Maalim Seif Shariff Hamad Aitikisa SMZ

Mwenzio nshapata jimbo na 2010 nitakuwa Chukwani(jengo jipya la BLW) Inshallah. Ila hayo ya kutengeneza mabomu a a a!! kazi hiyo ni ya usalama wa taifa uchwara wa SMZ wanaotaka kuwazuga watu na dunia kuficha upuuzi wao wa kuhujumu demokrasia, Pemba hawauwani kwa mabomu bali kwa halbadiri na hii ni maalumu kwa wanaodhulumu tu si kwa barabara na madaraja ambayo hayajamkosea mtu, sasa we huoni viusalama vyao vya taifa vilivyokuwa vifyefye wa kufikiri, hata kuzuga hawajuwi au wanatumia mbinu za kizamani za kuzuga.
 
Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF, Maalim Seif Shariff Hamad ameishushia lawama nzito Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(SMT) kuwa inahusika moja kwa moja kuvuruga uchaguzi mkuu wa Zanzibar 2010.
Akizungumza na Idhaa ya kiswahili ya BBC ya Uiengeraza, Maalim seif amesema, hali hiyo inatokana na hali inayoonekana kuwa ni shinikizo la SMT kutaka watu wenye sifa za kuandikishwa wasiandikishwe na wengine kutoka bara wasiokuwa na sifa kuandikishwa.
"...nashangaa licha ya agizo la Rais Karume kutaka wale wenye haki na sifa waandikishwe bado kumekuwa na uzito wa kutekelezwa agizo hilo na tume, jambo linaloonyesha kuwa kuna nguvu zaidi ya mamlaka yake(Karume) zinazoshinikiza hali hiyo" alisema Maalim Seif.
Kadhalika Maalim amesema kuwa kuna taarifa za uhakika kuwa kuna watu kutoka Pangani wameonekana na vitambulisho vya ukaazi, wakitayaarishwa kwa ajili ya kuandikishwa katika DKWK.
Akijibu madai hayo ya Maalim Seif Katibu Mwenezi wa CCM Cpt.John Chiligati alisema kuwa licha ya kuwa madai hayo hajayasikia lakini haoni ukweli wake kwa kuwa chaguzi za Zanzibar zinaongozwa kwa sheria za uchaguzi za huko,ukiondoa uchaguzi wa rais wa Muungano na wabunge.
"Nashangaa madai hayo kutolewa na Maalim Seif akiwa huku bara(Buguruni) badala ya kuyatolea huko huko Zanzibar katika vyombo husika, kuna Mahakama, tume n.k..." alijibu Chiligati.
Akijibu majibu hayo Maalim Seif alisema kuwa ni kawaida ya SMT kujifanya hawahusiki kwa mambo wanayotaka.
"...chaguzi za Zanzibar zinahusiana pia na chaguzi za bara kwa kuwa wapiga kura hao hao wanaoandikishwa na ZEC, wanatumia sheria za uchaguzi za Zanzibar kuchagua rais wa Muungano na tume ya uchaguzi ya zanzibar(ZEC) ni wakala wa Tume ya uchaguzi ya Tanzania(NEC)..." alisema Maalim Seif.

SOURCE:BBC SWAHILI SERVICE.
 
Tanzania ni Nchi ya kuigwa barani Obama kesha sema so haya ya Maalimu sijui inabidi akanyage kweli kweli .UN kuna Asha Rose Migiro kuna kazi kubwa ya wazungu kuujua ukweli kirahisi
 
I just cannot get it .CCM wanasema wao wana deliver na wana aminika lakini kifikia katika chaguzi na haki kutafutwa lazima maguvu mengi mizengwe na hata kutangaza washindi kwa nguvu why all that ?
 
Malecela amenukuliwa(Mwananchi) akisema kuwa CCM ina mbinu nyingi za kushinda uchaguzi.


Alisema CCM ina mbinu nyingi na hawajawahi kuzitumia zote katika chaguzi zao na kwamba, baadhi ya mbinu mpya walizonazo walizitumia katika chaguzi ndogo zilizopita hivi karibuni na wakaibuka kidedea.

"Tuna mbinu nyingi za kuwashinda wapinzani wetu, baadhi yake zilitumika katika chaguzi zilizopita na katika uchaguzi mkuu mwaka ujao tutazindua mbinu mpya ambazo hatujawahi kuzitumia."

MWANANCHI.
 
Na hii imehusu nini na bandiko hili?
 
Na hii imehusu nini na bandiko hili?


Kibunango sitaki kuamini kwamba wewe ni mtupu kiasi hicho kwamba huoni connection na bandiko hili .Hapa issue ni uchaguzi na huwezi kupiga kura kama huna kadi ya kupiga ama kuandikishwa .Malecela kasema wana mbinu nyingi za kushinda .Sasa mojawapo ya mbinu kushinda huko kwa Wagunya ni kuwavuruga na kuwanyima kuandikishwa.Umeamka ama bado umelala ?

Duh !!
 
Huyu mnayemwita Maalim anatumia umaarufu wake vibaya! Ahahisi tu kwamba kuna shinikizo kutoka SMT na hana ushahidi wowote wa SMT kuishinikiza SMZ au ZEC. Kimbelembele cha CUF na maalim wao ndio kinachokiponza chama! SMT inaonekana kwa Wapemba kuwa ni jalala la kutupia takataka za toka huko Pemba hata zisizoihusu. Shame on you maalim na mabomu yako ya kulipua madaraja!
 


Buchanan
Tuache ushabiki Watanzania wenzetu wanaumia Pemba na kama hatuwezi kukemea siku itahamia bara japokuwa tayari iko ki aina .Tumeshuhudia tabia ya CCM kutumia polisi wengi na vurugu katika chaguzi na hata kuamua kutangaza matokeo hata kama wameshindwa .

Kule Pemba wanaichukia Serikali kwa uhalali maana wanayo tendewa si ya kawaida .Yaani watu wananyimwa kujiandikisha vipi ? Usalama wa Taifa kulaa vituoni maana yake nini ?Head Usalama ni mmoja , Amiri Jeshi mmoja , IGP mmoja leo mambo yanafanyika wakisema unasema nini ? Tuwatendee haki watanzania wale .CCM ijue madaraka yanapatiana kwa rishaa na si zaidi .
 

Katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Magogoni hakukutokea malalamiko yoyote toka CUF na kwa mara ya kwanza katika historia ya kuundwa kwa chama hicho kilikubali matokeo! Kulalamika kwa CUF huwa ni technique ya kutafuta public sympathy, yaani wao ni kulalamika tuuuuuuu! Muda si mrefu watakimbilia UN na kwa bahati mbaya nchi za magharibi ikiwepo Marekani na Uingereza zimeshasomeshwa na CCM kwamba CUF ni chama cha kigaidi (kidini) na wameelewa somo hilo! Wamebaki kulialia tu Buguruni! Poleni sana CUF, mwakani mtaachilia kiti cha siku nyingi cha Chama Kikuu cha Upinzani kwa CHADEMA!
 
Mimi sipendi kuamini kuwa u mvivu wa kupima mambo kwa kina namna hii! Matatizo yote kabla na baada ya uchaguzi hutokea Pemba, licha ya CUF kuwa ndie kidedea huko tena kwa kishindo!

CCM, SMZ na sasa SMT wala hawana muda wa kupoteza kuhusu Pemba wala kutumia mbinu yoyote kisiwani humo, na hii inatokana na rekodi ya awamu tatu sasa za chaguzi.

Hata hivyo, ikumbukwe kuwa huko PBA, pamoja na wengi kuwa ni CUF, bado chama hicho kinaendeleza tabia yake ya kupandikiza watu. Kwa safari hii wamekumbana na kisiki, na ndio maana akina Maalimu wanalia lia na kuwashawishi Wapemba kuwa materoristi.
 
Na hii imehusu nini na bandiko hili?
Malecela anasisitiza tena hapo juu kuwa mbinu nyingine hata bado hawajazindua, hebu vuta tafakuri kidogo ikiwa mbinu kongwe tu, tu-maji kama hivi, je hizo mbinu mpya tutakuwa hali gani?
 

Nikweli sumu ilianza kumwagwa siku njingi na CCM kuwa CUF ni chama cha Kidini (Kisilamu )na miongoni waliokuwa wakipita kila kona kusema hilo hakuna mwengine isipokuwa aliyekuwa waziri wa mambo ya Nje, na sasa ni Rais Jk alikuwa akipita na kusema kwa nchi za ulaya na marekani kuwa hawa CUF ni waisilamu sana kupindukia uisilamu wao ni mbaya kwa usalama wa Dunia na pale anapoulizwa kwani wewe si muisilamu vile vile ?husema uisilamu wake ni tafauti na ule uisilamu wa Zanzibar (kwa mana nyingine wake ni mwepesi na hautilii manani sana)
 
WaTanganyika msiwe na haraka na kuiponda CUF au kumponda Maalim Seif Sharif Hamadi SImba wa Nyika ambae sio anaitikisa SMZ peke yake ,anaitikisa hata Serikali ya Muungano tena amefika mbali sana natumai hotuba yeke aliyoitoa baada ya Raisi Kikwete kutembelea Pemba na kufungua bomba la upepo mliisikia vizuri sana.

CUF kama Chama kikuu cha Upinzani Tanzania basi itegemewe kuwa kufanikiwa kwake ni kufanikiwa kwa vyama vyote vya upinzani ,vita inayopigana CUF sio vita ya mchezo ni vita kuu kabisa katika siasa za Tanzania.

CUF haina wafuasi wengi kama walioko Bara (Tanganyika) ,kama mnavyopima idadi ya wananchi wa Zanzibar kwa kulinganisha na jimbo au mtaa wa bara basi inatakiwa muelewe kuwa kwa upande wa wafuasi CUF inao wafuasi wengi zaidi huku Tanganyika.

Kitu wanachokifaidi CUF ni ile kuwazidi wapinzani wa CCM walioko Zanzibar na hivyo kuifanya CCM Utawala kufikia kufanya vitendo vya kinyama au kuwazidi wanyama.
Ukweli haupo mbali utajulikana pindipo upande wa Bara wananchi wengi wataanza kuikataa CCM hapo ndipo mtakapoona ni kwa nini CCM ilikuwa inafikia stage ya unyama katika chaguzi za Zanzibar.

Kama vitendo vilivyotokea Pemba vimefanywa na wazalendo wenye kuchoka na utawala wa CCM nitakuwa mwenye kufarijika sana na kuona kuwa sasa tunaingia katika hatua nyingine ya kuzipinga tawala za kidhalimu ,hatua ambazo wananchi wa Nchi nyengine wamezifikia na kuwasaidia katika kuziondoa tawala zao za kidhalimu.

Kinachonifanya niamini kuwa mambo yaliotokea na yanayoendelea kutokea Pemba yametayarishwa na mapolisi yaliopelekwa na Kikwete ni kuwa hakuna alieathirika na milipuko hiyo kwa misingi ya kuwa anaeonewa ni lazima ajeruhi tu na kuuwa kwake inakuwa rahisi sana pindipo akiwa na zana zinazomuwezesha kufanya hivyo na hajali matokeo kuwa nae atakamatwa ,hilo halijali kabisa mtu ambae amechoka na dhulma au amechoka kudhulumiwa.

Kama Wapemba wangekusudia kumlipua sheha na familia yake na nyumba yake wala wasingepata tabu sana ni jambo rahisi sana kulitekeleza wala si kwa kutumia mabomu dramu la petrol lingetosha kabisa ,kumaliza sheha aliekuwa amelala usingizi mnono.

Haya ni mambo yaliyopangwa na hao mapolisi waliokwenda kwa makundi huko na sasa inaonekana namna wanavyotekeleza yale waliyoyaandaa au waliyopangiwa kuyafanya ila kasoro inayojitokeza ni kuwa wanatekeleza kiwoga woga hawatekelezi vile inavyotakiwa ,matokeo yawepo mazuri kuwa masheha wakumbwe na vifo ,waandikishaji walipukiwe na mabomu.

Hapo ndio utaona kuwa mambo haya ni ya kupangwa na ni ya woga woga maana ikitokea mmoja wapo kukamatwa basi itakuwa ni aibu kubwa na hilo ndilo wanaloliogopa wale wanaopanga hila hizo ,eti wamewaona wakikimbia kwenye mashamba ya migomba.

Pemba Nchi ambayo imetawaliwa na kiza , ukisimama tu mtu hakuoni. Kichekesho nilichokiona kwa waliopanga habari za matokeo ni pale aliposema kuwa Sheha alikuwa amelala akasikia watu wanachimba nje ya nyumba yake akafungua mlango na kuelekea nyuma ya nyumba kufika huko watu walikuwa wakichimba ambao walikuwa wawili wakakimbia na mara ukatokea mripuko hapo ,sheha akaanguka na ukuta nao pia ukaanguka ,yaani ni hadithi ya paukwa pakawa ,panga upangavyo lakini kwa kitendo hiki sheha angepoteza maisha ,hakuna asieelewa mlipuko wa baruti za kupasulia miamba ,halafu unatwambia sheha amepona ,maana kiakili tu sheha lazima angesogea pale palipokuwa pakichimbwa kuona ni kitu gani kilikuwa kinachimbwa ,kwa waliokimbia lazima watakuwa wamesimama na kuona alietoka kama anawafuata au anafanya kitu gani ,jamani kama hamujui kupanga habari tukodisheni tuwapangie newz.
 

Tatizo lako unaamini kila anachosema maalim Seif kwamba ni kweli. Mbona hajatoa ushahidi wa shinikizo la SMT kwa ZEC? Mbona haendi mahakamani kulalamika basi na kufungua mashtaka kama madai yake ni ya kweli? Ni mara ngapi tumeona chaguzi za bara matokeo yake yakibatilishwa kwa sababu ya mambo mbalimbali kutokwenda vizuri? Kwa Seif ni malalamiko tu kwenye vyombo vya habari! Hajui kwamba vyombo vya habari navyo vina yao? Otherwise, kuamini kila neno toka kwa Seif na CUF tutalishwa pumba mara nyingine!
 

Hujaelewa, ni chama cha Kigaidi!
 
Malecela anasisitiza tena hapo juu kuwa mbinu nyingine hata bado hawajazindua, hebu vuta tafakuri kidogo ikiwa mbinu kongwe tu, tu-maji kama hivi, je hizo mbinu mpya tutakuwa hali gani?
Mbinu ambazo zinazosemwa si zingine zaidi ya kampeni katika sura mpya, CCM haina mbinu chafu kama wengi mnavyotaka kusushawishi.

Tena mnakosea sana kusema kuwa CCM inacheza rafu Pemba! Zaidi ni CUF ambayo inatumia rafu ili kuweza kuwaingiza watu hao Unguja kwa kupiga kura.
 

Hisia hizi hazina tofauti sana na zile za maalim Seif, hana ushahidi wowote wa kuona. Kama angekuwa nao si angekimbilia mahakamani? Otherwise, tutashindwa kutofautisha lipi limefanywa na hao unaowaita mapolisi na lipi limefanywa na hao unaowaita wazalendo wa Pemba!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…