Maamuzi Magumu: Nimeamua kuwa baba wa mtoto wa rafiki yangu

Kweli nimeamini wanga wapo.
Mleta mada keshasema na kaweka wazi.
Kuwa yeye ana hudumia kijacho na mtoto atamhudumia na kumtayarishia maisha ya badae mtoto atakayezaliwa.
Inaonekana wengi hawajui nini maana ya ubaba.

Mwanamke awe malaya arudi kwa baba mtoto yeye havimhusu.
Yeye analea mimba na mtoto tu.
Dunia ya sasa ni ngumu kiasi hiki mpaka msiamini haya?

Kuna wanaume kibao wanaolea, kusomesha na kuwajengea watoto ambao si wa kwao na hawajui hata wametokea wapi ni just wameamua kuwapa furaha watoto hao na kuwatayarishia maisha ya baadae.
 
Il in reality ni ngumu sana kufanya hayo bila mama kutaka mahusiano na wewe
Wanawake wengi tunashindwa kutenganisha hilo.
Mwanaume akimpenda mtoto na akiwa wa karibu na mtoto automatically unajikuta upendo umejengeka, upendo ukiwepo wivu lazima uwepo.
Ni ngumu sana kutenganisha mapenzi hayo.
Wewe utakuwa na msimamo huo mwenzako ataanza kucatch feelings.

Mitego itaanza.

Kama ulichoandika ndo utakachofanya simama kwenye nafasi yako ukirudia kula tunda tu utaharibu kila kitu na future ya huyo mtoto.
 
Amini kua,una seat yako mbinguni
Mungu akubariki mno
 
Watu wana roho mbaya sana
 
Ulivutiwa nae mlipokutana ofisi flan,mkatongozana na mkakulana.

Akaenda kwa mpenz wake nche ya nchi kakuacha unamsubiria arudi

Wakazinguana na mpenz wake akarud na kabla hajakufikia akakutana na njemba ikambandua na chata ikaacha.

Akarudi kwako na badae akakwambia ana ujauzito na umekubali kuulea na kua baba wa hiari na et hautakua na mahusiano nae kimapenzi tena...jombaa zinduka huko usingizini hii Mambo ata ungekua malaika ni ngumu kueleweka..ningeamin Kama tu hamkuwahi kua na mahusiano Cha mhimu akijifungua Lea mtoto na badae piga na wewe chata yako hapo Mambo yatabalance.
 
Nilikuwa na kawaida ya kwenda kwa bro weekend. Mke wa bro ambaye ni shemeji yangu tulikuwa marafiki San. Shem alkuwa na marafiki zake watatu walioshibana hasa.
Mimi nikamzoea sana mmoja, tumpe jina la Mwajuma. Alikuwa ni mkimya sana weekend hiyo tofauti na nilivyomzoea. kama mwenye mawazo sana. Nikamuita shem pemben kuteta, kumuuliza mbona mwajuma leo anaonekana hayuko poa.

Shem akaniambia dogo kaharibu kwao. Amefukuzwa ana mimba. Nikiri taarifa ya shem ilinimaliza kabisa, kwani nilishaanza mpango wa kuwa nae mwajuma.
Nikamuomba mwajuma anipe nafasi ya kuongea nae.
Alinielezea kuwa mpenzi wake amemfukuza sababu ya mimba. Hataki hata kumuona. Mwajuma akaanza kulia nikamuacha alie kwanza.

Nikawa najiuliza kwann jamaa amfukuze demu wake sababu ya mimba? Au huyu dogo mwingi? Nikamsubiri amalize kulia

Itaendelea
 
Itaendelea lini sasa
 
Hujui ya ulimwenguni ndugu, damu ni nzito kuliko maji. Damu isiyo yako lazima uwe na kiasi na mipaka juu yake kwani mwisho wa siku lazima ujute sana.

Ninachoweza kusema hukujipa nafasi ya kutafakari kuhusu uamuzi wako, ama ulifanya maamuzi kwa mihemko yako ama kwa sababu kwa sasa unaona huna majukumu zaidi.

Mwisho wa siku vipi akipata ujauzito wa mtoto mwingine kwa MTU mwingine, pia utaendelea kulea ama umeamua awe mke wako!! Kuna mengi ya kutafakari na si kukurupuka. Si swala jepesi kama unavyoweza kufikiri.

Pia jiangalie sana huyo mwanamke ni mwepesi sana na wewe ni mgeni kwenye maswala ya mahusiano na malezi
 
Alikuwa mjamzito mara ngapi..???View attachment 1539890
Mbona inaeleweka? Kwenye paragraph ya mwanzo bidada alimjulisha tu kuwa ni mjamzito ila hakumpa habari nyingine na huenda mtoa mada alijua ametoka nayo kwa mchumba wake...baadae akaja akamsimulia jinsi mambo yalivyokuwa na hadi kupata ujauzito
 
Reactions: amu
dah asante sana kwa hii mada, maana mimi ni mtunzi wa simulizi, hiki kida chako kitafaa sana kuchezewa muvi ya bongo muvi

sipati picha wewe nafasi yako asimame ray ama gabo zigamba, nomaa bado staa wa kike awe huyo rafiki yako, nadhani hapo kajala atafaa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…