WaTanganyika msiwe na haraka na kuiponda CUF au kumponda Maalim Seif Sharif Hamadi SImba wa Nyika ambae sio anaitikisa SMZ peke yake ,anaitikisa hata Serikali ya Muungano tena amefika mbali sana natumai hotuba yeke aliyoitoa baada ya Raisi Kikwete kutembelea Pemba na kufungua bomba la upepo mliisikia vizuri sana.
CUF kama Chama kikuu cha Upinzani Tanzania basi itegemewe kuwa kufanikiwa kwake ni kufanikiwa kwa vyama vyote vya upinzani ,vita inayopigana CUF sio vita ya mchezo ni vita kuu kabisa katika siasa za Tanzania.
CUF haina wafuasi wengi kama walioko Bara (Tanganyika) ,kama mnavyopima idadi ya wananchi wa Zanzibar kwa kulinganisha na jimbo au mtaa wa bara basi inatakiwa muelewe kuwa kwa upande wa wafuasi CUF inao wafuasi wengi zaidi huku Tanganyika.
Kitu wanachokifaidi CUF ni ile kuwazidi wapinzani wa CCM walioko Zanzibar na hivyo kuifanya CCM Utawala kufikia kufanya vitendo vya kinyama au kuwazidi wanyama.
Ukweli haupo mbali utajulikana pindipo upande wa Bara wananchi wengi wataanza kuikataa CCM hapo ndipo mtakapoona ni kwa nini CCM ilikuwa inafikia stage ya unyama katika chaguzi za Zanzibar.
Kama vitendo vilivyotokea Pemba vimefanywa na wazalendo wenye kuchoka na utawala wa CCM nitakuwa mwenye kufarijika sana na kuona kuwa sasa tunaingia katika hatua nyingine ya kuzipinga tawala za kidhalimu ,hatua ambazo wananchi wa Nchi nyengine wamezifikia na kuwasaidia katika kuziondoa tawala zao za kidhalimu.
Kinachonifanya niamini kuwa mambo yaliotokea na yanayoendelea kutokea Pemba yametayarishwa na mapolisi yaliopelekwa na Kikwete ni kuwa hakuna alieathirika na milipuko hiyo kwa misingi ya kuwa anaeonewa ni lazima ajeruhi tu na kuuwa kwake inakuwa rahisi sana pindipo akiwa na zana zinazomuwezesha kufanya hivyo na hajali matokeo kuwa nae atakamatwa ,hilo halijali kabisa mtu ambae amechoka na dhulma au amechoka kudhulumiwa.
Kama Wapemba wangekusudia kumlipua sheha na familia yake na nyumba yake wala wasingepata tabu sana ni jambo rahisi sana kulitekeleza wala si kwa kutumia mabomu dramu la petrol lingetosha kabisa ,kumaliza sheha aliekuwa amelala usingizi mnono.
Haya ni mambo yaliyopangwa na hao mapolisi waliokwenda kwa makundi huko na sasa inaonekana namna wanavyotekeleza yale waliyoyaandaa au waliyopangiwa kuyafanya ila kasoro inayojitokeza ni kuwa wanatekeleza kiwoga woga hawatekelezi vile inavyotakiwa ,matokeo yawepo mazuri kuwa masheha wakumbwe na vifo ,waandikishaji walipukiwe na mabomu.
Hapo ndio utaona kuwa mambo haya ni ya kupangwa na ni ya woga woga maana ikitokea mmoja wapo kukamatwa basi itakuwa ni aibu kubwa na hilo ndilo wanaloliogopa wale wanaopanga hila hizo ,eti wamewaona wakikimbia kwenye mashamba ya migomba.
Pemba Nchi ambayo imetawaliwa na kiza , ukisimama tu mtu hakuoni. Kichekesho nilichokiona kwa waliopanga habari za matokeo ni pale aliposema kuwa Sheha alikuwa amelala akasikia watu wanachimba nje ya nyumba yake akafungua mlango na kuelekea nyuma ya nyumba kufika huko watu walikuwa wakichimba ambao walikuwa wawili wakakimbia na mara ukatokea mripuko hapo ,sheha akaanguka na ukuta nao pia ukaanguka ,yaani ni hadithi ya paukwa pakawa ,panga upangavyo lakini kwa kitendo hiki sheha angepoteza maisha ,hakuna asieelewa mlipuko wa baruti za kupasulia miamba ,halafu unatwambia sheha amepona ,maana kiakili tu sheha lazima angesogea pale palipokuwa pakichimbwa kuona ni kitu gani kilikuwa kinachimbwa ,kwa waliokimbia lazima watakuwa wamesimama na kuona alietoka kama anawafuata au anafanya kitu gani ,jamani kama hamujui kupanga habari tukodisheni tuwapangie newz.