukiwa nje unawezasema ni uzembe wa wagombea.
Hizo documents wanazozisambaza mitandaoni ni feki wamezichezea.
 
Mkuki kwa nguruwe! Sisi malofa na wapumbavu tumeshazoea kuitwa hivyo!
 
Kwani tume ya uchaguzi ni tume ya mtihani ?
 
Rais wa sasa wa JMT huwa yupo worse kuliko haya unayomtuhumu nayo Maalim.
List ipo ulitaka!
 
Wacha kutuletea FIGISU ZA USALAMA WA TAIFA TISS katika harakati zao za mapishi
Hakuna mgombea wa upinzani anayeweza kushindwa kujaza fomu. Watu wengi wenye elimu ndogo na wajinga, wamejaa CCM. Kwa nini hayo makosa yasionekane na huko CCM?

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajua wee ndugu yangu Kuna wakati huwa nakushangaa sana.
Kama unadhani wamebadilishiwa hizo fomu Kama unavyosema kwanini hawa wabunge wasitoe copy za fomu walizo jaza sahihi? Kama wanaweza kuweka post kibao za kulalamika kwanini wasiweke na huo ushahidi wa hizo fomu zao walizo badilishiwa?
Hivyo ndivyo walivyojaza usitake kuwatetea mkuu.

Kweli ccm kuna majuha wengi tu lakini inavyo onekana Kuna watu maaluma kwenye kila Kanda wanao wasimamia hawa wagombea wao kujaza hizi fomu na wanazipitia kikamilifu.
Hata huku upinzani pia inaonekana Kuna baadhi ya majimbo wamekuwa makini sana kusimamia ujazaji fomu mfano mzuri ni kawe kwa halima Mdee umesikia Kuna diwani hata mmoja kakatwa au bunda kwa Bullaya umesikia Kuna mtu kaenguliwa? Bullaya ni mjanja sana watu wake aliwapiga lecture mapema shida inakuja kwa hawa wajuaji na CHADEMA bado hawajawawekea watu wao misingi mizuri.
 
Mkuu Mimi sitaki kuamini kuwa heti hujui kuwa uchaguzi ni kitu kinachoendeshwa kwa Sheria na kanuni na kwamba ukikosea mojawapo ya kanuni maana yake kwamba tayari umekosa vigezo vya kuendelea na mchakato wa uchaguzi.

Yani unatuletea mfano wa kujaza fomu za laini za simu kwenye ishu ya kikatiba Kama uchaguzi mkuu serious?

Hakuna huruma inayo tumika kwenye uchaguzi hapo ni kufuata Sheria na kanuni tu ndo kinachotakiwa, huwezi ukaulizwa tarehe ya kuzaliwa we unaandika 2020 au sehemu ya kuandika jina la Jimbo we unaandika jina la mgombea kanuni ziko wazi hapo lazima utaenguliwa.
 
Kiufipi ccm si watu wazuri kwa maendeleo ya kila mmoja mmoja.zanzibar uchaguz huwa unachakachuliwa kila mwaka wa uchaguz, wawaache wachague wanao wataka, si kuhanithi chaguzi, hiyo ni dhambi kama dhambi zingine
 
Sawa kabisa kutumia maneno hayo. NEC na wasimamizi wao wankera sana. Hakuna kiongozi hapa nchini apata kuwa na maneno makali kama ya Hayati Nyerere akitendewa dhuluma.
 
Sawa kabisa kutumia maneno hayo. NEC na wasimamizi wao wankera sana. Hakuna kiongozi hapa nchini apata kuwa na maneno makali kama ya Hayati Nyerere akitendewa dhuluma.
Uongozi wa NECK unataka kuvuruga tunu za nchi yetu.
Spunda Rungwe akiingia madarakani awasukumie ndani.
 
Kwa jamii iliyostaarabika hapo ilikuwa ni suala la kumuelekeza tu.
Kwa jamii iliyostaarabika ni wakali kuliko hilo. Sasa kama mgombea hajui kujaza fomu ya kugombea alafu anaomba kuwaongoza watu maelfu inakaaje? Hata kama ni Profesa ni bora tupa kule
 
Walichomfanyia kule Pemba siyo kizuri, tena angeongeza maneno makali zaidi muache ushamba wenu. Mnawaengua wagombea wao majimbo karibia yote hizo akili au matope.
Naona leo yuko meza moja na yule khanithi, sasa sijui wote wamekuwa makhanithi ama vipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…