Maamuzi gani mabaya uliwahi kuyafanya yakakugharimu?

Maamuzi gani mabaya uliwahi kuyafanya yakakugharimu?

kitalembwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2014
Posts
3,607
Reaction score
9,430
Wasalaam,

Kwenye maisha Kuna kukosea, ni jambo/mambo gani ulishawahi kuyafanya ukabakia kujuta Sana?

Binafsi niliwahi kufanya yafuatayo!

1. Mwaka 2018 Kuna shamba Kama hekari 4 zilikuwa zinauzwa mahali, nikafika Bei vizuri mpaka process za kwenda kwa serikali za mitaa kukamilisha deals zikaanza, akatokea mwana mmoja akanistua Kuna mishe flan (business ya kupiga chap) nikaghairi, ile hela tukafanya lile dili, return Yale haikuwa nzuri kiviiile Bora ningenunua tu shamba!

Lile shamba jamaa mmoja akalinunua, now Kuna mradi flani serikali imepeleka pale, Yani barabara ndo imetenganisha tu! Now lile eneo limegeuka hot cace! Hapanunuliki, jamaa alienunua alikata vipande vipande akauza 20*40 , eneo lingine ameweka frame pia kwa nyuma anajenga Lodge, najuta Sana kwa Yale maamuzi!

Kisa kingine, Kuna sehemu palikuwa chimbo zuri la kisasa(bar) na lodge, Ni sehemu panahit Sana, mmiliki wake ni boss flan serikalini, safari nyingi haziishi, hata muda wa kupafatilia vizuri akawa anakosa, wakawa wanampiga Sana! Siku moja tumekaa mahali Kama utani akanigusia pale wanampiga Sana, anatafuta mtu amkodishie jumla, lodge na hio bar! Yeye aendeshe anavyojua apate riziki alipe na wafanyakazi, kwa hela alionitajia niliona nyingi Sana maana sikuwahi kufanya hii shughuli before! Nikampotezea akaona sieleweki, Kuna jamaa akapachukua, aloo jamaa katusua mbaya!

Kuna visa vingine vidogo vidogo Kama elimu niliosomea🤣, mambo ya mapenzi, kukopeshana hela na washkaji n.k! Lakini hivyo viwili najuta Sana, wewe ni maamuzi gani uliwahi kufanya now yanakugharimu/unayajutia??
 
Every life experience (good/bad) is a lesson in it's own way...
 
Nilimla msichana kwa dharura siku moja tu, bila kinga. Akanasa.Babake hadi leo hatusalimiani japo ni miaka 22 sasa imepita.
 
Nilikataa kazi ya afisa kodi TRA kisa ni loan officer bank flani kipindi cha corona nikapunguzwa
 
Back
Top Bottom