Maamuma's Thread:Inakuwaje ikiwa....

Maamuma's Thread:Inakuwaje ikiwa....

Wanajamii naomba kuweka hii mada hapa ambayo maamuma alikuwa ameipost katika thread ya "The Remainder....) Nadhani inastahili kuwa thread mpya kwa heshma na taadhima naomba niiweke hapa kwa niaba ya Maamuma.(Samahani kama nitakuwa nimekosea)

WanaJF, naomba mnipe ufumbuzi wa tatizo ambalo lipo miongoni mwa baadhi ya wanandoa. Ntafananisha ndoa (mke na mume) kama kufuli na ufunguo. Kimaadili ni kwamba huruhusiwi kukutana kimwili na mchumba wako hadi siku ya ndoa (au baada ya ndoa). Sasa inakuwaje unapokuja kugundua kwamba kufuli ulilochukua haliendani na ufunguo wako? Nina maana ya majambo ya chumbani. Mtu huruhusiwi kujaribisha ufunguo kama unafunguaje kufuli, labda kwa taabu au unapwaya au hadi uweke grisi. Hapo nadhani ndio mwanzo wa mtu kwenda nje kutafuta kufuli linaloendana na ufunguo. Vinginevyo uhusiano wa chumbani unakuwa na upungufu kama huo wa pasi kuchelewa kuwaka au haiwaki kabisa. Balbu nayo inapata shoti mara kwa mara. Mnasemaje kuhusu hili? Tuendelee kuelimishana.
Umeandika Fasaha sana, hongera yako, lakini kitamaduni inatakiwa mwanamke aolewe akiwa na (seal) wajuvi wa mambo wanasema mwanamke aliyeolewa hivyo mara nyingi huridhika na kile kitakacho kuwa offered siku hiyo na baade.
Lakini wengi wao wanakuwa wameguswa sana, wameshaona Kila aina ya ufunguo, huyo anaeambiwa mpaka ndoa kwa kweli ni kama kapigwa vumbi la macho. Siku hiyo ufunguo ukiingia linakutwa bwawa.
Ama ufunguo kuwa mkubwa hiyo ni kwenda hospitalini na kupata nasaha.
 
Back
Top Bottom