Tetesi: Maalim Seif under house arrest

Tetesi: Maalim Seif under house arrest

Status
Not open for further replies.
Hii ni kwa mujibu wa Mzalendo.net Zanzibar.

taarifa zinasema wengine wanaotakiwa kuwekwa ndani ni

Mh Mazrui
Edy Riyami
Mh Hamad Masoud ambaye leo asubuhi alikamatwa akiwa nyumbani kwake Zanzibar.

Imeelezwa lengo kubwa ni kupisha uchaguzi wa marudio.

stay tuned.

Chanzo: Mzalendo.net

UWIKE USIWEKE KUTAKUCHA.

KIMSINGI SERIKALI YA CCM IMEFANYA HUGE TECHNICAL ERROR AMBAYO HATA KAMA CUF WANGESEMA WANASHIRIKI UCHAGUZI NA WAKASHINDWA KWA HALALI, BADO CHAGUZI UNAENDELEA KUWA BATILI KWA SABABU KUU ZIFUATAZO PAMOJA NA NYINGINE NYINGI TU.

1. JECHA ALITUAMBIA TUME ILIFARAKANA NA HAJARUDI KUTUAMBIA LINI ILIPATANA TENA NA KUWEZA KUSIMAMIA UCHAGUZI UKAWA WA BILA DOSARI KULIKO WA AWALI, MBALI YA KUMWONA YEYE TU TENA CHINI YA ULINZI MKALI NA MAFICHONI.
2. KATIBA INATAKA UCHAGUZI WOWOTE WA MARUDIO IKIWA NA MAANA MTU AKILALAMIKA NA UKARUDIWA KWA AMRI YA MAHAKAMA, UWE UMEFANYIKA NDANI YA SIKU 90. HUU WA JECHA NI ZAIDI YA SIKU HATA 120 MIEZI 4, BATILI KUBWA
3. WOTE TWAJUA BILA CUF HAKUNA CHAMA CHENYE AT LEAST 10% KWA HIYO CCM WATAAMUA GAWA ILI KULIDIA MATAKWA YAO.
4. WAMELAZIMISHA KWA NGUVU MAJINA YA WAGOMBEA WA CUF KUENDELEA KUWAPO PAMOJA NA WAO KUJITOA KWA WAZI NA TARATIBU WALA BILA UGONVI. SWALA NI KUWA WAKISHINDA CUT NA HAWAKO TAYARI KWENDA KWENYE BARAZA LA WAWAKILISHI WATARUDIA AMA WATAPELEKA WA CCM.

NINAWAOMBA HATA WABUNGE WA CUF/UKAWA KWA JUMLA WALIOPO KWENYE SERIKALI YA MUUNGANO WAJITOE WAACHIE CCM WAENDELEE TAWALA KAMA HILI HALIPATIWI UFUMBUZI WA KIDEMOCRASIA.

DUNIA NZIMA INAYAONA HAYA NA HATA WALAZIMISHE HATA WATANZANIA WANAJUA ZANZIBAR RAIS NI MAALIM SEIFU.

RAIS MAGUFULI PAMOJA NA KAZI NZURI SANA ANAYOFANYA KWA MAMBO MENGINE, HAKIKA HILI LITATIA DOA KUBWA SANA HUENDA LITAFUNIKA MENGINE YOTE. SUBIRINI MUONE AS DAYS GOES BY.

Mtazusha sana. Mara Jecha kafuta uchaguzi wa marudio, mara moto wawaka zanzibar, sasa house arrest!!! Kelele za mlango hazimnyimi mwenye nyumba usingizi. Uchaguzi utafanyika tu
nasikia mwenye mavi hazuiwi kujinyea !!!

Nijui ingekua next move, mfano akitangazwa rais inakuje??

Angekuwepo hai kina seif wangekua wamepotea siku nyingi sana. Enzi zile ndio ulikua udictator sio sasa.
Ila enzi hizo ulikua mfumo wa chama kimoja,
Tulikubali ndoa ya vyama vingi lazima tufuate masharti yake

Kuna ukweli wowote kwenye hii habari?

Mods, Jiridhisheni kwanza kabla ya kuacha huu uzi uendelee.

Matukio yafuatayo ni dalili ya kukomaa kisiasa kwa chama pendwa cha CCM katika misingi ya haki na demokrasia.
1-Kutumia jeshi la polisi kufanya mauwaji ya january 27 2001 Pemba,kwa waandamanaji.
2-Daudi mwangosi kufia mikononi mwa polisi
3-Kukamatwa kwa viongozi wa CCM wakiwa na masunduku feki ya kura,akiwemo waziri mkongwe Nagu huko Manyara ktk uchaguzi wa 2015
4-Kuahirishwa pasipo sababu ya msingi kwa uchaguzi wa meyor wa jiji la Dar es salaam na hatimae kufoji(jinai) hati ya mahakama na kuweka zuio feki
5-Kuwakamata na kukifungia kituo cha tallying station cha CDM hali wenyewe wakiwa na kituo kama hicho kwenye uchaguzi wa 2015
6-Kufuta uchaguzi wa Zanzibar kama vile wanamfuta mtoto uji shavuni, bila kufuata utaratibu huku wakidai wanataka uchaguzi safiiiii usio dosari na wakati huohuo wakiseka lupango wafuasi wa CUF zoezi linaloendelea hadi leo hii..
7-Kutumia lugha kama vile..CCM HAITONG'OKA KIRAHUSI KAMA JINO,WAPINZANI WASAHAU KUINGIA IKULU,HATUTOFANYA KOSA KUKABIDHI IKULU KWA WAPINZANI..

asante mungu kwa kuendelea kutuletea machaguo yako !

Watu waliowekwa Ndani chini ya Nyerere kwa sababu za kisiasa ni wengi sana kuliko waliowekwa ndani na tawala zote zilizofuata.
Nyerere kuepuka kadhia kama hizi 1965 alipiga Marufuku vyama vyote vya kisiasa isipokuwa TANU na akafuta Uchifu kuepuka Changamoto za kisiasa walizokumbana nazo warithi wake.
Oscar Kambona alikimbizwa kwa kukataa Azimio la Arusha.
Christopher Kasanga Tumbo alifungwa kwa kupinga Vijiji vya Ujamaa n.k
Ukiwa Kiongozi huwezi kuwaacha Vichwa maji hasa wanaokwenda kinyume au kupinga Vision na Malengo yako (ambayo ni mazuri kwa Maslai mapana ya Taifa), ukawaacha waendelee kuota kama uyoga.
You have to bind, or to finish them, maana wengine wanapinga Uongozi wa mtu si kwa nia njema bali ni kutaka kutekeleza maovu yao.

Sasa hao wanafanya nini??Kwa kuwashikilia ndiyo wanasababisha kadhia zaidi
Mkuu yaani nashindwa kuelewa washauri wa viongozi wetu yaani hawaoni kama kuwashikilia hao ndio wanaamsha hisia za wafuasi wao?hivi shein anaogopa kitu gani wakati uchaguzi anashiriki pekee yake?

Hii ni kwa mujibu wa Mzalendo.net Zanzibar.

taarifa zinasema wengine wanaotakiwa kuwekwa ndani ni

Mh Mazrui
Edy Riyami
Mh Hamad Masoud ambaye leo asubuhi alikamatwa akiwa nyumbani kwake Zanzibar.

Imeelezwa lengo kubwa ni kupisha uchaguzi wa marudio.

stay tuned.

Chanzo: Mzalendo.net
hakuna marefu yasio na ncha...iko cku watoto zao au wajukuu zao watapitia hayahaya......

Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom