Tetesi: Maalim Seif under house arrest

Tetesi: Maalim Seif under house arrest

Status
Not open for further replies.
Mtazusha sana. Mara Jecha kafuta uchaguzi wa marudio, mara moto wawaka zanzibar, sasa house arrest!!! Kelele za mlango hazimnyimi mwenye nyumba usingizi. Uchaguzi utafanyika tu
 
Nyerere angekuwepo haya yasingetokea

Watu waliowekwa Ndani chini ya Nyerere kwa sababu za kisiasa ni wengi sana kuliko waliowekwa ndani na tawala zote zilizofuata.
Nyerere kuepuka kadhia kama hizi 1965 alipiga Marufuku vyama vyote vya kisiasa isipokuwa TANU na akafuta Uchifu kuepuka Changamoto za kisiasa walizokumbana nazo warithi wake.
Oscar Kambona alikimbizwa kwa kukataa Azimio la Arusha.
Christopher Kasanga Tumbo alifungwa kwa kupinga Vijiji vya Ujamaa n.k
 
Hii habari haiwezi kuwa yahakika!! Ni hatari sana na ni ya kichochezi...lah kama ni kweli,tutakua tunachezea utulivu tulionao.
 
Angekuwepo hai kina seif wangekua wamepotea siku nyingi sana. Enzi zile ndio ulikua udictator sio sasa.

Fuatilia historia. Mwl alifanya kazi na Maalim miaka ya 1980 wakati wa chama kimoja.

wakati wa kuchafuka kwa Zanzibar na kufukuzwa urais rais jumbe Maalim alikuwa kwenye safu ya uongozi.

Hata hivyo Maalim alipofukuzwa CCM na wenzake Mwl Nyerere alikuwa bado yupo.

Tukubali kitu kimoja licha ya huo udikteta wa mwl unaosema kama ulikuwepo Basi Mwl nyerere alikuwa mwana siasa aliyepikwa na kuiva. Asingefanya haya dhahiri hivi katika zama za vyama vingi.

Na wakati huo huo Dunia inashuhudia.

Mh Kolimba alishasema ...........CCM imepoteza mwelekeo...
 
Mtazusha sana. Mara Jecha kafuta uchaguzi wa marudio, mara moto wawaka zanzibar, sasa house arrest!!! Kelele za mlango hazimnyimi mwenye nyumba usingizi. Uchaguzi utafanyika tu

Uko sahihi! Labda kisimame Kiyama ndio kitasimamisha Uchaguzi au Mweneyźmung alete ghalika.
 
Huu uchaguzi na yanayoendelea zanzibar yanaichafua sana serikali ya Tanzania, sijui kwa nini wamwameamua kupoteza sifa ya nchi hii.
 
Huu uchaguzi na yanayoendelea zanzibar yanaichafua sana serikali ya Tanzania, sijui kwa nini wamwameamua kupoteza sifa ya nchi hii.
Hakuna lolote linaloendelea Zanzibar zaidi ya tishiatoto, we unatupa bomu kwenye nyumba isiyoishi mtu kijijini. angalia picha zinazosambazwa toka jana ni vurugu za 2012, angalia barua iliyowekwa leo ati Jecha kafuta uchaguzi propaganda za kitoto uchaguzi zinafanywa na watu wanaodai hawatashiriki uchaguzi!!
 
Hii ni kwa mujibu wa Mzalendo.net Zanzibar.

taarifa zinasema wengine wanaotakiwa kuwekwa ndani ni

Mh Mazrui
Edy Riyami
Mh Hamad Masoud ambaye leo asubuhi alikamatwa akiwa nyumbani kwake Zanzibar.

Imeelezwa lengo kubwa ni kupisha uchaguzi wa marudio.

stay tuned.

===========

Chanzo: Mzalendo.net
mkuu tunakushukuru kwa taarifa hii .
 
Haya kina jecha sibwalisema maalim bado ni mgombea halali sasa atafuatilia vipi matokeo yake kama atakua undr house arest .na atafanya vipi kampeni za mikutano ya ndani kama kweli jecha anasema ni mgombea halali
 
Watu waliowekwa Ndani chini ya Nyerere kwa sababu za kisiasa ni wengi sana kuliko waliowekwa ndani na tawala zote zilizofuata.
Nyerere kuepuka kadhia kama hizi 1965 alipiga Marufuku vyama vyote vya kisiasa isipokuwa TANU na akafuta Uchifu kuepuka Changamoto za kisiasa walizokumbana nazo warithi wake.
Oscar Kambona alikimbizwa kwa kukataa Azimio la Arusha.
Christopher Kasanga Tumbo alifungwa kwa kupinga Vijiji vya Ujamaa n.k
kama Nyerere angefanya hayo nyakati hizi bila Shaka angeishia waliko kina Laurent Gabbo, nyakati zimebadilika Zama za udikiteta zinatoweka kwa kasi
 
Sasa mmelazimisha kuwafanya wagombea wakati wao waliisha sema mfute majina yao, hawatahusika katika uchaguzi, leo hii mnawafunga wagombea, yaani hata wasijipigie kura? au mtawapelekea kituo cha kupiga kura majumbani mwao, wengine ndani ya cero!
 
Enyi wazanzibari kuweni wenye fikra pevu,mnaempigania anakula kula bata batani nyie mnachezea moshi wa mabomu na virungu (Serena hoteli).

Kisha uza uchaguzi anazuga tu.
 
Zenji hali ni tete watu walio kinyume na ccm wanatekwa au wanakamatwa live wanakula kichapo cha haja kisha wanafunguliwa mashtaka ya kutunga huku sisi tunamkenulia meno Magu....hivi hii ndio ile ahadi yake ya kusema kuwa atahakikisha Zanzibar inakuwa salama! ? Kwa mtindo huuu!?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom